PENZI LA NEY WA MITEGO LASABABISHA WASANII KUCHAPANA HADHARANI MCHANA KWEUPE TENA BAA

HII sasa kali! Wasanii wa sinema ndani ya Bongo Movies, Fatuma Ayubu `Bozi’ na Brenda Marembeka `Kunguru’ wametoa aibu ya mwaka baada ya kupigana kwenye baa tena mchana kweupe kwa kile kilichodaiwa walikuwa wakigombea mabwana ambao ni mastaa  wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ huku Kasim Yusuf `Young D’ naye akitajwa.
Wasanii wa sinema ndani ya Bongo Movies, Fatuma Ayubu `Bozi’ na Brenda Marembeka `Kunguru’ wakiamuliziwa baada ya kuzichapa.
Sekeseke hilo la aina yake lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye Baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar ambapo kwa mujibu wa shuhuda mmoja wa tukio hilo, Bozi alitangulia kufika mahali hapo na kuagiza kinywaji.
WALIFIKA TOFAUTI
“Baada ya muda yule mwenzake (Kunguru) akafika na kuanza kumrushia vijembe mwenzake kisha kummwagia kinywaji chake na kumvua wigi alilokuwa amevaa.“Yaani hawa wasanii siyo siri wanaidhalilisha tasnia. Yule mwenzake alipofika tu, bila hata salamu akaanza kumtupia maneno makali mwenzake huku akimtuhumu kwa nini alitembea na bwana wa rafiki yake ambaye ni Nay wa Mitego kisha akaanza  kumkunja.
WAUMBUANA
“Yule mwingine (Bozi) akapamba moto na yeye, akasimama na kumuwakia mwenzake akimwambia  alitembea na bwana wake ambaye ni Yuong D. Yaani wamesababisha watu kujazana na kusitisha shughuli zao,” alisema shuhuda huyo.

MENEJA APATA WAKATI MGUMU
Wakati maparazi wanafika eneo la tukio walimkuta mtu mmoja aliyetambulishwa kuwa ni meneja wa baa hiyo akiwa katikati kuwaamua wasanii hao na kuambiwa waondoke.

Wakitupiana maneno baada ya kuamuliziwa.
WAHUDUMU PIA WANENA
Mbali na meneja kuwataka waondoke, wahudumu wa baa hiyo maarufu nao walionekana kutofurahishwa na kitendo cha wasanii hao kuzichapa kwenye baa hiyo kiasi cha kuwabughudhi wateja. Waliwatolea matusi mazito ambayo hayaandikiki gazetini huku wakiwaambia siku wakiziona sura zao kwenye baa hiyo wataishia polisi.

WENYEWE SASA
Baadaye kwa njia ya simu, mapaparazi wetu waliwatafuta wasanii hao, kila mmoja kwa wakati wake na kuwahoji juu ya ugomvi wao uliosababisha kujaza watu baa ambapo kila mmoja alimtupia lawama mwenzake kwa usaliti.

BOZI
“Yule Kunguru kwa kipindi kirefu hatujaonana na wala hatuongei. Cha ajabu leo nimekaa zangu pale baa nastarehe, hata sijui alipotokea, kaja na kuanza kunichokonoa. Ukweli mimi niliwahi kuwa na uhusiano na Young D kabla yake, yeye akaiba namba kwenye simu yangu wakatongozana mpaka kuwa wapenzi na huenda wameshaachana, sasa sijui kimemuuma nini? Labda alijua angeolewa.”


Staa  wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
KUNGURU
 “Sitaki kumuongelea huyo mtu, hana maana yoyote nitampa ujiko tu. Yeye alijua rafiki yangu (hakumtaja jina) anatoka na Nay na yeye akajipeleka. Kiko wapi sasa? Mbona kaachwa! Tena ndiyo kwanza kaambulia kusambaziwa picha zake za utupu mitandaoni.

