RAY, STEVE NYERERE WANAFIKI WAKUBWA'

Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.

STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kusema kwamba, wasanii wenzake Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ ni wanafiki wakubwa baada ya kumtosa kwenye Pati ya Instagram iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.
Staa wa filamu Bongo,Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Akizungumza na paparazi wetu, Wema alisema alikubaliana na mastaa hao kutoenda kwenye Shoo ya Zari All White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar badala yake waongozane naye jijini Mwanza lakini wakamgeuka.
“Sitaki kabisa nisikie mtu ananiambia habari ya Steve Nyerere au Ray maana ni wanafiki wakubwa, hawawezi kuniahidi kutokwenda pati ya Zari lakini wakaenda na wasije Mwanza kama walivyoniahidi,” alisema Wema.Paparazi wetu baada ya kupata malalamiko ya Wema, alimsaka Steve ili aweze kuzungumzia unafiki wao, akafunguka:
“Kweli mimi na Ray tuliahidi kuungana na Wema kwenye shoo yake ya Mwanza ila siku ya mwisho tulikwama baada ya kupungukiwa fedha ya nauli, hivyo tukashindwa kabisa na tusingeweza sisi kwenda huko kwa kumtegemea yeye atulipie kila kitu.Tukaona twende kwa Diamond ambaye naye alitualika.” Ray hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tuhuma hizo.

ADAIWA KUBANJUKA NA AUNT, BAADAE ALIAMUA KUJITOSA KWA LULU - 7


JUMAMOSI iliyopita tuliishia pale nguli wa sinema za Kibongo, hayati Steven Kanumba alipoanzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo aliyetwaa taji la Miss Kinondoni, Sylvia Shally.
SASA ENDELEA...
Walipendana sana, kama ilivyokuwa kwa wapenzi wake waliotangulia, vyombo vya habari vilianza kuwafuatilia lakini wenyewe hawakujali. Walipendana sana. Kwa kipindi cha mwaka mmoja waliishi kama bibi na bwana.Baadaye nao walianza kugombana mara kwa mara. Maisha yao yalimulikwa kila wakati na vyombo vya habari.
Kuna wakati Kanumba alikwenda Marekani, Sylvia alibaki nyumbani Tanzania. Kipindi hicho vyombo vya habari vilizidi kueneza habari za kutatanisha kuhusu uhusiano wao. Kuna wengine walisema wameshamwagana lakini wengine wakasema bado.Lakini kama ilivyokuwa kwa Wema na Nargis, ilifika wakati Sylvia na Kanumba nao wakamwagana.
AKOMAA
NA FILAMU
Kazi na dawa, baada ya kuachana na mrembo huyo, Kanumba alielekeza nguvu zake katika kurekodi sinema. Akatoa sinema kama Fake Smile, Unfortunate Love ambayo aliigiza na wakali kama Aunt Ezekiel, Lisa Jensen na Zamda Salum.
Sinema hiyo ilikuwa gumzo kutokana na kuzungumzia jinsi gani mtu unaweza kumtamani mtu ndani ya dakika moja, inahitaji saa nzima kumpenda mtu, inahitaji siku nzima kumuenzi mtu lakini inahitaji maisha kutomsahau mtu.
Baada ya muvi hiyo akatoa, Hero of The Church ambayo ilikuwa na mafundisho ya dini. Kanumba akiwa kama mhusika mkuu, alionesha anapambana na wazee wanaowadanganya waumini na kufichua ukweli wa mambo.
Mwendo wa kurekodi sinema ukaendelea, akatoa Saturday Morning, Crazy Love, More Than Pain, Uncle JJ, This is It, Off Side, Deception, Young Billionaire na Devil Kingdom ambayo ameigiza na mwigizaji mkali kutoka Nigeria, Ramsey Nouah.
Filamu hiyo imeonesha uwezo wa nguvu za shetani. Nguvu ya giza ilitumika kushawishi watu waamini muujiza wa Mungu lakini mwisho wa siku ukweli ulijulikana kwamba Mungu anabaki kuwa Mungu na ndiye anayeweza yote.
ADAIWA KUBANJUKA NA AUNT EZEKIEL
Wakati akiendelea kufyatua sinema, Steven alidaiwa kuanzisha uhusiano wa siri na muigizaji Aunt Ezekiel. Uhusiano huo ulifichwa sana na hata vyombo vya habari havikuweza kuambulia.
AJITOSA KWA LULU
Mwaka 2012, uhusiano wa Aunt na Kanumba haukudumu sana, akahamishia majeshi kwa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18.Kama ilivyokuwa kwa Aunt, uhusiano wa Lulu na Kanumba nao ulikuwa wa siri.
Vyombo vya habari havikuwa na la kusema hadi siku ya kifo cha Kanumba. Lulu akakiri kuwa walikuwa wapenzi baada ya tukio hilo na walikuwa chumbani pamoja wakati wa kifo chake.
Vyombo vya habari vikaanza sasa kuripoti mambo mbalimbali yaliyokuwa yamejificha kati ya wawili hao. Mwigizaji huyo alifunguliwa mashtaka ya kuua bila kukusudia ambapo kesi inaendelea hadi sasa.

LULU AMGANDA VAN VICKER KISAWASAWA

Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na mwigizaji kipenzi wa akina dada wa Ghollywood Movies kutoka nchini Ghana, Van Vicker.
Habari kutoka chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu kilidai kwamba, mwanadada huyo amekuwa na mawasiliano ya karibu na Van Vicker tangu walipokutana Septemba, 2013 kwenye Jengo la Akade, Posta jijini Dar ambapo jamaa huyo alitua nchini kurekodi filamu na mastaa wa Bongo.
“Kwa taarifa yenu Lulu sasa hivi mambo yake na Van Vicker ni bambam na wanawasiliana usiku na mchana, nadhani kuna kitu kikubwa kinakuja. Yaani Lulu amemganda jamaa japokuwa sijajua kamili kama wana project gani.
“Kama mtakumbuka kipindi kile Van Vicker alikuja Bongo kucheza filamu ya Hashim Kambi (mwigizaji wa Bongo) ndiyo walifahamiana.
“Inawezekana anataka kufanya naye kazi kama Wema (Sepetu) ambaye hivi karibuni alikwenda Ghana na picha zikasambaa wakifanya yao,” alisema mtu huyo kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilizungumza na Lulu juu ya ishu hiyo ambapo alikiri kuwa ni mtu wake wa karibu na kwamba ni kweli amekuwa akiwasiliana naye.“Van Vicker ni mtu wangu, nimekuwa nikiwasiliana naye, kusalimiana na kuulizana maendeleo ya kazi zetu za sanaa,” alisema Lulu.

