PENZI LA NEY WA MITEGO LASABABISHA WASANII KUCHAPANA HADHARANI MCHANA KWEUPE TENA BAA

HII sasa kali! Wasanii wa sinema ndani ya Bongo Movies, Fatuma Ayubu `Bozi’ na Brenda Marembeka `Kunguru’ wametoa aibu ya mwaka baada ya kupigana kwenye baa tena mchana kweupe kwa kile kilichodaiwa walikuwa wakigombea mabwana ambao ni mastaa  wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ huku Kasim Yusuf `Young D’ naye akitajwa.
Wasanii wa sinema ndani ya Bongo Movies, Fatuma Ayubu `Bozi’ na Brenda Marembeka `Kunguru’ wakiamuliziwa baada ya kuzichapa.
Sekeseke hilo la aina yake lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye Baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar ambapo kwa mujibu wa shuhuda mmoja wa tukio hilo, Bozi alitangulia kufika mahali hapo na kuagiza kinywaji.
WALIFIKA TOFAUTI
“Baada ya muda yule mwenzake (Kunguru) akafika na kuanza kumrushia vijembe mwenzake kisha kummwagia kinywaji chake na kumvua wigi alilokuwa amevaa.“Yaani hawa wasanii siyo siri wanaidhalilisha tasnia. Yule mwenzake alipofika tu, bila hata salamu akaanza kumtupia maneno makali mwenzake huku akimtuhumu kwa nini alitembea na bwana wa rafiki yake ambaye ni Nay wa Mitego kisha akaanza  kumkunja.
WAUMBUANA
“Yule mwingine (Bozi) akapamba moto na yeye, akasimama na kumuwakia mwenzake akimwambia  alitembea na bwana wake ambaye ni Yuong D. Yaani wamesababisha watu kujazana na kusitisha shughuli zao,” alisema shuhuda huyo.

MENEJA APATA WAKATI MGUMU
Wakati maparazi wanafika eneo la tukio walimkuta mtu mmoja aliyetambulishwa kuwa ni meneja wa baa hiyo akiwa katikati kuwaamua wasanii hao na kuambiwa waondoke.

Wakitupiana maneno baada ya kuamuliziwa.
WAHUDUMU PIA WANENA
Mbali na meneja kuwataka waondoke, wahudumu wa baa hiyo maarufu nao walionekana kutofurahishwa na kitendo cha wasanii hao kuzichapa kwenye baa hiyo kiasi cha kuwabughudhi wateja. Waliwatolea matusi mazito ambayo hayaandikiki gazetini huku wakiwaambia siku wakiziona sura zao kwenye baa hiyo wataishia polisi.

WENYEWE SASA
Baadaye kwa njia ya simu, mapaparazi wetu waliwatafuta wasanii hao, kila mmoja kwa wakati wake na kuwahoji juu ya ugomvi wao uliosababisha kujaza watu baa ambapo kila mmoja alimtupia lawama mwenzake kwa usaliti.

BOZI
“Yule Kunguru kwa kipindi kirefu hatujaonana na wala hatuongei. Cha ajabu leo nimekaa zangu pale baa nastarehe, hata sijui alipotokea, kaja na kuanza kunichokonoa. Ukweli mimi niliwahi kuwa na uhusiano na Young D kabla yake, yeye akaiba namba kwenye simu yangu wakatongozana mpaka kuwa wapenzi na huenda wameshaachana, sasa sijui kimemuuma nini? Labda alijua angeolewa.”


Staa  wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
KUNGURU
 “Sitaki kumuongelea huyo mtu, hana maana yoyote nitampa ujiko tu. Yeye alijua rafiki yangu (hakumtaja jina) anatoka na Nay na yeye akajipeleka. Kiko wapi sasa? Mbona kaachwa! Tena ndiyo kwanza kaambulia kusambaziwa picha zake za utupu mitandaoni.