NAY, YOUNG D
Kwa upande wake, Young D alipotafutwa kwa simu na kuambiwa kuhusu wasanii hao aligoma kuwazungumzia. Nay yeye alipoulizwa alianza kwa kucheka, akasema: “Ha! Ha! Mimi sijawahi kuwasikia hao watu na siwajui kabisa labda kuna kitu wanakitafuta kutoka kwangu.”
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS

HII NAYO KALI ETI TUMBO LA LULU LAYEYUKA GHAFLA


Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka na yupo ‘flati skriini’.
Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano wa Umma, akiwa hana lile tumbo la Aprili.Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walidai msanii huyo alikuwa hafiki chuoni hapo kwa muda mrefu lakini sasa amejaa tele ‘mwepesii’.
“Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’ kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,” alisema mmoja wa wanachuo hao.Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila majibu.
Baadaye alitumiwa ujumbe wa kwanza uliosomeka: “Tafadhali naomba upokee simu, nahitaji kuzungumza na wewe jambo muhimu.” Hata hivyo, hakujibu.Baada ya kuona kimya, mwandishi wetu alimtumia ujumbe ulioonesha madai hayo: “Kuna tetesi kuwa ulinasa mimba na kuficha na sasa inadaiwa kutoka na kwamba hata chuoni haukuwa ukihudhuria, hili likoje?”
Baada ya kimya cha saa kadhaa, Lulu alijibu:
“Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.”
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.

MWANAMKE AMTUPA MWANAWE BARABARANI KUMKOMOA ALIYEZAA NAYE

UKATILI WA MAMA

UCHUNGU wa mwana si aujuae mzazi? Sasa mama mzazi huyu vipi?! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke Pendo Mabuko amejikuta akipokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira waliokerwa na kitendo chake cha kumtupa barabarani mwanaye wa kumzaa baada ya kunyimwa matumizi ya mtoto huyo na mwanaume aliyezaa naye, Daniel ambaye ni mume wa mtu.
Mtoto anayedaiwa kutupwa na mama yake, Pendo Mabuko.
Tukio hilo lililojaza umati lilitokea Ijumaa iliyopita, saa 10 jioni katika Mtaa wa Simu ‘A’ Kata ya Mji Mpya mkoani hapa.
Wakihojiwa na gazeti hili,  mashuhuda wa tukio hilo, Asha Hussein, Mussa Juma na Paskal Msimbe kwa nyakati tofauti, walisema:
”Tukiwa hapa barabarani tulimshuhudia huyu mwanamke na mwanaume mmoja wakizozana kwa muda mrefu, tulipowasogelea ili kuwasuluhisha, mwanaume alipanda bodaboda na kutimka.
“Ndipo huyu mwanamke akamtupa mtoto kisha naye akaanza kuondoka huku akisema amechoka kumlea mtoto wa mtu, sisi tukamzuia.
Mwanamke huyo akilia baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi waliokelwa ha kitendo hicho.
“Tulimlazimisha kumchukua mwanaye lakini aligoma, tukaamua tukuite wewe mwandishi kwa msaada zaidi.”
Wakati mwandishi wetu anawasili eneo la tukio, aliwashuhudia baadhi ya wananchi wenye hasira wakimshushia kichapo mwanamke huyo kwa kitendo cha kumtupa mwanaye.
Mwandishi aliita polisi wa pikipiki ambapo Afande Mwajabu alifika fasta na kumchukua mwanamke huyo na mwanaye na kuwapeleka  kituoni kwa mahojiano zaidi.  
Awali, akihojiwa na mwandishi wetu kuhusu uamuzi wa kumtupa mtoto wake barabarani, mwanamke huyo alisema:
”Muda huu tunatoka Ustawi wa Jamii kusuluhishwa. Mimi nilipeleka malalamiko, mzazi mwenzangu kagoma kumtunza mwanaye na kuniachia mzigo peke yangu.

Mama huyo akiwa mikononi mwa polisi.
“Nikimuuliza anasema mkewe kamzuia kumtunza mwanangu ndiyo maana na mimi kwa hasira nikaamua kumtupia mwanaye akamlee na mkewe.”