MAFURIKO YAWALIZA MASTAA WA BONGO

Adha ya mafuriko jijini Dar.
Wakizungumza na gazeti hili juu ya majanga hayo ya mafuriko yaliyowakumba hasa watu waishio mabondeni, mastaa hao walikuwa na haya ya kusema:
WASTARA JUMA:
“Mafuriko yameniathiri kwani niko karibu na Mto Msimbazi (nyumbani kwake Tabata) hivyo hata kutoka nyumbani naogopa kwa sababu ya watoto. Nyumba ninayoishi kuna mfereji niliochimba nje, ukijaa maji yanaingia kwenye vyoo ndani, shida tupu.”
AUNT EZEKIEL:
“Niko tu ndani (Mwananyamala) siwezi hata kutoka kwenda popote kwa sababu maji yamejaa kila sehemu, nimesimamisha shughuli zangu kwa sababu barabara zenyewe hazipitiki, ukweli hii mvua imeathiri sana.”
YOBNESH YUSUF ‘BATULI’.
YOBNESH YUSUF ‘BATULI’:
“Ukweli naipongeza sana serikali kwa miundombinu mibaya, bungeni kila mwaka wa bajeti zinapitishwa mamilioni ya fedha lakini miundombinu mibovu, mafuriko kila sehemu nyumbani (anaishi maeneo ya Sinza) ni shida.
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
“Namshukuru Mungu nyumba yangu ipo mlimani (anaishi Jet-Lumo) maji hayajaingia ndani lakini hali ni mbaya kwani siwezi kutoka kwenda kwenye shughuli zangu, mipango yote imekufa nashinda ndani tu na familia.“Watoto hawajaenda shule, walimu walitupigia simu wakasema wasiende kutokana na hali halisi ya mafuriko.”
AUNT EZEKIEL.
MAYASA MRISHO ‘MAYA’:
“Huku ninakoishi (Msasani) maji yamejaa kweli kila sehemu, hakuna pa kupita huko kwa mama yangu Magomeni sijui itakuwaje maana ndiyo zaidi, serikali inatakiwa iliangalie suala hili na kulitatua kwani hii yote inatokana na miundombinu mibovu.”

WEMA ANABWIA UNGA AMEKANUSHA MARA KIBAO KUHUSIANA NA MADAI HAYO

Supastaa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Madam’.
UBUYU WAVUJISHWA
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wema amekuwa akitumia kilevi hicho kwa muda mrefu huku akifanya jambo hilo kwa siri kubwa.“Hivi hamna habari ya Wema kubwia unga? Mbona kila mtu anajua, watu wengi tu wanafahamu lakini wanashindwa namna tu ya kumueleza mwenyewe ili aache maana kila mtu anamhofia si unamjua naye Madam mtu wa kumaindimaindi,” kilisema chanzo hicho.
MITANDAO YAKAZIA MADAI
Kama hiyo haitoshi, kwa nyakati tofauti, watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakidai kuwa staa huyo anabwia unga licha ya kuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja.“Mimi sijawahi kumuona lakini kuna watu wake wa karibu tu wananihakikishia kwamba Wema anatumia madawa ya kulevya, ila naamini mwenyewe anaujua ukweli wote wa haya yanayosemwa,” ilisomeka sehemu ya maoni mtandaoni.
RISASI LAMFUNGIA KAZI
Baada ya kupata madai hayo, Risasi Jumamosi lilimfungia kazi Madam ili kuweza kumsikia anazungumziaje tuhuma hizo nzito.
Jumatano iliyopita, mwanahabari wetu alikwenda nyumbani kwa mwigizaji huyo mwenye mvuto wa kipekee, Mtaa wa Bwawani-Kijitonyama lakini bahati mbaya alikuwa ametoka kwenda kurekodi na hata alipofanya subira hadi jioni, bado hakurejea huku simu yake ikiita bila kupokelewa.
JITIHADA ZAIDI
Siku iliyofuata, mwanahabari wetu aliyeambatana na mmoja wa wahariri wa Global Publishers, walitia timu kwa mara nyingine nyumbani kwa Madam lakini pia mwigizaji huyo alikuwa ametoka lakini bahati nzuri alipopigiwa simu alipokea, mambo yalikuwa hivi:Risasi: Wema tumekutafuta sana hapa nyumbani kwako bila mafanikio tuna ishu ya msingi kweli tunataka kujua kutoka kwako?
Wema: Poleni, ishu gani?
Risasi: Tumepokea habari kuwa wewe unatumia madawa ya kulevya,  umewahi kusikia hizi habari?
Wema: Ndiyo hizo habari nimewahi kuzisikia. Nakumbuka nilianza kuzisikia tangu kipindi kile mimi natembea na CK (yule kigogo wake), walivumisha sana lakini hakuna ukweli wowote.
ADAI WAMEMPONZA
“Tena imefika wakati wananikosesha hadi amani, imenifanya hadi niwe nakaguliwa kupindukia bila sababu za msingi, juzi hapa wakati naenda Mwanza (kwenye shoo ya Instagram), walinibana sana pale Air Port hadi nikataka kuachwa na ndege.
Wema Sepetu ‘Madam’.
AISHI KWA TAHADHARI
“Yaani kwa sasa nimelazimika kuweka hadi ulinzi mkali pale nyumbani, maana huwezi jua watu wasionipenda wanaweza kuja wakanibambikia nikaonekana natumia kumbe sijui hata ukoje. Sasa hivi kila atakayeingia lazima akaguliwe, ahojiwe ndipo aingie.
ATAJA KUHUSISHWA NA ROMMY
“Kuna wakati walinitaja kuwa natumia kwa kuwa nina ukaribu na Rommy Johnson (binamu yake msanii Diamond) kitu ambacho nilikikanusha na ninaendelea kusema hakuna ukweli wowote.
MAMA’KE ARIPOTI POLISI
“Ili kuwataka watu wasinihusishe kwa namna yoyote na kujihadhari, tuliongea na mama, akaenda kutoa taarifa polisi Mabatini ili nisije kupata tatizo lolote linalohusishwa na madawa ya kulevya.”
RAFIKI ZAKE WANENA
Mwanahabari wetu aliwavutia waya marafiki wa Wema, Aunt Ezekiel na Martin Kadinda ambaye ni meneja wa mwigizaji huyo ambao kwa pamoja walidai hawajawahi kumuona Madam hata siku moja akibwia unga achilia mbali kukaa karibu na wabwiaji.
“Sijawahi kumuona Wema hata siku moja anatumia hivyo vitu (unga), watakuwa wanamzushia ili watimize azma yao ya kumchafua si unajua si wote wanampenda?,” alisema Aunt huku Martin akikazia:“Hakuna kitu kama hicho, Madam hatumii bwana, sisi tupo naye, tunafanya naye kazi siku zote, hatujawahi kumuona, huo ni uzushi tu.”

