KUMBE MTOTO WA JOHARI AMEZAA NA YAY AFUNGUKA!

Staa wa filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
Hivi karibuni gazeti hili lilimbana staa huyo anayetamba sokoni kwa sasa na Filamu ya Chicken Head baada ya kubambwa nje ya Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za Tuzo za TAFA ambapo aliweka wazi.
Awali, Ray alisema si busara wala hataki...
kuzungumza mengi juu ya madai hayo kwani hahusiki kwa lolote na kwamba watu wasimtafsiri kutokana na maneno yasiyokuwa na ukweli huku akimtaja mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans kuwa ndiye mwanamke wake wa maisha.
Ray alifunguka kuwa, kati ya mambo yanayomchukiza ni ama kuzushiwa au kuhusishwa na mambo ambayo yanamfanya aonekane wa hovyo katika jamii na kusisitiza kusiwepo na mjadala unaopingana na kauli zake.
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa na mwanaye.
Huku akiwa amemganda Chuchu kimahaba mbele ya kadamnasi, Ray alikwenda mbele zaidi na kusema ni jambo la heri kujiweka mbali na watu wanaotafuta umaarufu kupitia migongo ya watu, kauli iliyozua viulizo kwa waandishi wetu na yeye kushindwa kuifafanua kwa kile alichokiita ‘hakuwa na mudi ya mazungumzo zaidi’.
“Achaneni na hayo mambo, sihusiki kwa lolote na jambo hilo (mtoto) na sipendi kabisa kuzushiwa mambo kama hayo, watu wasinitafsiri kwa minong’ono na badala yake wafuate ninachokisema.
“Kwa sasa mwanamke wa maisha yangu ni huyu (Chuchu) na nitakuwa natembea naye kila mahali ili kuwafunga midomo wanaojinadi kuwa ni wapenzi wangu,” alisema Ray huku akiwatazama waandishi wetu kwa macho ya ‘nadhani mmenielewa sasa’ na kuondoka eneo hilo sanjari na mahabuba wake.
Hivi karibuni Johari alithibitisha kuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miezi saba ambaye alimpa jina la Maria linalofanana na la mama wa Ray hivyo kuibua minong’ono kuwa huenda jamaa huyo anahusika.

MKE AKODISHA KIBAO KATA KUMKOMESHA MCHEPUKO WA MUME WAKE!

Wakimsimanga kwa staili ya kusasambua.
Tukio hilo lilitokea Mei 23 mwaka huu maeneo ya Kimara Mwisho, ambapo awali mke wa mume aliyechepuka, aliyejitambulisha kwa jina moja la Upendo, alidai mara kwa mara amekuwa akipokea taarifa kuwa mwanamke huyo anatembea na mumewe jambo lililomfanya amtafute, lakini alikataa katakata, akidai wao ni marafiki wa kawaida.
Akizungumza na waandishi wetu, mke huyo wa mtu alisema baada ya kuzungumza na mumewe mambo hayo yaliisha, lakini siku chache zilizopita aliiona simu ngeni ndani ya gari la mumewe, alipoipiga akagundua kuwa ni ya mwanamke huyo, jambo lililoibua upya mgogoro baina yao.
Ngoma ya kibao kata ikilindima wakati wa zoezi hilo.
“Nilimalizana na mume wangu lakini safari hii nikampigia simu yule mwanamke na kumpa tahadhari, lakini majibu aliyonipa nilipata hasira sana, eti alisema kama namchunga sana mume wangu basi nimjengee zizi nimfungie. Nikaona hizo ni dharau, nikaamua lazima nimsute,” alisema Upendo.
Kama  hiyo haitoshi mke huyo wa mtu alisema kuwa siku moja alipata taarifa kuwa mumewe amepigwa chupa na mchepuko huo, kisa kikiwa ni wivu wa kimapenzi ambapo katika sekeseke hilo gari yake ilivunjwa kioo jambo lililomzidisha hasira kiasi cha kumtafutia kibao kata.
Waandishi wetu waliokuwa katika kusaka matukio walilinasa tukio hilo ambapo walishuhudia umati wa kina mama wa mjini walioshushwa eneo hilo kutoka kwenye gari aina ya kirikuu, wakimvaa mwanamke huyo aliyekuwa saluni kwake bila habari kama ngoma hiyo imemfuata ili asutwe na mwenye mali.
Mke anayedai kuibiwa mumewe.
Katika hali ya kushangaza, ghafla aliwachoropoka na kutoka mbio kukimbilia chooni katika nyumba ya jirani na kujifungia ndani  huku juhudi za kumtoa zikishindikana.
Kama hiyo haitoshi ngoma ya kibao kata iliendelea kupigwa huku wakina mama wakimwaga radhi waziwazi, wakimchamba vilivyo huku mtaa ukiwa umefungwa kwa muda, kuhakikisha tabia ya mwanamke huyo inajulikana mtaa mzima hali iliyofanya umati wa watu kujaa wakitaka kushuhudia nini kinachotokea eneo hilo.

DIAMOND ATELEKEZA WATOTO ALIJITOLEA KUWASOMESHA SHULE!

KABANG! Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewatelekeza watoto katika Shule ya East Africa International jijini Dar ambao aliahidi kuwalipia ada, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.