NAY, YOUNG D
Kwa upande wake, Young D alipotafutwa kwa simu na kuambiwa kuhusu wasanii hao aligoma kuwazungumzia. Nay yeye alipoulizwa alianza kwa kucheka, akasema: “Ha! Ha! Mimi sijawahi kuwasikia hao watu na siwajui kabisa labda kuna kitu wanakitafuta kutoka kwangu.”
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS

HII NAYO KALI ETI TUMBO LA LULU LAYEYUKA GHAFLA


Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka na yupo ‘flati skriini’.
Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano wa Umma, akiwa hana lile tumbo la Aprili.Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walidai msanii huyo alikuwa hafiki chuoni hapo kwa muda mrefu lakini sasa amejaa tele ‘mwepesii’.
“Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’ kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,” alisema mmoja wa wanachuo hao.Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila majibu.
Baadaye alitumiwa ujumbe wa kwanza uliosomeka: “Tafadhali naomba upokee simu, nahitaji kuzungumza na wewe jambo muhimu.” Hata hivyo, hakujibu.Baada ya kuona kimya, mwandishi wetu alimtumia ujumbe ulioonesha madai hayo: “Kuna tetesi kuwa ulinasa mimba na kuficha na sasa inadaiwa kutoka na kwamba hata chuoni haukuwa ukihudhuria, hili likoje?”
Baada ya kimya cha saa kadhaa, Lulu alijibu:
“Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.”
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.

MWANAMKE AMTUPA MWANAWE BARABARANI KUMKOMOA ALIYEZAA NAYE

UKATILI WA MAMA

UCHUNGU wa mwana si aujuae mzazi? Sasa mama mzazi huyu vipi?! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke Pendo Mabuko amejikuta akipokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira waliokerwa na kitendo chake cha kumtupa barabarani mwanaye wa kumzaa baada ya kunyimwa matumizi ya mtoto huyo na mwanaume aliyezaa naye, Daniel ambaye ni mume wa mtu.
Mtoto anayedaiwa kutupwa na mama yake, Pendo Mabuko.
Tukio hilo lililojaza umati lilitokea Ijumaa iliyopita, saa 10 jioni katika Mtaa wa Simu ‘A’ Kata ya Mji Mpya mkoani hapa.
Wakihojiwa na gazeti hili,  mashuhuda wa tukio hilo, Asha Hussein, Mussa Juma na Paskal Msimbe kwa nyakati tofauti, walisema:
”Tukiwa hapa barabarani tulimshuhudia huyu mwanamke na mwanaume mmoja wakizozana kwa muda mrefu, tulipowasogelea ili kuwasuluhisha, mwanaume alipanda bodaboda na kutimka.
“Ndipo huyu mwanamke akamtupa mtoto kisha naye akaanza kuondoka huku akisema amechoka kumlea mtoto wa mtu, sisi tukamzuia.
Mwanamke huyo akilia baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi waliokelwa ha kitendo hicho.
“Tulimlazimisha kumchukua mwanaye lakini aligoma, tukaamua tukuite wewe mwandishi kwa msaada zaidi.”
Wakati mwandishi wetu anawasili eneo la tukio, aliwashuhudia baadhi ya wananchi wenye hasira wakimshushia kichapo mwanamke huyo kwa kitendo cha kumtupa mwanaye.
Mwandishi aliita polisi wa pikipiki ambapo Afande Mwajabu alifika fasta na kumchukua mwanamke huyo na mwanaye na kuwapeleka  kituoni kwa mahojiano zaidi.  
Awali, akihojiwa na mwandishi wetu kuhusu uamuzi wa kumtupa mtoto wake barabarani, mwanamke huyo alisema:
”Muda huu tunatoka Ustawi wa Jamii kusuluhishwa. Mimi nilipeleka malalamiko, mzazi mwenzangu kagoma kumtunza mwanaye na kuniachia mzigo peke yangu.

Mama huyo akiwa mikononi mwa polisi.
“Nikimuuliza anasema mkewe kamzuia kumtunza mwanangu ndiyo maana na mimi kwa hasira nikaamua kumtupia mwanaye akamlee na mkewe.”

RAY ATESWA NA PICHA ZAKE ZA UTUPU MTANDAONI

Supastaa kunako Bongo Muvi, Vincent Kigosi, ‘Ray’ anateswa na tuhuma anazopata kutokana na mtu asiyejulikana kufungua akaunti feki ya Facebook yenye jina la Ray kisha kuposti picha za utupu.
Supastaa kunako Bongo Muvi, Vincent Kigosi, ‘Ray’.
Akizungumza na paparazi wetu, Ray alisema kuwa japokuwa ametoa ufafanuzi kupitia mtandao wake wa Instagram kuhusu picha hizo na akaunti hiyo feki, anashangaa kuona watu wanamuandama na kukomalia kwamba yeye anahusika.
“Yaani hii ishu inaniumiza na nimetoa ufafanuzi lakini sieleweki, naomba niseme kwamba mimi ni mtu ambaye najiheshimu sana, siwezi kufanya kitu kama kile mashabiki zangu waelewe hivyo tu,” alisema Ray.