RAY ATESWA NA PICHA ZAKE ZA UTUPU MTANDAONI

Supastaa kunako Bongo Muvi, Vincent Kigosi, ‘Ray’ anateswa na tuhuma anazopata kutokana na mtu asiyejulikana kufungua akaunti feki ya Facebook yenye jina la Ray kisha kuposti picha za utupu.
Supastaa kunako Bongo Muvi, Vincent Kigosi, ‘Ray’.
Akizungumza na paparazi wetu, Ray alisema kuwa japokuwa ametoa ufafanuzi kupitia mtandao wake wa Instagram kuhusu picha hizo na akaunti hiyo feki, anashangaa kuona watu wanamuandama na kukomalia kwamba yeye anahusika.
“Yaani hii ishu inaniumiza na nimetoa ufafanuzi lakini sieleweki, naomba niseme kwamba mimi ni mtu ambaye najiheshimu sana, siwezi kufanya kitu kama kile mashabiki zangu waelewe hivyo tu,” alisema Ray.

KIMENUKA TENA KWA DAVINA:MUME AMCHANA LIVE DAVINA

KIMENUKA! Mume wa muigizaji nyota wa filamu nchini, Halima Yahaya ‘Davina’, Abdallah Shakoor ambaye amekuwa kimya tangu kuenea kwa madai ya mkewe kutoka na staa mwenzake, Mike Sangu, hatimaye amefunguka kuhusu skendo hiyo na kudai anafuatilia kila hatua ya wawili hao na hivi karibuni atatoa msimamo wake.
Muigizaji nyota wa filamu nchini, Halima Yahaya ‘Davina’.
Chanzo chetu makini kimeripoti kuwa wasiwasi wa mume huyo kwa mkewe ulianza muda mrefu uliopita, hasa baada ya staa huyo kusafiri kuelekea Iringa kwenye mazishi ya shangazi yake akiwa ameongozana na Mike, kitendo kilichomkera sana.
Inadaiwa kuwa kutokana na madai hayo kuandikwa magazetini mara kwa mara, yamesababisha familia ya mume kutaka kujua kinachoendelea baina ya wawili hao waliofunga ndoa yao Kiislamu.Gazeti hili lilipomtafuta mume wa staa huyo alisema anasikitishwa na kinachoendelea kwa kuwa alimpenda sana mkewe, lakini uvumilivu wake umefikia mwisho, hasa kufuatia kashfa zinazotajwa dhidi yake.
“Jamani hakuna mwanaume anayefurahia kashfa za mkewe gazetini, hainiletei picha nzuri kwenye familia, tena yenye maadili ya kidini kama yangu. Siwezi kushindana na Mike kama mke wangu haoni tatizo.“Mimi mwenyewe ni mtoto wa mjini sana, lakini sioni sababu ya kulumbana au kumfanyia kitu Mike, kwa nini nifanye hivyo kama Davina haoni tatizo?” alihoji.
Kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mume huyo alisema endapo Davina ataendelea na maisha aliyojichagulia, atalazimika kuoa mwanamke mwingine.Davina alipotafutwa alisema: “Kiukweli mimi bado nampenda mume wangu ila kama anaamua hivyo, sawa.”

AUNT ASEMA BILA CHETI CHA NDOA, SIMUACHI MOSE IYOBO

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ambaye hivi karibuni alipata mtoto aitwaye ‘Cookie’ amesema kama kuna mwanamke ambaye ana cheti cha ndoa na Moses Iyobo ajitokeze la sivyo hawezi kumuacha.
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Aunt alisema alipokuwa mjamzito amekuwa akipewa vitisho vingi ikiwa ni pamoja na mwanamke kudai ameporwa mumewe huyo.
“Kuna watu wanapenda sana kuongea, sasa mimi nasema kama kuna mtu ambaye ana cheti cha ndoa aliyofunga na Iyobo aje tu kisha mimi nitamuachia, la sivyo siwezi kumuacha,” alisema Aunt.