Wanafunzi wanaodaiwa kutelekezwa na Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili juzi kwamba, baada ya Diamond kuwashindanisha watoto hao, Hillary na Hamis (katika picha no. 1 na 2 zilizoko ukurasa wa mbele walipelekwa shule na Diamond) katika shindano la Ngololo lililonyika Januari, mwaka jana katika Viwanja vya Leaders Club, Dar na kushinda aliamua kuwapeleka katika shule hiyo na kuahidi kuwalipia ada kila mwaka lakini kuanzia hapo aliwatelekeza.
“Jamani Diamond kila kukicha anafanya shoo za mamilioni lakini ameshindwa kuwalipia ada wale watoto ambao aliahidi kuwasomesha. Wamesoma mwaka mmoja tu,  mwezi uliopita walitimuliwa na sasa wako nyumbani. Inauma sana kwani hawa watoto walitolewa kwenye shule za kawaida na yeye ndiyo akawapeleka kule,” kilisema chanzo hicho.
WAZAZI WANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Fadhili alisema watoto wao walitimuliwa shuleni tangu April mwaka huu kwa kuwa, Diamond hakuwahi kuwalipia ada tangu alipowaingiza pale.“Inauma sana, kwani tangu watoto wetu watimuliwe tumekuwa tukifuatilia kwa mtu tuliyeambiwa ni msimamizi wa Diamond (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) lakini hatupi jibu la kueleweka.
Nasibu Abdul ‘Diamond akiwa na wanafunzi hao pamoja na mwalimu wao.
“Tulipewa namba za simu za mameneja wa Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Said Fella lakini kila tukiwapigia simu tunaambiwa msanii huyo hayupo Dar, mara amesafiri, mara yuko kwenye shoo, yaani kila siku tunazunguka tu hatujui tufanye nini.
“Tunaomba sana jamani, mtusaidie na nyie waandishi maana watoto wanapitwa na masomo na isitoshe kabla ya hapo walikuwa wakisoma kwenye shule za kawaida,” alisema mzazi huyo.
MSIKIE MWALIMU MKUU
Paparazi wetu alifunga safari mpaka shuleni hapo maeneo ya Mikocheni, Dar na kufanikiwa kuzungumza na Mwalimu Mkuu, Mercy Githirua ambapo alithibitisha watoto hao kusimamishwa masomo kutokana na kukosa ada.“Tulivumilia kwa muda mrefu sana kwani tulimwamini Diamond tukawapokea watoto hao na kuanza masomo. Siku aliyokuja kuwakabidhi hapa shuleni aliomba ‘invoice’ kwa ajili ya kututumia  ada lakini yuko kimya mpaka leo.
...Akisalimiana na mwalimu.
“Hata fedha ya kuwashonea sare za shule ilibidi niwasiliane na (linatajwa jina, linasitiriwa) maana tunafanya naye kazi nyingi, akatoa hizo fedha lakini ada ndiyo ikawa tatizo. Hivyo ilipofika Aprili 14, mwaka huu ilibidi niwarudishe nyumbani mpaka kieleweke kwa kweli.
“Sijapenda tabia ya Diamond, hivi anajua watoto wakimchukia itakuwa ni hatari sana kwake? Watoto wa watu walikuwa wanasoma huko akaenda kuwatoa na kuwaleta hapa lakini amewatelekeza, siyo vizuri kabisa,” alisema mwalimu mkuu huyo.
WANADAIWA SHILINGI NGAPI?
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo, watoto hao tangu walivyoingia Januari 21, 2014 hawakuwahi kulipiwa ada yoyote hivyo kila mmoja anadaiwa shilingi milioni moja na laki sita (1,600,000).

DIAMOND, MAMENEJA WAKE!
Juzi, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kwa njia ya simu lakini ilikuwa imesetiwa kwamba inafanya kazi muda wote ‘bize’ hata alipotumiwa meseji hakujibu. Vivyo hivyo kwa mameneja wake, Fella na Bab Tale simu zao ziliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka jana, Diamond aliandaa shindano la Nani Anaweza Kucheza Staili ya Wimbo wa Ngololo ambapo watoto kibao walijitokeza Leaders Club. Watoto hao wawili waliibuka kidedea kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kucheza na ndipo zawadi yao aliamua kuwapeleka kwenye shule hiyo na kukutwa na yaliyowakuta!

JE WAIFAHAMU HII!!!!‘NIMEKUMISS’ YA MWANAMKE, ‘NIMEKUMISS’ YA MWANAUME, TOFAUTI

Leo katika makala haya nazungumzia neno maalum kabisa katika uhusiano linaloitwa miss! Miss yaani kosa, pia ‘kosana’ hutumiwa zaidi na watu wenye uhusiano wowote ule, iwe ndugu, wapenzi na hata marafiki walioshibana.
MATUMIZI YAKE
Ni neno la Kiingereza ambapo watumiaji wanapaswa kuwa Waingereza wenyewe lakini pia wasio Waingereza ambao wanajua maana yake.
Hutumika kwa watu waliopotezana kwa muda ambao mhusika amehisi kumkumbuka mwenzake kwa maana ya kuonana naye laivu.
“Shoga, upo?”
“Nipo shoga yangu, niambie, mzima?”
“Mi mzima tu, nimekumisi ‘miss’ ile mbaya.”
“Nimekumisi pia shoga yangu.”
Maneno hayo ni watu wawili walioshibana ambapo wamepotezana au hawajaonana kwa siku kadhaa. Idadi ya siku za ‘kumisiana’ hutegemea mtu na mtu na si kwamba ni kiwango cha kimataifa kuwa lazima ziwe siku mia moja!
MATUMIZI MENGINE
Matumizi mengine ya neno hili limekuja kujikita kwa watu walio kwenye uhusiano wa kimapenzi. Walio wengi wanapokuwa kwenye mapenzi, hufika wakati kila mmoja akatamani kuwa na mwenzake ‘laivu’ kwa maana ya kukaa pamoja na kuzungumza au kuonana tu pia kunashibisha hamu ya upendo.
Wapenzi walio wengi, iwe mke na mume au wachumba na hata wasiokuwa na vyeo vyote viwili hulitumia neno kumisi kama ishara ya kukumbukana kwa maana kuonana laivu.
MFANO MZURI NI HUU
Mfano mzuri, wapenzi wawili, mmoja amesafiri hivyo kuwa mbali na mwenzake, sasa yeyote yule anaweza kumkosa mwenzake kama ilivyo mazoea yao. Hivyo ni rahisi kumsikia mmoja akianza:
“Baby nimekumisi sana.”
“Hata mimi nimekumisi pia mpenzi wangu.”
“Unarudi lini baby?”
“Wiki ijayo baada ya kumaliza hii kazi.”
“Poa baby, nakutakia kila la kheri.”
“Asante baby.”
Hawa wawili wamemisiana kwa kutoonana laivu kutokana na mmoja kuwa mbali na mwenzake tofauti na mazoea yao.