STARTIMES YAWAPIGA TAFU WANAFUNZI UHURU MCHANGANYIKO

Msanii wa Bongo Flava na balozi mpya wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Nurdin Bilal au maarufu kama Shetta (kulia) akimkabidhi msaada wa vyakula mbalimbali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam, Bi. Anna Mshana (kushoto). Kampuni hiyo ilitembelea na kutoa msaada wa vyakula kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo ina kitengo kinachofundisha wanafunzi wenye ulemavu. Pamoja naye kutoka kushoto ni wafanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Elena Liu na Bw. Richard Yan.
Msanii wa Bongo Flava na balozi mpya wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Nurdin Bilal au maarufu kama Shetta akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati kampuni hiyo ilipotembelea na kutoa msaada wa vaykula kwa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana.
Dar es Salaam, Mei 6, 2015.
Katika kuijali jamii ya watanzania ambao ndio wateja wake wakubwa, kampuni ya usambazi na uuzaji wa ving’amuzi nchini, StarTimes Tanzania, imetembelea na kutoa msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 3.5 kwa wanafunzi wenye ulemavu, shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vyakula vilivyotolewa shuleni hapo ni mchele zaidi ya kilo 200, unga zaidi ya kilo 150, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi, sabuni za kupikia na vinginevyo.
Akizungumza baada ya kupokea masaada huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Anna Mshana alishukuru sana kwa msaada huo kwani wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na StarTimes ni mara ya pili kwenda shuleni hapo.
“Hii ni mara ya pili kuja hapa kwani mara ya kwanza walituletea luninga na king’amuzi ambacho tunakitumia mpaka hivi leo. Hivyo StarTimes ni kama walezi wetu naweza kusema kwani tukiwa na tatizo tunawaona na kutusaidia. Mimi sina cha ziada zaidi ya kuwashakuru kwa moyo wao wa kutukumbuka kila wanapofanya shughuli zao.” Alisema Bi. Mshana
“Shuleni hapa tunawanafunzi wa kawaida lakini pia kuna walemavu wa ngozi (albino), , viziwi, vipofu, wenye ulemavu wa akili na ulemavu mwingine. Wanafunzi hawa tuna hapa, tunawafundisha na pia wana mabweni yao ambayo ndimo wanapokaa. Chakula ni kitu muhimu kwao kwani ndio kinawapa motisha ya kuhudhuria na kupenda kusoma zaidi. Hivyo msaada huu umekuwa mwokozi wetu mkubwa kwa wakati huu.” Alimalizia mwalimu mkuu huyo
Kwa upande wake akizungumza na wanafunzi na uongozi wa shule, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif amesema kuwa wanajisikia wenye wajibu mkubwa kusidia jamii inayowazunguka kwani wapo kwa ajili yao.
“StarTimes tunajisikia kuwajibika kwa jamii inayotuzunguka na ambao ndio wateja wetu katika shughuli zetu. Linakuwa si jambo la busara kuendesha shughuli zako huku hauna msaada wowote kwa jamii yako. Leo tumejumuika hapa na msanii huyu wa muziki wa kizazi kipya kushirikiana kuwafariji wanafunzi hawa wenye uhitaji maalumu ili waweze kusoma.” Alisema Bi. Hanif
“Najua hata kama ningekuwa mimi ni mzazi wa mmojawapo wa watoto hawa ningefurahi kuona kuwa kumbe kuna watu wanawajali na kuwatambua watoto wao. Suala hili linatia faraja na hata kuwapa moyo wazazi ambao wana watoto wa namna na kuwaficha majumbani mwao kwa kudhani kuwa hawawezi kufanya jambo lolote. Ningependa kuwaambia kwamba wasiwanyime watoto wao fursa ya elimu au ya kujichanganya na watoto wenzao kwani kuzaliwa mlemavu si sababu ya kutoweza kufanya jambo lolote.” Aliongezea
“Hivyo basi wanafunzi na uongozi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko nawaomba mpokee kidogo hiki tulichwaletea ili kiweze kuwasaidia katika shughuli zenu za kimasomo. Napenda kuwatoa hofu kuwa msisite kutushirikisha pale mnapoona tunaweza kuwasaidia. Natoa wito kwa watu wengine kujenga utaratibu wa kuwakumbuka na kuwasiadia watu wenye uhitaji maalumu kama watoto hawa. Ninaamini watanzania ni wakarimu na watu wa kusaidiana siku zote.” Alihitimisha Bi. Hanif

AUNTY LULU ASEMA MAKALIO YANANITESA MAANA WANAUME WANAMTAKA KINYUME NA MAUMBILE

MWIGIZAJI Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ametoa kioja cha aina yake baada ya kuibuka na kusema kuwa makalio yake yanamtesa akidai anasumbuliwa sana na wanaume wanaovutiwa nayo faragha.
Mwigizaji Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Aunty Lulu alisema wanaume wengi wamekuwa wakimiminika kutaka baada ya kusambaziana kuwa mwigizaji huyo analitumia umbo lake ndivyo sivyo.
“Nawaomba wanaume waache kunifatafata jamani wananikosesha amani kwani mimi nimefundwa  najua madhara ya hako kamchezo kabaya, siwezi kuthubutu hata  mara moja,” alisema Aunty Lulu.