REMBO AMWIBIA SIMU BOB JUNIOR UKUMBINI

Musa Mateja
Msichana mmoja mrembo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja hivi karibuni alifanya kitendo cha aibu baada ya kunaswa akimchomolea simu Mwanamuziki Raheem Rumy Nanji ‘Bob Junior’.Tukio hilo la kushangaza lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bills Posta jijini Dar, ambapo Bob Junior alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wakipafomu.
Mrembo huyo akimpiga simu Mwanamuziki Raheem Rumy Nanji ‘Bob Junior’.
Awali, paparazi wetu alimuona mrembo huyo akipanda jukwaani na kuonekana kama aliyekuwa na lake jambo lakini alipofeli alishuka. Mara ya pili demu huyo alipanda tena, safari hii alifanikiwa kumkumbatia msanii huyo lakini katika hali ya kushangaza alionekana akihangaika kuzama mfukoni mwa Bob Junior na kuichomoa simu kiulainiii.
Tukio hilo liliwafanya watu waliokuwa wakimkodolea macho kupiga kelele za; Unaibiwa simuuu…unaibiwa simuuu…, kitendo kilichomfanya msichana huyo kuirudisha mfukoni simu hiyo fasta kisha kushuka.
Haikuweza kufahamika mara moja kama alikuwa akitania au alidhamiria kuiba kilongalonga hicho
 Baada ya tukio hilo mwandishi wetu alijaribu kuongea na Bob Junior ambapo alisema. “Mimi awali sikujua kama naibiwa lakini yale makelele ndiyo nikashituka, yaani yule demu bwana angeondoka na ile simu ingekuwa balaa.”

DIAMOND ABANWA KUMSALITI MEMBE NA KUUNGANA NA LOWASSA

Nimwendo wa kutangaza nia kwa baadhi ya wanasiasa ambao wanaomba ridhaa ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu ambapo upepo huo umemgusa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kwenda kufanya shoo wakati Waziri Mkuu Mjiuzulu, Edward Lowassa akitangaza nia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Benardi Memba akiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
TUHUMA ZA USALITI
Mara baada ya Diamond kuangusha bonge la shoo kwenye ‘iventi’ hiyo ya kuanza Safari ya Matumaini ya Lowassa akiungana na wasanii wengine kama Tunda Man, Khadija Kopa, Makomandoo, Nay wa Mitego, Dully Sykes na wengine kibao ndipo madai mazito yakaibuka kuwa amemsaliti mtangaza nia mwingine, Bernard Membe.
TEAM MEMBE MZIGONI
Mara baada ya ishu hiyo, kundi la siri linalojiita Team Membe kwenye Mitandao ya Kijamii ya Instagram, Twitter, Facebook na WhatsApp linalodaiwa kumuunga mkono waziri huyo wa Mambo ya Nje ya Nchi, Memba walianza kutoa vitisho kwa Diamond kuwa watamshikisha adabu kwa kuisaliti kambi yao.“Hakuna asiyejua kama Diamond alikuwa ni Team Membe. Kitendo cha kwenda kumsapoti Lowassa ni usaliti.
ETI WAMETOKA MBALI?
“Sisi (Team Membe) tunajua vitu vingi. Tunajua ukaribu wa Membe kwa Diamond na namna ambavyo amekuwa akimpa sapoti. Ukweli tumeshtushwa kumuona jamaa kwa Lowassa,” ilisomeka sehemu ya maoni ya mmoja wa memba wa Team Membe na kuungwa na mwingine:
Diamond akiongozana na waziri Membe.
“Hata kipindi kile (mwaka jana), Membe alimpa shavu la shoo Mtwara na Lindi na zaidi sana akamkaribisha hotelini wakala chakula pamoja kwa lengo la kujipanga namna ya kusapotiana.“Kuna madai kwamba walikubaliana kwamba Membe atamsaidia kwenye kuupaisha muziki wake kimataifa naye akamuahidi kumsapoti kwenye siasa hasa atakapotangaza nia kwa sababu Diamond ana ushawishi mkubwa ndani na nje ya Bongo.”
WANAMTISHAJE?
Kwa mujibu wa taarifa hizo za mitandaoni, vitisho hivyo vimekuwa vikifanywa kwa maneno tu katika kurasa za Diamond lakini siyo uso kwa uso kwani bado kundi hilo ni la siri.
DIAMOND ANASEMAJE JUU YA SAKATA HILI?
Baada ya kujikusanyia data hizo ambazo ndizo habari ya mjini kwa sasa hasa ikizingatiwa Membe naye atatangaza nia ya kutaka kuwania urais kesho Jumamosi, gazeti hili lilimtafuta Diamond ambapo alitoa waraka mzito:
“Kwanza kabisa watu wanatakiwa kufahamu kwamba mimi sina chama na wala siko upande wowote.
“Yeyote atakayechaguliwa na kuonekana bora kwa wananchi basi mimi kwangu ni sawa maana sina ufahamu mzuri wa siasa kujua yupi anafaa kuliko mwenzake.Lowasa akihutubia kwenye safari ya matumaini.
“Ila wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa mimi ni mwanamuziki na kazi yangu ni kuburudisha…hivyo yeyote atakayeniita kwenye hafla yake niburudishe na akafikia matakwa ya malipo yangu basi siwezi kuacha kwenda.“Hivyo nawataarifu wagombea na viongozi wote…mimi ni mwanamuziki wa Tanzania na nipo kwa ajili ya kuwatumikia kiburudani Watanzania wote…. Yeyote atakayetaka nimpatie burudani basi awasiliane na uongozi wangu.”
VIPI KUHUSU VITISHO?
Alipoulizwa juu ya vitisho kutoka kwa kundi lolote, Diamond alisema hajavipata lakini endapo atapata itabidi akaripoti polisi kwa usalama wake.
TUJIKUMBUSHE
Mapema mwaka jana Diamond alialikwa na Membe kwenye shoo za kuhamasisha amani huko Mtwara na Lindi ambapo baada ya shoo alipata fursa ya kula chakula pamoja na mheshimiwa huyo. Huo ndiyo ukawa msingi kwamba staa huyo yupo upande wa Membe.Diamond akitumbuiza.
Hata hivyo, katika maelezo yake, Diamond alikiri kufanya mazungumzo na Membe. Mazungumzo ambayo alidai yalihusu pongezi jinsi anavyojituma na kuitangaza Tanzania.Alisema pia waziri huyo alimuahidi kumpa sapoti kwa kumtafutia shoo nyingi za nje ya nchi huku Diamond yeye akiishia kuisihi serikali kuweka nguvu kwenye Muziki wa Bongo Fleva unaoajiri kundi kubwa la watu.
TUKIRUDI KWA WATANGAZA NIA
Mbali na Lowassa na Membe, wengine ambao wametangaza nia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni pamoja na Steven Wasira, Mwigulu Nchemba, Profesa Mark Mwandosya, Luhanga Mpina, Profesa Mark Mwandosya, Fredrick Sumaye na wengine kibao.