LAKINI SASA
Pamoja na yote hayo, uchunguzi wa kawaida nilioufanya nimebaini kuwa, neno nimekumisi limekwenda mbele zaidi na kutumika katika uhitaji wa tendo la ndoa, hasa kwa wanawake!
Kivipi? Wapenzi, baadhi yao tena kwa sehemu kubwa wamekuwa wakilitumia neno hili kwa maana ya kutaka kukutana kwa tendo la ndoa.
Unaweza ukakuta wapenzi wanaishi mbalimbali, wamekutana asubuhi lakini jioni, mmoja anamtumia meseji mwenzake ya kumwambia amemmisi sana.
Nilijaribu kutafuta maana yake nini, je ni kumisi kwa maana ya kumuona laivu nikajua si hivyo, nimekumisi hii ni ya kutaka kukutana kwa tendo la ndoa.
TOFAUTI YA MWANAMKE NA MWANAUME!
Ila sasa, kuna tofauti kubwa ya misi ya mwanamke na misi ya mwanaume! Katika wanawake kumi, nane hulitumia neno hili kwa maana ya kutaka kukutana kwa tendo la ndoa tofauti na misi ya mwanaume ambao karibu wote hulitumia kwa kutaka kuonana laivu.
Kama wewe ni mwanaume, una mpenzi wako, tena mkeo kabisa, mko nyumba moja, kitanda kimoja, unaweza kuwa kazini akakutumia meseji kukwambia amekumisi lakini yenye maana ya tendo la ndoa.
Kama wewe ni mwanamke, una mpenzi wako, ni mumeo, ukiwa mbali naye kwa siku nzima, anaweza kukutumia meseji ya hivyo akimaanisha kutokukuona laivu.
WAPENZI, WACHUMBA
Kundi hili ndilo linathibitisha matumizi hayo. Kwamba, wapenzi, wachumba wanaweza kukutana saa kumi jioni, wakiachana usiku, msichana akatuma meseji ya misi akimaanisha kukutana kimwili.
Mara nyingi sana, wanawake hulitumia neno hilo kwa maana hiyo. Nimefanya utafiti na kubaini hilo. Hata wapenzi wanapokuwa hawajakutana kimwili kwa siku kibao, mwanamke akijisikia anakuwa mgumu sana kusema wazi kwamba anahitaji tendo hilo, njia yake kubwa ni kusema ‘baby nimekumisi’ wakati mwanaume huenda moja kwa moja.
Kwa hiyo nathibitisha kwamba, nimekumisi ya mwanamke na nimekumisi ya mwanaume tofauti! Hivyo wanaume mnapaswa kulijua hilo badala ya kudhani ni ile ya kutokuonana na wewe ukajibu ‘na mimi pia’.
Tukutane wiki ijayo katika mada nyingine.

UKWELI KUHUSU KIFO CHA MTOTO ALIVYONYONGWA MOROGORO

SIKU tatu baada ya mazishi ya mtoto Edyline Barnabas Mafwere (9), aliyedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na mtoto wa baba yake mkubwa, simulizi kamili imepatikana baada ya ndugu jamaa na majirani wa marehemu kuzungumza na gazeti hili.
Marehemu Edyline Barnabas Mafwere enzi za uhai wake.
Judith, msichana anayedaiwa kufanya mauaji hayo ambayo yamegeuka kuwa gumzo mjini hapa, anadaiwa alijaribu kumuua msichana huyo mara ya kwanza Mei 10, mwaka huu, lakini akashindwa baada ya jirani mmoja kumuwahi na kumkuta akiwa amemkaba shingo.
Mwenyekiti mstaafu wa serikali ya mtaa huo, Hasda Msuya alisema akiwa nyumbani kwake, siku hiyo alisikia sauti ya mtoto akilia kwa muda mrefu, alipokwenda katika nyumba hiyo alimkuta Judith akimpiga marehemu huku akiwa amemkaba shingo, lakini akamkemea na kuondoka zake.
Mama mzazi wa Edyline Barnabas Mafwere akilia kwa uchungu.
“Jana (Mei 20, 2015) majira ya saa 12 jioni nilisikia kilio kwa mbali, wakati najiandaa kwenda, Judith akaja kwangu na kunieleza Edyline ameanguka na kutoka damu mdomoni, nilipokwenda nilikuta kweli hali hiyo nikampigia simu mama yake, alipofika tumekuta tayari mtoto amekufa, lakini tukaamua kumpeleka hospitali na madaktari wakathibitisha alishafariki muda mrefu,” alisema mama Msuya.
Mmoja wa wanafamilia hiyo aliyesafiri na wazazi wa mtuhumiwa wa mauaji hayo, alisema haelewi kwa nini baba na mama walishindwa kuhudhuria mazishini licha ya kuwa walishafika Morogoro.
Jeneza lililobeba mwili wa Edyline Barnabas Mafwere likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
“Sisi ni wakazi wa Ukerewe, wazazi wa Judith wamefika jana, wamefikia gesti moja ipo Kichangani wakiwa miongoni mwa watu tisa, lakini sijui sababu ya wao kushindwa kufika mazishini,” alisema mwanafamilia huyo huku akiomba hifadhi ya jina lake.
Baba mzazi wa marehemu, Barnabas Mafwere alisema siku ya tukio alikuwa kazini hivyo hana maelezo marefu, lakini akasema alimchukua mtoto huyo wa kaka yake ili aishi naye kama mwanaye kabla ya kupokea taarifa za kitendo chake cha kumnyonga mwanaye.
Akiongoza lbada ya mazishi Padri John Greyson wa Kanisa la Kolla la Mwili na Damu ya Yesu, aliwaliza watu baada ya kusema marehemu alikuwa miongoni mwa watoto waliokuwa wapokee Ekaristi Takatifu mwishoni mwa mwaka huu.
Wanafunzi wakiuaga mwili wa mpendwa wao Edyline Barnabas Mafwere.
Naye mwakilishi wa Shule ya Kata ya Kolla Hill aliyokuwa akisoma Judith, Mwalimu Neema Lupena alisema ni jambo la kusikitisha kuwa mtuhumiwa wa mauaji ni mwanafunzi wao wa kidato cha kwanza, lakini akasema alipokelewa shuleni hapo licha ya nafasi kujaa kutokana na heshima ya baba yake mdogo.

MICHEPUKO IMEPELEKEA MPENZI WA FACEBOOK AMNYONGA MKE WA MTU GESTI!