BOKO HARAM YASHAMBULIA CHUO NIGERIA, 12 WAJERUHIWA VIBAYA

Shambulio la Boko Haram nchini Nigeria.
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram, amefanya shambulizi la kujitoa mhanga katika Chuo kimoja cha Masomo ya Uongozi wa Biashara nchini Nigeria na kuwajeruhi wanafunzi kadhaa.
Tukio hilo limetokea jana Mei 8, 2015 baada ya mtu huyo kuvuka geti na kuingia ndani ya chuo hicho na kutekeleza shambulio hilo kwa kufyatua risasi kisha kujilipua kwa mabomu.
Madhara ya shambulio la Boko Haram nchini Nigeria.
Vyombo vya habari nchini Nigeria vimeripoti kuwa, shambulizi hilo lilifanyika katika Chuo kimoja cha Masomo ya Uongozi wa Biashara kilichopo mji wa Potiskum katika jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Katika shambulio hilo, watu 12 wanasemekana kujeruhiwa wakiwemo wanafunzi wa chuo hicho na wengine wakiwa katika hali mbaya.
Hii ni katika hali ambayo mtu mwingine aliyekuwa amejifunga mabomu amepoteza maisha baada ya mabomu hayo kumripukia kabla ya kufika eneo alilokusudia kufanya shambulio.
“Tumewaona watu 12 waliojeruhiwa vibaya na shambulio hilo ambao wamepelekwa hospitali kwa matibabu”.
“Tulikuwa ndiyo tumeingia darasani kuanza vipindi, tukasikia milio ya bunduki kutoka kwenye usawa wa geti la kuingia chuoni, hapo tukagundua kuwa tumevamiwa ndipo kila mtu akaanza kukimbia kutoka darasani ili kunusuru maisha yake” Tijjani Musa, alisema.
Ingawa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mashambulizi hayo, lakini polisi ya Nigeria imelitaja kundi la kigaidi la Boko Haram kuwa ndilo linalohusika.
Watafiti wa mambo wanayataja mashambulizi hayo kuwa ni juhudi za mwisho za Boko Haram katika kuonesha uwepo wake, baada ya kuzidiwa nguvu na jeshi la Nigeria hivyo kuyakimbia maeneo mengi liliyokuwa likiyadhibiti.

MUME WA MTU NI SUMU KAA MBALI!!!!!!! MREMBO ABABULIWA ‘RECEPTION’

INASIKITISHA sana! Muuza baa mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Halima, anajiuguza vidonda vikubwa mwilini vilivyotokana na kumwagiwa maji ya moto na mwanamke ambaye ni mtalaka wa bosi wake ambaye ndiye mmiliki wa baa anayofanyia kazi, Amani linakupa zaidi.

Halima anayedaiwa kumwagiwa maji ya moto.
Kwa mujibu wa chanzo ambacho ni ndugu wa majeruhi huyo, tukio hilo lilijiri mwezi uliopita ndani ya baa moja maarufu iliyopo maeneo ya Ubungo, Dar es Salaam ambapo majeruhi huyo anafanyia kazi baada ya mwanamke huyo kuamini Halima anatembea na mtalaka wake.
Inadaiwa kuwa, mwanamke huyo ambaye ni mtuhumiwa na mwanaume mmiliki wa baa aliyejulikana kwa jina moja la Mushi waliachana miaka mingi iliyopita.“Lakini mwanamke akawa anamfuatilia mumewe kila siku na kwa kila kitu. Ilifika mahali akaambiwa kuwa, mwanaume huyo aliyetengana naye ana uhusiano wa kamapenzi na baamedi wake mmoja.”
“Ndipo siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kwenye baa hiyo akitoka kusikojulikana. Wakati huo, Halima alikaa kwenye kiti akiangalia kaunta. Mwanamke huyo alipitiliza jikoni, akachukua sufuria yenye maji ya moto akammwagia Halima bila kujua kuwa, siye aliyemlenga mpaka Halima aliposema ‘siyo mimi’.”
“Kusema kweli baamedi aliungua sana hadi ngozi kuchunika na kuwa nyekundu kama mnyama aliyechunwa. Aliungua sehemu mbalimbali za mwili. Mfano, usoni ndiyo sana! Mgongoni pia, kifuani na mikononi,” kilisema chanzo hicho.
Ilidaiwa kuwa, maumivu ya maji yalimfanya baamedi huyo kulia kwa maumivu makali. Maana wakati anaungua, palepale ngozi ilianza kuchunika na kutoa majimaji ya malengelenge.”
Jeraha alilolipata sehemu ya bega.
“Ni ukatili mkubwa sana kutendeka maana hakuna ukweli wowote kwamba, yule baamedi alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi wake na hakulengwa yeye. Halafu hata kama ni kweli alikuwa na uhusiano naye, yeye walishaachana kwa miaka saba nyuma, sasa wivu wa nini?” kilisema na kuhoji chanzo hicho.
“Ishu ilikwenda kisheria kabisa, walikubaliana kuachana. Wakagawana mali na hata watoto waligawana. Wapo watoto wanne, mwanamke akachukua wawili, wengine wakabaki kwa baba yao.Kikaendelea: “Mbaya zaidi, baada ya ukatili huo, yule mtuhumiwa hakuchukuliwa hatua zozote zile! Hii inaonesha ni jinsi gani wanyonge wanaishi kwa hatari ndani ya nchi yao wenyewe. Pale hakuna cha bahati mbaya bwana.
“Halima hakuwa na pesa za kujitibu zaidi ya kutegemea misaada kutoka kwa wasamaria wema ambao walifahamu kisa kizima. Inauma sana kwa kweli.”Baadhi ya vyanzo vilidai kwamba, baada ya tukio hilo, mtuhu
miwa alitumia pesa kumlaghai majeruhi kwa lengo la kutochukua hatua yoyote na kwenda kumficha mahali akiuguza vidonda.
Baada ya madai hayo, Amani lilimsaka mwanamke anayedaiwa kutenda unyama huo ambapo ilidaiwa anaishi maeneo ya River Side, Ubungo jijini Dar.Hata hivyo, nyumbani kwa mwanamke huyo hakuwepo ambapo baadhi ya majirani walisema alitoka kwenda kwenye biashara zake na muda wake wa kurudi hauna ratiba inayosomeka sawasawa.
...Jeraha alilolipata mgongoni.
Walipoulizwa kama wanajua lolote kuhusu mwanamke huyo kumuunguza kwa maji ya moto Halima, walisema wanatambua lakini walishaombana radhi.“Tunajua, lakini si waliombana msamaha wenyewe kwa wenyewe? Nadhani walipatana,” alisema mmoja wa majirani.
Nacho chanzo hicho kilipoulizwa kuhusu madai ya wawili hao kupatana na kusameheana, kilisema:
“Hakuna kitu kama hicho. Kwanza unajua kwamba, Halima amelazwa Hospitali ya Mwananyamala? Amelazwa kule kwa sababu hali yake bado si nzuri.”
Jitihada zote za kumpata Halima hospitalini hapo hazikufua dafu baada ya mganga mkuu ambaye ndiye aliyetakiwa kutoa kibali cha Amani kuzungumza na majeruhi huyo kuwa bize kwa muda mrefu

