Gumzo la mjini wiki hii ilikuwa ni shoo ya mchumba wa Nasibu
Abdul ‘Diamond’ Zarinah Hassan ‘Zari’ iitwayo Zari All White Party
iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar na ile ya Instagram Party ambayo ilimhusu mrembo Wema Sepetu
iliyofanyika jijini Mwanza ambapo nyuma ya pazia, warembo hao walitoana
jasho kuhakikisha wanafunikana, Risasi Jumamosi lina stori kamili.
Staa wa Bongo movie,Wema Sepetu.
MVUTANO WAANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mvutano wa Wema aliyewahi
kuwa mchumba wa Diamond na Zari ambaye anammiliki Diamond kwa sasa,
uliibuka Alhamisi iliyopita wakati kila mmoja akijiandaa kwenda kwenye
shoo inayomhusu.
“Wema na Zari leo ni full kutoana jasho, kila mmoja anataka kuwavuta mashabiki wengi upande wake.
ZARI APEWA SAPOTI
“Zari amepata sapoti kubwa kutoka kwa mpenzi
wake wa sasa Diamond kwani walikuwa wanafanya shoo pamoja hivyo alikuwa
na kibarua cha kuwakusanya mashabiki wote wa Diamond waende kwenye shoo
yake ili Wema asipate watu,” kilisema chanzo hicho.
UPANDE WA WEMA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kwa
upande wa Wema, yeye alikuwa na kibarua kizito cha kuwakusanya marafiki
zake hususan mastaa wa Bongo Movies wasiende kwa Zari na badala yake
waende Mwanza kwenye Instagram Party.
Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Ni mnyukano wa aina yake, Wema alikuwa na kibarua kizito
kuwashawishi Bongo Movies waikache shoo ya Zari waende Mwanza kwenye
Instagram, bahati nzuri alifanikiwa kwani wasanii wengi walimuunga
mkono,” kilisema chanzo hicho.
MATUSI
Hadi jana jioni, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii,
Timu ya Zari (Team Zari) na ile ya Wema (Team Wema) zilikuwa
zikirushiana matusi huku kila mmoja akionesha hisia zake.“Hakuna kwenda
kwa Zari, twendeni kwa Wema Mwanza, watakaokwenda kwa Zari ni wapuuzi
kabisa,” ilisomeka moja ya komenti ya mdau wa timu Wema huku timu Zari
ikijibu:“Wajinga wakubwa watakaokwenda kwa Wema, mpango mzima ni kwa
Zari na Diamond pale Mlimani City.”
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
STEVE AFUNGUKA
Ili kuzidi kupata data zaidi, wanahabari wetu
walimtafuta mdau mkubwa wa kuwashawishi watu, mwigizaji Steven Mengere
‘Steve Nyerere’ ambaye aliweka bayana kuwa wao kama Bongo Movies,
wanamuunga mkono Wema.
“Niweke wazi tu kwamba sisi tutakwenda kwa Wema, hii shoo ya Zari na Diamond itatupitia kushoto kwa kweli,” alisema Steve.
KAJALA KWA ZARI
Kwa upande wake Kajala Masanja alikuwa tofauti na
waigizaji wenzake ambapo alipokea kwa mikono miwili mwaliko wa Zari na
kuanza kuihamasisha Team Kajala kwenda kwenye shoo hiyo.
WEMA AFUNGUKA
Jitihada za kumpata Zari aweze kufungukia mvutano
huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita bila majibu lakini bahati
nzuri Wema alipatikana na kufunguka:“Mimi kama mimi nakwenda katika
shoo inayonihusu ya Instagram, hiyo ya Zari siijui. Sijashawishi mtu ila
watu wameamua kuniunga mkono, siwezi kuwazuia na hao wanaofikia hatua
ya kutukana pia siwezi kuwazuia,” alisema Wema.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu.
MWISHO UKOJE?
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, shoo ya Zari
ilitarajiwa kurindima na mashabiki wake huku Wema akiwa na mashabiki
wake waliomuunga mkono hivyo kusababisha mtikisiko wa aina yake mjini.