KIMENUKA TENA KWA DAVINA:MUME AMCHANA LIVE DAVINA

KIMENUKA! Mume wa muigizaji nyota wa filamu nchini, Halima Yahaya ‘Davina’, Abdallah Shakoor ambaye amekuwa kimya tangu kuenea kwa madai ya mkewe kutoka na staa mwenzake, Mike Sangu, hatimaye amefunguka kuhusu skendo hiyo na kudai anafuatilia kila hatua ya wawili hao na hivi karibuni atatoa msimamo wake.
Muigizaji nyota wa filamu nchini, Halima Yahaya ‘Davina’.
Chanzo chetu makini kimeripoti kuwa wasiwasi wa mume huyo kwa mkewe ulianza muda mrefu uliopita, hasa baada ya staa huyo kusafiri kuelekea Iringa kwenye mazishi ya shangazi yake akiwa ameongozana na Mike, kitendo kilichomkera sana.
Inadaiwa kuwa kutokana na madai hayo kuandikwa magazetini mara kwa mara, yamesababisha familia ya mume kutaka kujua kinachoendelea baina ya wawili hao waliofunga ndoa yao Kiislamu.Gazeti hili lilipomtafuta mume wa staa huyo alisema anasikitishwa na kinachoendelea kwa kuwa alimpenda sana mkewe, lakini uvumilivu wake umefikia mwisho, hasa kufuatia kashfa zinazotajwa dhidi yake.
“Jamani hakuna mwanaume anayefurahia kashfa za mkewe gazetini, hainiletei picha nzuri kwenye familia, tena yenye maadili ya kidini kama yangu. Siwezi kushindana na Mike kama mke wangu haoni tatizo.“Mimi mwenyewe ni mtoto wa mjini sana, lakini sioni sababu ya kulumbana au kumfanyia kitu Mike, kwa nini nifanye hivyo kama Davina haoni tatizo?” alihoji.
Kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mume huyo alisema endapo Davina ataendelea na maisha aliyojichagulia, atalazimika kuoa mwanamke mwingine.Davina alipotafutwa alisema: “Kiukweli mimi bado nampenda mume wangu ila kama anaamua hivyo, sawa.”

No comments:

Post a Comment