DIAMOND, ZARI NDOA YAFUNGWA RASMI KIMYA KIMYA KAMA YA WEMA

Nyota  wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari.
Diamond aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipofanya mahojiano na waandishi wetu baada ya kumuuliza kama ana mpango wa kufunga ndoa na Zari.
SIKIA MAHOJIANO HAYO
Amani: “Zari ameshakubebea ujauzito, ameshaandaa shoo ya nguvu ile ya Zari All White Party hapa kwenu Tanzania na ameonekana kukubalika na baadhi ya mashabiki wako. Je, una mpango gani wa kufunga naye ndoa sasa?
Diamond: “Khaa! Mbona kama ni ndoa na Zari nimeshafunga kimyakimya!”
Amani: “Si kweli bwana! Lini na wapi?”
Diamond: “Hapahapa Dar. Lakini siwezi kusema ni wapi kwani tulishaamua iwe kimyakimya na imepita tayari, siku chahe kabla ya ile shoo ya Mlimani City.”Amani: “Kama ni kweli kwa nini haikuwa na mashamsham kama ndoa za mastaa wengine?”
KISA CHA KIMYAKIMYA
Diamond: “Unajua bi mkubwa (mama yake mzazi, Sanura Kasim) alikuwa anaumwa, kidogo ana nafuu kwa sasa. Ndiyo maana sikutaka mashamsham.”Amani: “Zari mwenyewe amekubaliana na uamuzi wa ndoa ya kimyakimya?”
Diamond: “Hakuwa na shida.”
KUHUSU DINI YA ZARI
Amani: “Amebadili dini? Maana ilisemekana alikuwa Muislam, akabadili kuwa Mkristo.”
Diamond: “Ilikuwa rahisi kurudi kwenye imani yake ya kwanza kwa hiyo ataendelea kuitwa Zarina.”
DIAMOND SASA
Rafiki wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini lakini wengi wanamjua, alipoulizwa kuhusu ndoa ya Diamond na Zari alisema:
“Jamani! Jamani! Jamani! Hivi kweli mnavyomjua Dangote (Diamond) nyie anaweza kufunga ndoa kwa siri au kimyakimya?”

...Wakipozi.
Amani: “Amesema kwa sababu mama yake bado hajakaa sawasawa kiafya?”
Rafiki: “Mbona kaenda kutumbuiza kwenye Zari All White Party, Mlimani City, si angekaa na mama yake nyumban? Hivi Dangote mnamjua, mnamsikia? Acheni kabisa.
“Dangote anapenda kiki! Kila siku anawaza kiki. Kwa hiyo kusema amefunga ndoa na Zari sidhani kama ni kweli inaweza kuwa ni kiki. Tena afadhali kama Zari asingekuwa na mimba, lakini ameshambebea ule mzigo ndiyo kabisa maana Dangote yeye hana cha kupoteza. Lakini anyway, labda kweli.”
NI SIKU CHACHE BAADA YA WEMA KUDAI AMEFUNGA NDOA
Hivi karibuni, mpenzi wa zamani wa Diamond aliye pia Miss Tanzania 2006 na staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu naye alitupia kwenye mtandao wa Instagram picha inayomwonesha amefunga ndoa kwa siri.
Baada ya picha hiyo kuwa gumzo, baadhi ya vyombo vya habari, hasa vya kielektroniki vilimpigia simu Wema ili kumuuliza kama kweli amefunga ndoa kwa siri kama inavyoenea kwenye mitandao, Wema alikiri.
Kwa ile sauti yake ndogo: “Yeah! Nimefunga kweli ndoa.”
Swali: “Sasa Wema wewe ni supastaa, kwa nini ufunge ndoa kwa siri mpaka wadau wako wasijue?”
Wema: “Mume wangu hapendi ijulikane. Hata mimi sipendi ijulikane.”
YALIYOMKUTA WEMA BAADA YA KUKIRI
Amani lilizungumza na mtu mwingine wa karibu na Wema ambapo alisema:
“Jamani Wema amejitakia matatizo, ndugu zake, dada yake na mama yake wamemjia juu. Kwanza walimuuliza kama ni kweli amefunga ndoa bila wao kujua, akasema hajafunga.
“Mama yake alimwambia alichokifanya cha kukiri kwenye redio ni nuksi kubwa kwake na Watanzania hawatamwamini tena hata akisema ukweli.“Unajua ndugu zake waliweka kikao. Walikubaliana kwamba, kama ndoa yake ilikuwa kwenye filamu si mbaya lakini walilaani kile kitendo cha kuulizwa na watangazaji wawili wa redio tena kwa muda tofauti akakiri. Pale ndipo penye tatizo. Leo hii Wema atazungumza ukweli gani kwa watu wakamuelewa?”
WEMA NA GAZETI LA AMANI
Wema alipotafutwa juzi na gazeti hili na kuulizwa kuhusu ndoa hiyo alikiri kuwa ilikuwa filamu ambayo itatoka hivi karibuni.