WEMA ANASWA LIVE KITANDANI AKIWA NA BWANA WA LINAH

Ubuyu! Staa wa Bongo Fleva almaarufu Ndege Mnana, Esterlina Sanga ‘Linah’, amedai kunasa ‘live’ tukio la mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu akiwa kitandani na aliyewahi kuwa bwana’ke (Linah), Nangari Kombo ambaye alipata umaarufu mwaka 2010 alipoingia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kumkumbatia Mchezaji wa Brazil, Ricardo Kaka kwenye mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Taifa Stars.
Staa mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu akiwa na aliyewahi kuwa bwana’ke (Linah), Nangari Kombo kitandani.
KUMBE PIA ALIKUWA MENEJA
Habari za kidaku zilidai kwamba, jamaa huyo ambaye amedumu na Linah kwa takriban miaka minne, pia ndiye alikuwa meneja wa msanii huyo ambaye alimsaidia mchakato wa kutengeneza video ya wimbo wake wa Ole Temba iliyofanyika nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’.
Estelina Sanga ‘Linah’ katika pozi la kimahaba na mpenzi wake Nagari Kombo.
Ilifahamika kuwa Wema ambaye hivi karibuni alidai kufunga ndoa ‘hewa’ amekutwa na skendo hiyo ikiwa ni siku kadhaa tangu alipoonekana ‘veri klozi’ na yule staa wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, raia wa Namibia, Luis Manana kwenye Shoo ya Instagram Party iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.
HAKUNA ALIYEJUA
Kama hiyo haitoshi, ilifahamika pia kwenye pati hiyo, pia Wema baadaye alionekana na Kombo lakini hakuna aliyejua kinachoendelea kwa kuwa alimtambulisha jamaa huyo wa Namibia kuwa ndiye mpenzi wake kwa sasa.
LINAH ACHARUKA
Ilidaiwa kwamba, baada ya Linah kuhakikishiwa kuwa Wema anatembea na Kombo alicharuka akitaka Wema amwachie mchumba’ke lakini alipoona maji yamefika shingoni aliamua kumwagana naye huku bado akimpenda.
“Unajua hii ishu siyo ya sasa hivi, ilianza kitambo sana, mwanzoni Linah alicharuka sana lakini alipoona yamemshinda akaachana na Kombo wakati bado alikuwa akimpenda sana,” kilisema chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Linah.
TEAM WEMA
Ilisemekana kwamba, baadhi ya wafuasi wa Wema wanaojiita Team Wema ambao wanaijua ishu vizuri wamekuwa wakijibu mapigo kwa Linah huku wakimmwagia matusi ya nguoni kuwa huenda alishindwa ‘mambo f’lani’ ya chumbani ndiyo maana Kombo akahamia kwa Madam ambaye ‘eti ni mkali wa hizo kazi’.
Wema na  Nangari wakifuatilia jambo.
LINAH ANASA PICHA ZA TUKIO
Habari za mjini ziliendelea kudai kwamba, katika kupata ushahidi, Linah alifanikiwa kunasa picha za Wema na Kombo wakiwa kitandani zilizomuonesha Wema akiwa na taulo pekee huku jamaa akiwa na ‘singilendi’ na boksa huku akionekana kutokwa na kijasho chembamba kwenye mashuka meupe hivyo kuwa na uhakika kuwa kuna kitu kinaendelea.
JE, NI PROJECT?
Tofauti na baadhi ya mastaa wengine ambao wamekuwa wakinaswa kimapenzi wakasingizia project ya kisanaa, ilidaiwa kwamba kwa Linah haamini hilo kwani hakukuwa na uhusiano wowote wa kisanaa kati ya Wema na Kombo.
HUYU HAPA NDEGE MNANA
Akizungumza na Risasi Jumamosi, juzi (Alhamisi) katika mahojiano maalum jijini Dar, juu ya ishu hiyo, Linah alisema kuwa alijua muda mrefu kwamba Wema anatembea na mpenzi wake huyo ambaye walikuwa wamefikia hatua ya uchumba.
“Kusema kweli nimeshaachana na Nangari (Kombo) na ninafahamu wazi kuwa anatoka na Wema Sepetu kwa sasa maana kuna picha kibao nimekuwa nikitumiwa zikionyesha wapo pamoja.“Mwenyewe kuna mahali nimekuwa nikiwakuta wako pamoja, jambo ambalo kwa sasa haliniumizi kichwa maana tumeshaachana na kila mtu ana mambo yake ila ninachoona kwa mwenzangu ameamua kuwa na Wema kama kuniumiza kichwa wakati kwa sasa naona ni kawaida tu.
“Kuna muda inafikia anakuwa kama anawatuma waje kuniambia maana kitu ambacho hata hakiniumi ila Wema naye namuona mtu wa ajabu sana kama yeye aliumizwa na ishu ya Kajala (Masanja) kumchukua CK wakati tayari alikuwa ameshaachana naye sasa kwangu mbona yeye kafanya hivyo.Staa wa Bongo Fleva almaarufu Ndege Mnana, Esterlina Sanga ‘Linah’ akiwa na aliyewahi kuwa bwanake Nangari Kombo.
“Ujue ingekuwa rahisi kwake kutoka na Nangari (Kombo) halafu mimi nisimuone wa ajabu kama angekuwa hajawahi kuniona naye lakini kwa sasa naye ameamua kufanya hivyo wakati anajua nilikuwa naye na mara kadhaa tulikuwa tukikutana tukiwa pamoja.
“Hata hivyo, nawatakia mapenzi mema kwa kuwa sina mpango na Nangari  (Kombo) tena ila ajue anachofanya naye ni ulimbukeni tu maana hata kama angeweza kuwa na Wema na asijioneshe kama hivyo kwa kuwa mimi siumizwi.
“Ila namshangaa Wema kumchukua mtu ambaye anajua alikuwa mtu wa rafiki yake ndiyo tatizo kwa kuwa yeye pia alishawahi kuwalaumu watu kwa ishu hiyo hadi leo hawazungumzi,” alifunguka Linah kwa uchungu kuonesha kukasirishwa na kitendo hicho.
WEMA VIPI?
Baada ya kuchukua maelezo ya Linah kinagaubaga, gazeti hili lilimsaka Wema kwa kila njia hadi kumfuata nyumbani juzi lakini liliambiwa kuwa amelala mchana wote na kila alipopigiwa simu haikuwa hewani hivyo jitihada za kusikia upande wake zinaendelea.
TUJIKUMBUSHE
Miezi kadhaa iliyopita, Linah na Kombo walitibuana na kutangaza kuvunja uchumba wao kwa kile kilichodaiwa kwamba kulikuwa na kundi la watu lililokuwa likiwachonganisha hivyo kila mmoja akachukua hamsini zake.