Marehemu Ashura Maulid enzi za uhai wake.
Tukio hilo lililojaa majonzi tele na kuacha maswali mengi, hasa kwa mume wa marehemu, Suleiman Othman, lilijiri  Mei 19, mwaka huu kwenye nyumba ya kulala wageni (jina lipo) iliyopo kandokando ya barabara ya kutoka Sinza Afrikasana kwenda Kijitonyama kupitia Kituo cha Polisi cha ‘Mabatini’, Dar.
Chanzo kinadai kuwa, enzi za uhai wake, mwanadada huyo alikuwa akijihusisha na biashara ya kuuza duka la friji maeneo ya Sinza ya Afrikasana na inasemekana amekuwa ndani ya ndoa na mumewe, Suleiman kwa miaka 15 na kujaliwa kupata watoto wawili, wa mwisho akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.
Akizungumza na Uwazi, Ijumaa iliyopita huku akiwa katika majonzi mazito, mume huyo alisema Jumanne ya Mei 19, mwaka huu, mkewe alimuaga anakwenda kazini huku akiumwa, alimtaka apumzike lakini mwanamke huyo akasema anajiona amepona hivyo ana uwezo wa kumudu majukumu yake.
“Ilipofika saa moja usiku akanitaarifu kuwa ameshatoka kazini. Cha ajabu mpaka saa nne usiku alikuwa hajafika nyumbani na nilipompigia simu hakupokea.“Mara kwa mara mke wangu alipokuwa akimaliza kazi na kuanza safari ya kurudi nyumbani alikuwa ananitaarifu, nachati naye kila wakati mpaka anafika. Siku hiyo nilikuwa nina majukumu mengi aliponitaarifu kamaliza kazi ndo’ anarudi sikuwa na presha.
“Sasa ilipofika saa nne mimi nikiwa nyumbani na simu hapokei, nikashangaa. Mbaya zaidi, baadaye simu yake ikawa haipatikani kabisa.“Nilifanya jitihada za kumtafuta kwa ndugu na jamaa, vituo vya polisi na hospitali mbalimbali, ikiwemo Muhimbili kuulizia kwenye wodi za wagonjwa lakini sikumkuta.
Mume wa marehemu Ashura Maulid.
“Juzi (Mei 20), nilishtuka kupigiwa simu na polisi wa Kijitonyama, wakaniambia kuna maiti imekutwa mahali (walimficha kama ilikuwa gesti) na aliyehusika na mauaji ni mwanaume ambaye walianza kufahamiana na mke wangu kupitia Facebook. Walisema marehemu alionekana alikufa kwa kunyongwa.
“Waliniambia huyo mwanaume alikimbia baada ya kufanya mauaji hayo. Palepale ndo’ wakaanza jitihada za kumtafuta mpaka wakamkamata,” alisema mume huyo.Akiendelea kuelezea tukio hilo alisema kisa cha kugundua kuwa Charles alikutana na mke wake kwenye Facebook ni siku ya tukio baada ya mawasiliano waliyoyafanya kwa kipindi kirefu bila yeye kujua.
Alisema ilionesha kuwa, siku hiyo waliamua kuonana laivu ambapo alimkaribisha dukani kwake na kuondoka naye baada ya kumaliza kazi na kufunga duka huku akiwa amemtaarifu bosi wake (si mumewe) fedha zilizopatikana siku hiyo.
“Niliambiwa na rafiki wa mke wangu kuwa siku hiyo mwanaume huyo alifika dukani kwa mke wangu akawatambulisha mashosti zake kuwa ni rafiki yake waliyejuana Facebook. Wakiwa hapo, mke wangu  alimpigia simu bosi wake kumwambia siku hiyo aliingiza shilingi milioni moja na laki saba. Huenda hicho ndo’ kilimfanya jamaa amgeuke na kumuua kwa tamaa ya zile fedha,” aliongeza.
Mumewe huyo alisema, haamini kama mkewe alishindwa kuiheshimu ndoa yake na kuwapa nafasi wanaume wengine tena kwa kwa mtu ambaye hakufahamiana naye ila kwa kukutana naye kwenye mtandao na kuanzisha uhusiano kwani yeye alimtosheleza kwa kila jambo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alipotafutwa ili aulizwe kuhusiana na tukio hilo, simu yake iliita bila kupokelewa.Uwazi lilipofika kwenye gesti hiyo ambayo marehemu alifia chumba Namba 4 lakini wahusika  waligoma kutoa ushirikiano na kudai hakukuwa na tukio hilo.
Kesi  hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ faili Namba KJN/RB/5081/15 TAARIFA YA KIFO huku mtuhumiwa akishikiliwa hapo baada ya kukamatwa akiwa na gari aina ya Toyota Carina (namba za usajili zipo).

WATOTO WAWILI NDUGU TUMBO MOJA WAFIA KWA GWAJIMA

 “KWA kweli sisi kwetu kama kanisa ni maajabu na mshtuko. Inapotokea ajali kama hii bila kutarajia lazima kutokee mshtuko. Hakuna anayependa kutokea kwa hali hii, tumuombe Mungu. Najua mengi yatasemwa lakini ukweli ni kumuachia Mungu tu,” ndivyo alivyoanza kusema Askofu Yekonia Byabaza ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Marehemu Sarah enzi za uhai wake.
Askofu Byabaza aliyasema hayo alipozungumza na Gazeti la Uwazi kufuatia vifo vya watoto wawili ndugu wa damu moja, Sarah (10) na Goodluck David Oturo (4) waliokufa kwa kunaswa na umeme wakiwa kwenye ibada katika kanisa hilo, Kawe jijini Dar wiki moja iliyopita.
Askofu huyo alizungumza na Uwazi kwenye ibada maalum ya kuaga miili ya marehemu hao iliyofanyika nyumbani kwa wazazi, Mbezi Juu jijini Dar es Salaam, Alhamisi iliyopita.
Aliendelea kusema: “Ninachokijua ni kwamba hali hiyo imetokea kwa wote baada ya Goodluck ambaye ni mdogo alipoona dada yake amenaswa na umeme alimfuata na kumgusa huku akilia na kusema; dada… dada…ndipo na yeye akanaswa lakini siyo kwamba kuna jambo. Mungu alipanga kuwa vifo vyao vitatokana na njia hiyo.”
Marehemu Goodluck enzi za uhai wake.
MASWALI YA WANAFUNZI
Katika msiba huo uliowaacha midomo wazi waombolezaji, wanafunzi waliokuwa wakisoma na Sarah walikuwa na maswali kwa muda mrefu:
“Kwa nini iwe familia hiyo tu? Kwa nini iwe Sarah na mdogo wake tu? Mbona kulikuwa na watoto wengi! Halafu tunasikia waya uliomnasa Sarah haukuwa umechubuka, sasa kwa nini anaswe?”
Wanafunzi hao muda mwingi walikuwa wakitokwa machozi kupindukia huku wengine wakiishiwa nguvu.
Mmoja wa wanafunzi aliyejitambulisha kwa jina moja la Samuel alisema kwamba, Sarah alikuwa mpole na alikuwa akipatana na kila mmoja, hakuwa mgomvi na alikuwa ana uwezo mkubwa darasani.
Mama wa marehemu hao akilia kwa simanzi kubwa wakati wa kuaga miili hiyo.
KITAALAM
Mtu mmoja msibani hapo ambaye alijitambulisha kuwa ni fundi umeme, alisema kuwa, kwa umeme wa majumbani, mtu akivaa viatu hata kama atakanyaga waya wenye umeme si rahisi kunaswa na kufa.
“Napata shida sana kama kweli Sarah alikanyaga waya wenye umeme. Mbona alivaa viatu tena viatu vyenyewe havikuwa na chuma, kwa nini anaswe? Haya kwangu ni maajabu hasa ninapoambiwa hata huo waya wenyewe haukuwa umechubuka,” alisema fundi huyo.
MAJIRANI, WAALIMU WAZIMIA
Ili kuonesha kuwa, vifo vya watoto hao viligusa wengi, baadhi ya majirani sambamba na walimu wa marehemu Sarah, jumla yao ikipata tisa, walianguka na kupoteza fahamu wakati wakipita kwenye majeneza kuiaga miili hiyo.