MVUA ZILIVYOATHIRI DARAJA LA KIVULE JIJINI DAR


Daraja la Kivule lilivyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar.Magari yakipita eneo hilo la daraja kwa tabu.Mkondo wa maji yanayopita darajani hapo.
(PICHA NA GLOBAL WHATSAPP 0753 715 779)

HALI NI TETE, DAR YAKUMBWA NA MAFURIKO!

Baadhi ya nyumba zilizo bondeni katika eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar.
Namna ambavyo soko la Sinza-Afrika Sana linavyoonekana kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar.
Mkazi wa Tandale kwa Tumbo akitoa maji yaliyojaa kwenye nyumba yake kufuatia mvua kali zinazoendelea kunyesha jijini Dar.
Wakazi wa Tandale kwa Tumbo na maeneo ya jirani wakipita kwa tabu katika njia hiyo kufuatia mvua ambazo zinaendelea kunyesha jijini Dar.
WAKATI mgomo wa mabasi ukimalizika juzi, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamekumbwa na adha nyingine, baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kuleta madhara mbalimbali kijamii na kiuchumi.
Katika maeneo mbalimbali ambayo waandishi wetu walitembelea leo, walikuta baadhi ya wakazi wakitoa maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao na sehemu za kufanyia bishara zao.
Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Mwanayamala Mkwajuni maarufu kama ‘Bondeni’ wameonekana kutupia lawama Kampuni ya ujenzi ya Strabag kuwa ujenzi wao wa barabara ndio umechangia nyumba zao kuingiliwa na maji kwani mifereji iliyotengenezwa haikidhi uwezo wa kusafirisha maji kwa kasi maana ni midogo, badala yake maji hujaa na kupitisha juu kuelekea katika makazi yao.
Wakati huo huo waandishi wetu walifika maeneo ya Jangwani na kukuta baadhi ya nyumba zilizoko bondeni zikiwa zimezama majini, huku wakilalamika kutaka serikali iwasaidie, licha ya ukweli kwamba walishaambiwa siku nyingi kuhama mabondeni.

Wakati huo huo, eneo la soko la Sinza-Afrika Sana, waandishi wetu waliwakuta wafanyabiashara ndogondogo wakilaumu mifereji inayopitisha maji barabarani kuziba kufuatia uchafu unaotupwa na kuziba maji kufika hadi sokoni hali inayopelekea biashara zao kudoda kutokana na wateja kukosa sehemu ya kupita.

THEA ASEMA HANA MPENZI NA WALA HAHITAJI MAANA NI SHIDAA

Msanii wa kitambo katika tasnia ya filamu Bongo, Ndumbangu Mesayo ‘Thea’ amefungua kinywa kwa mara ya kwanza kuwa, hivi sasa hana  wala hahitaji kabisa mpenzi na hapendi kukumbuka chochote kilichopita katika maisha yake ya kimapenzi.
Msanii wa kitambo katika tasnia ya filamu Bongo, Ndumbangu Mesayo ‘Thea’.
Akizu ngumza na gazeti hili juzi Thea alisema, hakuna kitu ambacho hakipendi kama kukumbuka mahusiano yake ya kimapenzi yaliyopita kiasi kwamba hata jina la aliyekuwa mumewe (Mike Sangu) eti kalisahau.
“Yaani sasa hivi sina mtu na wala sihitaji kabisa, mara nyingi sipendagi kukumbuka kabisa historia ya nyuma, ndiyo maana huwezi kuamini hata ukiniuliza jina la aliyekuwa mume wangu sikumbuki kabisa,” alisema Thea.

RAY AANIKA SABABU ZA YEYE KUTOOA, ASHANGAZA WATANZANIA!

Brighton Masalu

Msanii wa ‘long time’ kwenye anga la filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amefungukia sababu za kutooa licha ya kwamba umri umekwenda.
Msanii wa ‘long time’ kwenye anga la filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum, Ray alisema amekuwa akipangua mawazo ya kuoa kila wakati kutokana na ugumu wa kumpata mwanamke ambaye hatampa stress kama zinazowapata baadhi ya watu.Alisema, kwa kuwa suala la kuoa ni jambo nyeti, halihitaji kukurupuka na hicho ndicho kimemfanya mpaka leo asiingie kwenye maisha ya ndoa.
“Unajua hili suala la ndoa ni sensitive ‘nyeti’ sana, halihitaji kukurupuka, linakutaka ukiingia kwenye uhusiano umchunguze vizuri huyo uliyempata ili kujiaminisha kwamba, hatakusumbua.“Hilo ndilo linalonifanya niwe singo mpaka leo, najua wengi wananishangaa lakini kwa kifupi ugumu wa kumpata mweza sahihi ndiyo sababu ya kutooa mpaka leo,” alisema Ray.
Alipoulizwa kwamba, ina maana kwa wapenzi wake waliopita wakiwemo Ruth Suka ‘Mainda’, Blandina Chagula ‘Johari na Hans Chuchu hakuna aliyeona anafaa kuwa mke, msanii huyo alicheka sana kisha akasema: “Wewee, acha mambo yako.”

ZAMARADI ANOGEWA NA KUZAA MTOTO

Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, kinachorushwa kupitia Clouds TV, Zamaradi Mketema ‘Zama’ amefunguka kuwa, ataongeza tena watoto kwani tangu amejifungua mtoto wa pili ameona nyumba imekuwa na raha sana.
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, kinachorushwa kupitia Clouds TV, Zamaradi Mketema ‘Zama’.
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Zamaradi alisema, ameshangazwa na furaha iliyotawala kwake na mzazi mwenzake na kwamba siku si nyingi atabeba mimba nyingine mbili fasta.
“Yaani watoto ni furaha kubwa, mimi nitaongeza tena wawili wa haraharaka maana nimegundua kuna kitu kinaongezeka kila unapoongeza mtoto mwingine ndani ya nyumba ikiwa ni pamoja na baraka,” alisema Zamaradi.

JINSI YA KUISHI NA MWANAMKE MZURI BILA PRESHA

Kibinadamu tunasema hakuna mwanamke mzuri na mbaya. Wote ni sawa na yule ambaye unamuona kwako ni mzuri, huenda kwa mwenzako akawa mbaya.Hata hivyo, wapo wanawake ambao kiuhalisia ni wazuri na hata wenzao wanakiri kwamba Mungu kawapendelea.