LINAH AMWANIKA MWANAUME WAKE


BAADA ya minong’ono ya muda mrefu, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ ameweka wazi kuwa anatoka kimapenzi na Nagari Kombo.
Linah akipozi na Kombo.
Linah alisema: “Ni kweli kwa sasa natoka na Kombo, ndiye mwanaume wangu, sina haja ya kuficha. Mimi na Amini imebaki stori tu, hata yeye ana mtu wake.”

HUU NDIO NGO WA MCHAWI ULIOZUA KIZAAZAA!

Dustan Shekidele, Morogoro
NI mshangao! Katika hali isiyotarajiwa, ungo wenye vifaa vya kichawi umekutwa jirani na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mazimbu, Dayosisi ya Morogoro na kuzua kizaazaa kikubwa.
Ungo wenye vifaa vya kichawi ukiwa jirani na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mazimbu, Dayosisi ya Morogoro.
Tukio hilo la aina yake lilijiri saa 12  asubuhi, Jumatano iliyopita katika  eneo hilo lililopo Mtaa wa Boma ‘A’ Kata ya Mazimbu mkoani hapa.
Vitu vilivyokutwa kwenye ungo huo ni damu, pembe, nyembe, shanga, kipande cha gazeti, vitambaa vyeusi na vyekundu.
Baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na eneo la tukio walimshutumu mkazi mwenzao (jina tunalo) kwamba, ungo huo ulitoka ndani ya nyumba yake.
Kufuatia kuzipa nguvu shutuma hizo, wananchi hao waliizingira nyumba hiyo ya kifahari iliyopo jirani kabisa na Kanisa la KKKT na kusema maneno ya waziwazi kuhusu imani yao. lli kupata ukweli wa madai ya wananchi hao, mwandishi wetu aliingia ndani ya nyumba hiyo kwa lengo la kuzungumza na mmiliki wake huyo ambaye alisema:
Wananchi wakiangalia Ungo wenye vifaa vya kichawi.
“Usiku, kama saa 7 hivi, mbwa wangu walipiga kelele sana. Tulipotoka tukakuta huu ungo ila mwenye ungo hatukumuona. Huenda aligonga kwenye nyumba yangu, akaruka ukuta na kukimbia. Kulipokucha ndiyo tukaamua kuutupa nje.”
Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa vikali na wananchi hao wakidai mchawi mwenye ungo huo alitoka ndani ya nyumba hiyo.
“Kama ni kweli kwa nini mbwa wake wasimng’ang’anie huyo mwanga? Pia tunajua hii nyumba ina mlinzi kwa nini hakumkamata?” alihoji jirani mmoja.
Jirani mmoja yeye alikwenda mbele zaidi kwa kusema:
“Nakumbuka majira ya saa 12 asubuhi kuna mwenzetu mmoja kamuona mtu akitoka ndani ya nyumba hii na ungo na kuutupa kwenye eneo hili la kanisa kisha akarudi ndani fasta.“Tulipokuja kuangalia ndani ya ungo tukakuta damu, pembe, nyembe, vitambaa vyeusi na vyekundu. Majirani tukaamua kukusanyana na kuja kwenye nyumba hii. Tumekuta geti liko wazi huku milango ya nyumba kubwa ikiwa imefungwa kwa ndani.”
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Kilewa Bohari alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Ilikuwa kazi kubwa, wananchi waliivamia nyumba ya yule bwana wakidai mwanga yuko ndani. Mimi na baadhi ya wajumbe wangu na wananchi tuliingia kwenye ile nyumba na kusachi.
“Kiukweli hatukumwona mwanga na mwenye nyumba anakiri kuna mwanga alianguka usiku kwenye nyumba yake,” alisema mwenyekiti huyo.Licha ya mwenyekiti huyo kuwasihi wananchi hao kuondoka eneo hilo waligoma wakisisitiza mwanga alikuwemo ndani ya nyumba hiyo.
Kufuatia kizaazaa hicho, uongozi wa mtaa huo uliamua kuita polisi ambao walifika na kuuchoma moto ungo huo na kuwatawanya wananchi.