Baba wa marehemu hao(katikati) akiaga miili ya wapendwa wake.
MSEMAJI WA FAMILIA
Kutokana na hofu na mkanganyiko wa vifo hivyo kutanda, gazeti hili lilizungumza na ndugu wa karibu wa marehemu hao ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini na kumuuliza juu ya maoni ya familia hiyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa kweli kwangu haya ni maajabu! Mimi si msemaji mkuu wa familia lakini ninachokijua ni kwamba, marehemu kabla ya vifo vyao  walishatuhangaisha sana kwa kuumwa, hasa Goodluck. Na ajabu ni kwamba, kuumwa huko, tulipowapeleka hospitali hawakupata nafuu lakini tulipowapeleka kwa waganga wa kienyeji walipona.
“Kifupi ni kwamba, ukisimuliwa historia ya maisha yao kwa ujumla ilitafsiri vifo. Inatuuma sana! Ajabu ya magonjwa yao, walikuwa wakipelekwa kwa waganga wa kienyeji wanapata nafuu.“Baba yao amehangaika nao mpaka basi hali iliyomfanya mama yao kuamua kuwapeleka katika maombi kwa Askofu Gwajima.”
Wanafunzi wakilia kwa uchungu.
Msemaji huyo: “Nakumbuka Goodluck akiwa na umri wa miaka miwili, siku moja tukiwa ndani ya nyumba iliibuka harufu ya dawa za kienyeji, ghafla yeye alianza kunyooka huku akipoteza fahamu. Alipelekwa hospitali ikashindikana, akapelekwa kwa waganga wa miti shamba akapata nafuu.”
MWAKA MMOJA BAADAYE
“Baada ya mwaka moja alianza kuumwa tena, akawa anatembea huku akizunguka huku na kule bila kusema na mtu. Alionekana kama yupo kwenye ulimwengu wa pekee. Aliweza kupona kwa mganga.
Mmoja wa waombolezaji akiwa amezimia.
“Safari ya tatu akawa anatembelea makalio huku Sarah naye akianza kuumwa tumbo na kuwa mpole sana. Tuliamua kuwapeleka hospitali mbalimbali lakini hawakupona, tulipowapeleka kwa mganga wa miti shamba wakapona.
“Ndipo tulipogundua kuwa kuna mchezo mchafu unafanyika na hapo ndipo mama yao akawa anakwenda nao katika maombi. Nafikiri mengi zaidi mkamuulize baba yao.”
WAZAZI WASIMULIA
Baba mzazi wa marehemu hao, David Oturo yeye kwa upande wake alikiri kuumwa kwa watoto hao magonjwa ya ajabu ambapo alipokuwa akiwapeleka hospitali hawakupona bali walipata nafuu walipopewa dawa za kienyeji.“Na mimi nimepatwa na mshtuko kuhusiana na vifo vya watoto wangu.
Waombolezaji wakiwa na nyuso za majonzi.
Nimehangaika nao kwa muda mrefu na nilijua wameshapona, ndiyo maana nilimruhusu mama yao kwenda nao kwenye maombi. Sikutegemea kama mauti yangewakuta wote kwa siku moja kule kanisani. Lakini yote namuachia Mungu,” alisema kwa masikitiko mzazi huyo.
Akizungumza na Uwazi, mama mzazi wa marehemu hao alisema:
“Vifo vya watoto wangu siku hiyo kama niliviona tangu nyumbani. Ajabu ni kwamba, moyo wangu siku hiyo ulikuwa na ganzi kwenda kanisani. Lakini nikajipa nguvu tukaenda, kumbe ningeusikiliza moyo nikaacha kwenda, wanangu wasingekufa.
“Lengo la kuwapeleka kwa Askofu Gwajima ni kuombewa ili magonjwa ya ajabuajabu yawatoke, wawe salama nikijua hata kukwepesha vifo vyao maana kusema ule ukweli mimi na mume wangu tulihangaika nao sana, nikajua kwa Gwajima ndiyo nimefika kumbe bado!
Majeneza yaliyobeba miili hiyo yakiombewa kwa ajili ya mazishi.
MIILI YASAFIRISHWA
Miili ya watoto hao ilisafirishwa Ijumaa iliyopita kwenda Musoma mkoani Mara kwa mazishi yaliyofanyika Jumamosi. Oturo kwa sasa amebaki na mtoto mmoja wa kiume, mkubwa kwa wote.
Uwazi linatoa pole kwa familia ya Oturo kwa msiba mkubwa uliowapata na Mungu awape uvumilivu. Bwana ametoa Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe! Amina.Imeandaliwa
Na: Makongoro Oging’, Shani Ramadhani, Haruni Sanchawa na Gabriel Ng’osha.

BEYONCE na JAY Z MAPENZI MAZITO KAMA VILE WAMEANZA JANA!