Uzuri ninaouzungumzia hapa ni ule wa sura na umbo. Wapo ambao wamejaaliwa kuwa na figa bomba kiasi kwamba kila mwanaume anatamani ampate.
Linapozungumziwa suala la kuoa, wanaume wengi sasa hivi hawaangalii sura wala umbo, tabia imekuwa kigezo cha msingi. Ndiyo maana unaweza kushangaa wapo wanawake wazuri tu huko mtaani lakini hawapati wanaume wa kuwaoa, kwa nini? Kwa sababu hawana tabia nzuri.
Lakini pia sasa hivi wapo wanawake wengi wazuri na wenye tabia nzuri ila imekuwa ngumu kwao kupata wachumba. Ukifuatilia utagundua kuwa, kuna dhana kwamba kuoa mwanamke mzuri ni kujipa presha.Ukweli ni kwamba si kila mwanamke mzuri ukimuoa atakupa presha, bali yapo mambo ya kuzingatia ili uweze kuishi kwa amani na furaha.
YANAYOMHUSU MKEO
Awe amekupenda kwa dhati
Unapomuoa mwanamke ambaye wewe umempenda kwa dhati na unaamini ni mzuri kwako, chunguza kama na yeye uko moyoni mwake.
Hii ni kwa sababu unaweza kuingia naye kwenye ndoa lakini kama hana mapenzi na wewe ni rahisi kukufanyia vitimbwi pale atakapompata ambaye moyo wake umemridhia.
Ajiheshimu
Ukioa mwanamke mzuri ambaye hata yeye anajijua kuwa ni mzuri, zungumza naye kuhusu suala la kujiheshimu. Asiwe na utani na wanaume, ajue nguo za stara za kuvaa, ajue yeye ni mke wa mtu na kutowapa wanaume wakware nafasi ya kummendea.
Asiwe na tamaa za kijinga
Ni vyema ukazungumza naye mara kwa mara kuhusu maisha. Ujue kuna kupata na kukosa! Ajue kuwa pesa hazina thamani mbele ya utu. Atambue kwamba wapo watakaojifanya wanampenda, wakampa pesa lakini kumbe wana nia mbaya.
Ajue thamani ya ndoa
Ni vyema mwanamke utakayemuoa akajua thamani ya ndoa. Awe tayari kuitunza ndoa yake kwa gharama yoyote. Akumbuke pia kwamba, wapo wazuri zaidi yake ambao mpaka leo wanaililia ndoa lakini wasipate wanaume wa kuwaoa.
Uzuri wake si chochote
Huenda kweli ni mzuri na marafiki zake wanakubali hilo lakini yeye ajue kabisa kwamba uzuri wake siyo tiketi ya kumfanya adumu kwenye ndoa. Wapo wazuri ambao waliachika na leo hii wanatanga na njia wasipate hata wapenzi wa kuzugia.

Itaendelea wiki ijayo.

DIAMOND ASAKWA MAZISHI YA BABA WA BABU TALE BILA MAFANIKIOA

BABA mzazi wa Meneja wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amezikwa juzi Jumanne kijijini kwao Mkuyuni, mjini Morogoro lakini miongoni mwa mambo ya kushangaza ni kitendo cha baadhi ya waombolezaji kumsaka mwanamuziki Nasibu bila mafanikio.
Staa wa Bongo fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Hilo lilijitokeza baada ya msafara uliotokea Dar kufika eneo hilo ambapo vijana walilizingira gari lililokuwa na mastaa na kuanza kuuliza juu ya uwepo wa Diamond.Vijana hao waliotarajia kumuona msanii huyo msibani hapo, hata waliposikia tetesi kuwa hakuwepo, waliendelea kumsaka kila gari huku wakimuuliza kila waliyemuona lakini jibu lilikuwa lilelile, hakufika.
Majibu hayo yalionekana kuwanyong’onyesha vijana hao ambapo baadhi waliamua kuondoka kuonesha dhahiri kuwa kilichowapeleka pale ni kumuona Diamond na si kuzika.Hata hivyo, vijana wengine waliamua kujipoza kwa kupiga picha na Madee kisha kushiriki mazishi hayo mwanzo mwisho.

MADAI, DENTI MIAKA 12 AWEKWA KINYUMBA NA NA MWALIMU WAKE WA KIKE

MWANAFUNZI mmoja wa darasa la sita katika shule moja ya msingi iliyopo Ubungo jijini Dar, aliyefahamika kwa jina la Magida mwenye umri wa miaka 12, mkazi wa Kipawa jijini Dar, anadaiwa kuwekwa kinyumba na mwalimu wake aliyetajwa kwa jina moja la Kimweri katika tukio lililofanyika kwenye nyumba mbalimbali za kulala wageni na kumfanya kushindwa kuhudhuria masomo.
Magida anayedaiwa kuwekwa kinyumba na ticha.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Mary Joseph akizungumza na paparazi wetu alisema, akiamini mwanaye ana umri mdogo na anahudhuria masomo kama kawaida, alishangazwa Machi mwaka huu mtoto wake alipokwenda shule na kutorejea nyumbani hadi siku iliyofuata.
Aliporudi, alidai alisumbuliwa na tumbo na kwamba alipata hifadhi kwa mtu aliyekataa kumtaja.
“Siku iliyofuata usiku saa saba akaniomba funguo aende kujisaidia, alipotoka alikaa muda mrefu bila kurudi, nikamfuata na kumtafuta sikumuona.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Mary Joseph.
Kesho yake nikatoa taarifa polisi kwa kuwa moyo wangu ulijawa hofu nikihisi katekwa usiku ule, siku mbili baadaye limuona kituo cha mabasi Ubungo lakini alinikimbia,”alisema mama huyo na kuongeza:
“Siku iliyofuata nilienda na kuomba msaada wa watu wakamkamata, baada ya kumpeleka Polisi Mawasiliano, akiwa analia alidai kwa kipindi cha mwaka mmoja alikuwa kwenye uhusiano na mwalimu huyo ambaye alimwambia afanye siri na alimkataza kwenda shule, akawa anamsubiri chini ya mti mmoja ambapo alimpitia kila alipotoka kufundisha na kumpeleka gesti tofautitofauti na wakiwa huko, humpatia maswali kisha kumsahihishia, kitu kilichokuwa kigumu mimi kugundua kama alikuwa haendi shule,” alisema mama huyo.
Kamanda Camillius Wambura.
Kaongeza kuwa, cha ajabu siku hiyo waliporudi nyumba alitoroka tena na mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni hakuwa akijulikana aliko.Jitihada za kumpata mwalimu Kimweri ziligonga mwamba kwa kuwa aliacha kufundisha tokea mwaka jana na kuhamia shule nyingine iliyopo Kisarawe ambako pia hakupatikana kwa maelezo kuwa hajaonekana kwa muda mrefu. Jalada la kesi yake limeandikwa SGR/RB/1216/2015 KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.

