WAPIGANAJI WA AL SHABAAB WADAI KUWAUA POLISI ZAIDI YA 20 NCHINI KENYA

Wanamgambo wa Al Sbaab wamekuwa wakitishia hali ya usalama nchini Kenya daaba ya kudai kuwaua askari zaidi ya 20 na kujeruhi mmoja baada ya kuwepo kwa mapigano makali kati ya Polisi na Wanamgambo wa Al Shabaab, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Wizara ya Usalama wa Taifa nchini Kenya imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la Wanamgambo wa kundi la Al Shabaab katika kijiji cha Yumbis mjini Garissa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Viongozi katika eneo hilo wamesema Magari manne ya Polisi yamechomwa moto na wanamgambo hao wakati huo Polisi wamesema kuwa wamepeleka kikosi kuimarisha hali ya usalama katikia eneo hilo.
Aidha tarifa za awali zilieleza kuwa, askari kadhaa wanahofiwa kufa kwenye kwenye shambulio la usiku wa jumatatu.
Wakati huo huo, Al Shabaab wamedai kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi zaidi ya 20, lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo ni Propaganda.
Siku ya jumatatu Polisi watatu walijeruhiwa baada ya Gari lao kukanyaga Bomu la kutegwa ardhini.
Kikosi cha askari 20 kilifika katika eneo hilo kuwasaidia waliojeruhiwa wanaoelezwa kushambuliwa na Al Shabaab.
Al Shabaab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo na kuchoma magari mjini Garissa.
Msemaji wa kundi hilo Shaykh Abdiasis Abu Mus’ab amesema shambulio hilo limefanywa na kikosi maalum kiitwacho ‘mujahidin’.
Mus’ab amesema shambulio lilikuwa la “mafanikio” na kudai kuwa hasara waliyoipata askari wa Kenya ni kubwa.
 NA BBC

No comments:

Post a Comment