PENZI ni kikohozi kulificha huwezi! Ndivyo ambavyo wanaonyesha wapenzi wawili maarufu duniani, rapa Jay Z na mwimbaji Beyonce ambao hivi sasa wapo nchini Italia wakila raha na unaambiwa wamekuwa wakigandana na kuonyeshana mahaba hadharani utadhani walianza mapenzi yao jana kwa jinsi walivyoshibana.


Jay Z, 45, na Beyonce, 33, ambao kwa miezi kadhaa iliyopita walidaiwa wapo katika mgogoro wa ndoa, wameonyesha ndiyo kama mapenzi yao yameanza upya wakiwa wanakula bata katika Jiji la Florence.
Wawili hao ambao ni miongoni mwa wapenzi matajiri zaidi duniani, walionekana wakikatiza sehemu mbalimbali jijini humo huku wakionekana kuwa na nyuso za furaha.

WAPIGANAJI WA AL SHABAAB WADAI KUWAUA POLISI ZAIDI YA 20 NCHINI KENYA

Wanamgambo wa Al Sbaab wamekuwa wakitishia hali ya usalama nchini Kenya daaba ya kudai kuwaua askari zaidi ya 20 na kujeruhi mmoja baada ya kuwepo kwa mapigano makali kati ya Polisi na Wanamgambo wa Al Shabaab, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Wizara ya Usalama wa Taifa nchini Kenya imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la Wanamgambo wa kundi la Al Shabaab katika kijiji cha Yumbis mjini Garissa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Viongozi katika eneo hilo wamesema Magari manne ya Polisi yamechomwa moto na wanamgambo hao wakati huo Polisi wamesema kuwa wamepeleka kikosi kuimarisha hali ya usalama katikia eneo hilo.
Aidha tarifa za awali zilieleza kuwa, askari kadhaa wanahofiwa kufa kwenye kwenye shambulio la usiku wa jumatatu.
Wakati huo huo, Al Shabaab wamedai kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi zaidi ya 20, lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo ni Propaganda.
Siku ya jumatatu Polisi watatu walijeruhiwa baada ya Gari lao kukanyaga Bomu la kutegwa ardhini.
Kikosi cha askari 20 kilifika katika eneo hilo kuwasaidia waliojeruhiwa wanaoelezwa kushambuliwa na Al Shabaab.
Al Shabaab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo na kuchoma magari mjini Garissa.
Msemaji wa kundi hilo Shaykh Abdiasis Abu Mus’ab amesema shambulio hilo limefanywa na kikosi maalum kiitwacho ‘mujahidin’.
Mus’ab amesema shambulio lilikuwa la “mafanikio” na kudai kuwa hasara waliyoipata askari wa Kenya ni kubwa.
 NA BBC

ZARI APIGA YOWE KWA KUVUJA KWA PICHA ZAKE NA KATUNZI

MUSA MATEJA
MCHUMBA wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Zarina Hassan ‘Zari’ amedaiwa kuangua kilio baada ya kuvuja kwa picha yake na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Mzamili Katunzi ambayo ilidaiwa kuwa ni mtu wake na kusababisha gumzo mjini.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi.
Mtu wa karibu na Zari amefunguka kuwa Zari alijisikia vibaya sana baada ya kuona picha hiyo na kukasirika hivyo kuanza kuwasaka watu walioivujisha kwani walikuwa na nia mbaya ya kumgombanisha lakini wamechemka.
“Zari kamaindi kweli, anajiuliza huyo aliyeivujisha alikuwa na lengo gani?” alisema mtu huyo.
Supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’.
Jitihada za kuzungumza na Zari hazikuzaa matunda lakini bahati nzuri Diamond alipatikana na kufafanua:
 “Ni kweli zimemsumbua baby lakini nimemuweka sawa kwa kuwa najua ni mambo ya mitandao, hakuna ukweli wowote.”

HII NDIO PICHA YA DIAMOND AKILA MISHIKAKI MTAANI AMBAYO IMELETA GUMZO

PICHA ya staa wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayomuonesha akila mishikika uswahilini imezua gumzo la aina yake mitandaoni.

Staa wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akila mishikika uswahilini.
Picha hiyo ambayo ilipigwa mwaka mmoja uliopita maeneo ya Tip Top, Manzese jijini Dar, imeibua mjadala mpya juzikati kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengine walimpongeza kwa kitendo hicho wengine wakisema si cha hadhi yake.
“Hii ni nzuri kwa mtu kama Diamond akila uswahilini. Anaonesha siyo mtu wa majivuno,” alichangia mdau mtandaoni huku wengine wakidai si sawa kwani anajiabisha.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Baada ya chanzo hicho kuipata picha hiyo na kumtumia mwandishi wetu, Mikito Nusunusu ilimtafuta Diamond ili aweze kuizingumzia lakini simu yake haikupatikana lakini Bab Tale alipatikana na kukiri maelezo ya chanzo chetu.
“Hakukuwa na ishu zaidi ya kuitamani mishikaki, tukaona tununue, mbona ni ya toka mwaka jana?,” alisema Bab Tale.

JOKATE AMLIPUA DIAMOND HADHARANI!

Jino kwa jino! Sexy lady anayefanya poa na ngoma yake ya Leo Leo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, amemlipua aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye hivi karibuni alimwita makombo baada ya kusikia kwa sasa anatoka kimalovee na msanii Ali Kiba.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata yeye ni makombo na bado anakula makombo?
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
“Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia kuwa ninatoka  au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii.
“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond na kuongeza:
“Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya msingi ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na hiyo.”

SHILOLE AOMBA MSAMAHA KWA AKINA MAMA WOTE NISAMEHENI


BAADA ya wiki kadhaa kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni likiwa limevuka nakuachia ‘nido’ wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akipiga stori na Over The Weekend, Shilole alisema kuwa anajua kwamba kitendo hicho kimewakwaza wengi na hakukusudia kufanya jambo kama lile. “Nimejifunza mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili halitajitokeza tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,” alisema. Shilole alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji kwenye shoo ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda.