ZARI, PEDESHEE KATUNZI LAIVU!HUKU DIAMOND AKITANGAZA NDOA NA KUSUBIRI KUPOKEA MTOTO

KABAAANG! Wakati supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitembea kifua mbele huku akijinasibu kuwa anasubiri kwa hamu kupata mtoto kutoka kwa mchumba wake, Zarinah Hassan ‘Zari’, imevuja picha inayomuonesha laivu mwandani wake huyo akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi ikidaiwa kuwa ni mtu wake wa nguvu, Ijumaa lina stori kamili.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Katunzi ni mtu wake Zari kitambo kabla hata Diamond hajaanzisha naye uhusiano wa kimapenzi mwishoni mwa mwaka jana na walikuwa wakikutana mara kwa mara.“Katunzi na Zari walijuana kitambo sana. Yaani suala la Zari kuibuka Bongo na kufanya mambo yao haikuwa ishu na hata Katunzi alikuwa akiibuka Sauz (Afrika Kusini anakoishi Zari) na kuwa pamoja,” kilisema chanzo hicho.
KATUNZI ALIWAKUTANISHA ZARI NA DIAMOND
Kuonesha kwamba kina ubuyu kamili, chanzo hicho kilizidi kufunguka kuwa, hata safari ambayo iliwakutanisha Zari na Diamond kwa mara ya kwanza, mrembo huyo alikuja Dar, kumfuata pedeshee Katunzi, ndipo ‘dodo lilipomdondokea’ Diamond kama kumsukuma mlevi vile.
“Kweli Diamond ana zari kama lilivyo jina la mrembo huyo mwenye asili ya Kiganda. Siku hiyo ya kwanza kabisa walipokutana, Zari alikuwa anaibuka Bongo kuitikia wito wa mtu’we Katunzi.
NDANI YA NDEGE SASA
”Diamond alichangamkia fursa, alipoona ‘dhahabu’ inaelea ndani ya ndege katika daraja la  juu (business class), akaomba namba, akakubaliwa na ndipo wakaanza kupiga mapichapicha ya selfie ambayo yalivuja na Wabongo wakaanza kujiongeza kwani wakati huo tayari Diamond alikuwa ameshaachana na Wema Sepetu ‘Madam,” kilitiririka chanzo hicho.
Supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
PICHA ZAMSHTUA KATUNZI
Kwenye mazungumzo yake, chanzo hicho hakikusita kufunguka kuwa baada ya picha za Diamond na Zari kuanza kuvuja kwa mara ya kwanza, ilidaiwa kuwa zilimshtua Katunzi kiasi cha kumtumia ujumbe mfupi wa simu Zari kumuuliza ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kati yake na mwanamuziki huyo.“Katunzi ilibidi amuulize Zari kuhusu picha hizo, Zari akamwambia hakuna kitu chochote ni urafiki wa kawaida, hata hivyo jamaa hakujali.
DIAMOND UPOOO!!
“Diamond kama aliingia katika himaya ya Zari pasipo kujua kuna watu wanamjua kitambo atakuwa amechelewa. Pedeshee Katunzi alimjua kitambo sana Zari,” kilimalizia chanzo hicho.
PICHA TOFAUTI ZANASWA
Mbali na kumwaga ubuyu huo, chanzo hicho kilivujisha picha tofauti katika dawati la Ijumaa zinazomuonesha Katunzi akiwa kwenye pozi la pamoja na Zari kuthibitisha kwamba wawili hao ni watu wanaofahamiana.
KWA NINI URAFIKI WA SIRI?
Ijumaa lilifanya uchunguzi wa kwa nini urafiki wa Zari na Katunzi ulikuwa wa siri na kubaini kuwa wawili hao hawakutaka watu wajue kwa sababu ambazo wenyewe wanazijua lakini kitu walichokuwa wanazingatia ni mpango wa ‘kula bata’.
Timu yetu ya uchunguzi imebaini pia kuwa, wawili hao wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara kupitia simu zao za mikononi, mawasiliano ambayo bado yanafanyiwa kazi ili baadaye yapakuliwe yakiwa yameiva.
KATUNZI ANASEMAJE?
Baada ya kumsaka Zari bila mafanikio, mwanahabari wetu alimvutia waya Katunzi ili kumsikia anazungumziaje ukaribu wake na Zari, alipopatikana alijibu kwa kifupi.“Zari namfahamu, kuna nini kwani?” Alihoji  Katunzi. Alipoambiwa kuwa kuna picha na habari zake kuhusu Zari alikata simu na hata alipopigiwa tena hakupokea.
KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Kufuatia kuwepo kwa minong’ono mingi kuhusiana na ukaribu wa Zari na Katunzi, dawati la Ijumaa linaendelea kuchimba undani wa habari hii kwa kumtafuta Katunzi, Zari na Diamond ili wote wafunguke kwa kirefu.

MSHINDI WA NDINGA YA EFM AKABIDHIWA

Mshindi wa shindano la shika ndinga akiondoka na gari yake pembeni ni mke wake na mtoto wake. Mshindi wa shika ndinga Gabriel akiwa na mtoto wake wakifurahia kushinda ndinga, pembeni ni afisa uhusiano wa EFM Lydia moyo

MAFURIKO 'YALIVYOLIZAMISHA' ENEO LA KONA YA SHEKILANGO/BAMAGA

Maji yakiwa yamejaa katika barabara ya Shekilango eneo la Bamaga leo.
Vyombo vya moto vikiendelea kupita taratibu katika eneo hilo.
Maji yakiwa yamejaa kituo cha mabasi Chuo cha Ustawi wa Jamii.