BAADA YA KUPIGWA CHUPA UBONGO WA KAJALA WAPATA TATIZO

Maskini Kajala! Ndivyo unavyoweza kusema ukisikia mkasa wa staa wa kiwango cha juu kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’, ambaye anadaiwa kwa hivi sasa hayuko sawa kiafya baada ya kupigwa chupa kichwani akiwa katika shoo ya kumchangia mke wa msanii Mabeste iliyofanyika New Maisha Club, Masaki jijini Dar.
Kajala Masanja akionekana na jeraha usoni kipindi ambacho alikua amepigwa chupa.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala kimeliambia Ijumaa Wikienda kwamba, tangu staa huyo akumbwe na sekeseke hilo amekuwa katika kipindi kigumu kwani amekuwa akipata maumivu makali sehemu ya kichwani huku akianguka mara kwa mara.
Kajala Masanja.
Kilidai kwamba, pia Kajala amekuwa akipata kizunguzungu kikali hivyo kujiona yupo kwenye hatari kubwa hasa ikitokea akaanguka vibaya kwani anaweza kupoteza maisha.
 ASHINDWA KUENDESHA GARI
Mpashaji wetu huyo aliweka wazi kuwa tangu Kajala akumbane na mkasa huo mzito uliomsababishia kushonwa nyuzi mbili juu ya jicho, amekuwa hayuko vizuri na kuna wakati hawezi hata kuendesha gari hivyo kukwamisha shughuli zake za kila siku.
“Kiukweli Kajala hayupo vizuri kabisa,  amekuwa kwenye kipindi kigumu mno tangu alipopigwa chupa klabu.
“Amekuwa akianguka mara kwa mara kutokana na kizunguzungu kikali anachopata akisimama au kutembea,” kilisema chanzo hicho.
 CT-SCAN;mfano wa mashine ambayo Kajala amefanyiwa vipimo.
ATINGA HOSPITALINI
Habari zilizidi kumiminika kuwa, baada ya kuona hivyo Kajala alikwenda kwenye Hospitali ya Regency iliyopo Upanga jijini Dar kwa ajili ya kufanya vipimo.
 AFANYIWA CT-SCAN
Kilisema kuwa alipofika hospitalini hapo alifanyiwa kipimo cha CT-SCAN kichwani ambapo majibu yalipotoka aliambiwa kuwa kinachomsumbua ni damu iliyoganda sehemu aliyopigwa chupa.
 MAJIBU YA DAKTARI
“Daktari alimpa majibu ya kushangaza maana alimwambia kama angezembea, tatizo lingekuwa kubwa sana kwenye ubongo na lingeleta shida zaidi,” kilisema chanzo hicho.
 HUYU HAPA KAJALA
Baada ya kunyetishiwa mkasa huo wa kusikitisha, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kajala ili kuthibitisha tatizo hilo alilokuwa nalo ambapo alikiri kuwa alikuwa akihisi kizunguzungu kikali cha mara kwa mara lakini hakuwa amegundua kama alikuwa na tatizo la kuvilia damu kichwani.
“Lakini kwa sasa namshukuru Mungu niko sawa kidogo. Ukweli nilikuwa napata shida sana kila nikiinuka, napata shida ya kizunguzungu kikali sana,” alisema Kajala.
 TUJIKUMBUSHE TUKIO
Wakati Kajala akitoka Klabu ya New Maisha hivi karibuni, akiwa anashuka kwenye ngazi, ghafla alishangaa kurushiwa chupa kichwani iliyosababisha kuanguka kutoka kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na wasamaria wema waliompeleka katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar ambapo alishonwa jeraha alilolipata.
Katika sakata hilo, Kajala alisema kuwa mtu aliyempiga chupa ni mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio hilo alikuwa  hamjui na wala alikuwa hajawahi kumuona.

HAWA NDIO VINARA WA ‘KUUZA MECHI’ KWA WANAWAKE TOFAUTI!

Staa wa Bongo fleva, Ali Kiba.
Kama hujaelewa, Kuuza mechi ni kushiriki tendo la ndoa bila kinga. Wakati mwingine hutokea kwa bahati mbaya lakini kama itatokea zaidi ya mara moja, lazima watu watakuwa na mtazamo tofauti na wewe, inaonesha ni jinsi gani ni kinara kwenye suala hilo la kuuza mechi.
Uchunguzi unaonesha kuwa kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo, kuna wasanii lukuki ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki katika ishu hiyo na matokeo yake ni kuwa na watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
Makala haya yanakuletea listi ya vidume mastaa wa Bongo ambao wana watoto waliozaa na wanawake tofauti;

Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes.
ABDUL SYKES ‘DULLY’ (watoto watatu)
Huyu ni legendary wa Bongo Fleva ambaye hivi karibuni alifikisha miaka 15 katika muziki anaoufanya. Ana watoto watatu ambao anakiri kuzaa na wanawake tofauti ingawa majina ya mama zao huwa ni siri yake.

ALI SALEH KIBA (watoto watatu)
Kiba ni staa mkongwe mwenye mashabiki wengi anayekimbiza na mzigo mpya wa Chekecha Cheketua. Jamaa huyu anaingia katika orodha ya wauza mechi kwa kuwa anakiri kuwa na watoto watatu aliozaa na wanawake tofauti.
Q-Chillah akifikiria jambo wakati akihojiwa na Global TV Online.
ABOUBAKAR KATWILA ‘Q CHILLAH’ (watoto watatu)
Chillah kama ilivyo Dully naye ni legendary wa Bongo Fleva. Jamaa anakiri kuwa na watoto watatu, akiwa amewapata kwa wanawake tofauti ambao siyo mastaa kama alivyo yeye.

KHALEED MOHAMED ‘TID MNYAMA’ (watoto wawili)
Huyu ni mkali wa ngoma kibao kama Zeze, Nyota Yangu, Siku Kama Hizi, Kiuno na nyingine kibao ambazo ziliwahi kuwa nyimbo za taifa. Jamaa ana watoto wawili akiwa amezaa na wanawake tofauti. Mmoja alikuwa maarufu aliyejulikana kwa jina moja la Kinana.
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Khaleed Mohamed 'TID'.
EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’ (watoto watatu)
Jamaa anatikisa kwenye Bongo Fleva kwa sasa. Nay anaingia kwenye orodha hii akiwa na watoto watatu, mmoja alizaa na dada wa Kihindi (jina halifahamiki), akazaa na msanii wa Bongo Movies, Skyner Ally na mtoto wa mjini, Siwema Edson.

MACK SEKIMANGA ‘MAKAMUA’ (watoto wawili)
Jamaa ni mmoja wa wakali wa RnB Bongo aliyewahi kutamba na ngoma kama Tell Me Why na nyinginezo. Hakosi kwenye orodha hii kwa sababu ana watoto wawili ambapo kila mmoja ana mama yake.

KULWA KIKUMBA ‘DUDE’ (watoto saba)
Jamaa ‘bana’ ni tishio na  ndiye anaongoza kwa kuwa na watoto wengi kwa wasanii wa Bongo. Dude  ana watoto saba kwa wanawake wanne tofauti. Siku zote amekuwa muwazi kuhusu suala hilo.

SHOPPING YA MTOTO WA DIAMOND KUFURU!

KAMA ulishawahi kusikia neno kufuru na ukajua maana yake, basi ndiyo imefanywa na Mwanamuziki Bora wa Afrika Mashariki na Kati, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, baada ya kuteketeza mamilioni ya fedha kwa ajili ya kufanya ‘shopping’ ya nguo na vifaa mbalimbali vitakavyotumiwa na mwanaye ikiwa ni siku chache kabla mpenzi wake, Zarinah Hassani ‘Zari The Boss Lady’ kujifungua.

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akifanya shopping ya mtoto wake anayetarajiwa kuzaliwa.
KITU CHA DUBAI NA LONDON
Akizungumza na Ijumaa mapema wiki hii, mtu wa karibu wa Diamond anayekuwa naye popote anapokwenda alisema kuwa shopping hiyo aliifanya juzikati huko Dubai na jijini London, Uingereza ambako alikwenda kufanya shoo yake ya Diamonds Are Forever.
Alisema kuwa, akiwa London baada ya shoo, Diamond aliona ni vema akafanya manunuzi hayo kwani hivi karibuni atapata mgeni (malaika) kwenye familia yake.
 KUMBE ALIANZA KITAMBO
Mtu huyo aliendelea kunyetisha kwamba, Diamond alinunua vitu vingi zaidi ya hivyo ambavyo alivipiga picha kwani hata kabla ya kununua huko London tayari kuna baadhi alinunua njiani na kuna siku alinunua vingine jijini Dar.
Alisema kuwa kwa harakaharaka hadi sasa vitu ambavyo Diamond ameshanunua ukivipigia gharama ni zaidi ya Sh. milioni 10 za Kitanzania.‘Diamond Platnumz’ akishika tumbo la Zari.
“Mimi nipo na Diamond karibia kila sehemu anakoenda, nataka kukufahamisha kwamba, hivyo vitu ambayo amevianika ni vichache sana maana tangu siku tunaenda London kuna ‘mazagazaga’ kibao alinunua njiani.
“Ukiachia mbali hivyo vitu ambavyo mimi nimevishuhudia kuna vingine vingi,” alisema mtu huyo kwa sharti la kutochorwa gazetini.
 ZARI AANDALIWA BONGE LA PATI
Jamaa huyo aliendelea kutiririka kuwa, pamoja na kutumia mkwanja huo mrefu kwa shopping pia Diamond amejipanga kwa hali na mali kumuangushia Zari bonge la pati inayofahamika kwa jina la Baby Shower ambayo wajawazito wengi huwa wanafanyiwa kabla ya kujifungua na kuzawadiwa baadhi ya mahitaji ya mtoto wa kike atakayezaliwa.

BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, paparazi wetu alifanya mahojiano na Diamond kwa lengo la kutaka kujua gharama za mazagazaga hayo ambayo amenunua kwa ajili ya mwanaye.
Zari akijipiga picha.
Diamond aliweka wazi kwamba kile kitoroli kimoja cha mtoto pekee kilighalimu pauni 1,450 (zaidi ya Sh. 3,625,000).
Alisema kuwa vikorokoro vingine vina thamani ya pauni 1800 (zaidi ya Sh. milioni 4.5) hivyo kwa shopping ya London jumla alitumia pauni 3,250 (zaidi ya Sh. 8,125,000).
Alisema mbali na hivyo kuna vitu vingine ambavyo alivinunua nje ya shopping hiyo hivyo amesahau ni vya aina gani na thamani yake ila kwa harakaharaka hivyo ndivyo anavyokumbuka ingawa thamani inaweza kuwa imepitiliza kwenye Sh. milioni 10 kama kila kitu akikipigia hesabu sawasawa.
“Nafahamu watu wengi wanaweza kushindwa kuamini au kunielewa vizuri ila kweli nimetumia gharama kubwa kununua vitu hivyo ikiwa ni maandalizi ya mwanangu tu.
“Ukweli mimi sitakuwa wa kwanza Tanzania na duniani kununua vitu kama hivyo japokuwa kuna watu wasioacha kubeza wataongea wanachowaza wao,” alisema Diamond.
 WAKOSOAJI WA MAMBO YA WATU
Kwa mujibu wa wakosoaji wa mambo ya watu waliozungumza na gazeti hili baada ya kusikia ishu hiyo walidai kwamba Diamond amefanya kufuru kubwa kwani kuna Watanzania wengi hawana hata fedha ya kununulia kidonge lakini yeye anateketeza mamilioni kwa shopping ambayo hata mtoto bado hajazaliwa.
“Unajua hatuombei litokee jambo baya lakini huyu dogo (Diamond) amefanya kufuru sana maana hata mtoto mwenyewe hajamuona.
“Kibongobongo kuna watu wengi wanasota wanakosa hata mlo mmoja kwa siku lakini yeye anateketeza mamilioni. Ni sawa lakini ajue kuna leo na kesho. Yupo wapi… (anatajwa jamaa mmoja aliyekuwa msanii mkubwa Bongo lakini kwa sasa amefulia).
“Jamaa anatakiwa kuangalia vitu anavyovifanya ili kesho na keshokutwa watu wasisema tulisema..,” alisema mmoja wa wakosoaji hao.
 AGEUZIWA KIBAO
Hata hivyo, wakati mkosoaji huyo akiendelea, mmoja wa Team Diamond aliingilia mazungumzo:
“Acheni hizo, kwa levo ya Diamond lazima afanye hivyo na ukizingatia ni mwanaye wa kwanza. Jamani kwani shopping ya milioni kumi kwa Diamond ni kitu gani? Hivyo ndivyo zinavyokuwa shopping za watoto wa mastaa.
Wewe muone North wa Kanye West na Kim Kardashian anavyofanyiwa shopping ndiyo utajua Diamond ni cha mtoto.”