WASTARA ASEMA ALIYENIONJA’ AJITOKEZE MAANA AMECHOKA KUSINGIZIWA

VUNJA ukimya! Baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu na fununu za kutembea na wanaume kadhaa tangu kufariki kwa aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma hatimaye amefunguka na kujiapiza kwa kulamba kidole, kuchovya mchanga na kukipitisha shingoni akidai tangu kuondoka kwa Sajuki hajawahi ‘kuchangia shuka’ na mwanaume yeyote na kama yupo, ajitokeze hadharani!
Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma.
‘Akibadilishana sentensi’ na ‘kiruka’ njia wetu kwa njia ya simu hivi karibuni, Wastara ambaye bado anafanya vyema kwenye sanaa, alishutumu na kuonekana kuchukizwa vikali na tetesi juu yake akihusishwa na wanaume kadhaa akiwemo msanii mwenzake, Bond Bin  Suleiman.
“Nashangazwa sana na wanaoeneza uvumi wa mimi kutembea na wanaume wengi baada ya kifo cha mume wangu, kwani mimi sina haki kama mwanamke jamani? Kama kuna mwanaume mwenye uthibitisho wa kutembea na mimi si ajitokeze!” alisema Wastara huku akiashiria jazba.

MWANAMKE MMOJA AKATWA MAPANGA KWA MADAI YA KUGONGANISHA WANAUME

MCHEPUKO usitajwe kwako! Mrembo aliyejulikana kwa jina la Bahati Nyamkira (20) (pichani), mkazi wa Kijiji cha Singu, Kata ya Kukirango, Butiama, Mara, amenusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na mwanaume anayedaiwa kuwa hawara yake kisa kikisemekana ni kumkuta akiwa na hawara mwingine, (kuwagonganisha).
Bahati Nyamkira amenusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea saa 4 usiku wa Mei 23, mwaka huu nyumbani kwa mwanamke huyo katika kijiji hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda, siku ya tukio, saa 2 usiku, kijana mmoja aitwaye Nyamkinda James (23), mkazi wa Kijiji cha Buturu ambaye anadaiwa aliwahi kuishi na mwanamke huyo na kuzaa naye mtoto mmoja, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo kwa lengo la kumchukua ili aende kulala naye kwao lakini mwanamke aligoma na kumfanya mwanaume huyo kutia shaka kwamba, huenda ana mwanaume mwingine.
Ilizidi kudaiwa kuwa, mara baada ya mwanamke huyo kugoma, kijana huyo aliondoka kimyakimya hadi nyumbani kwao na kuchukua panga kisha akarudi kwa kunyatia na kujificha sehemu.“Yule kijana akiwa amejificha huku macho yakiwa kwenye nyumba ya mwanamke huyo, ghafla alimwona mwanaume mwingine akifika nyumbani hapo na kugonga mlango.
“Mwanamke alifungua mlango na kuondoka na mwanaume huyo. Ndipo Nyamkinda alitoka pale alipokuwa amebana na panga lake na kumvamia kisha kuanza kumcharanga hovyo mwanamke huyo na kumsababishia majeraha makubwa,” alisema shuhuda mmoja.
“Sisi tulisikia kelele kutoka nyumbani kwa Bahati, tulipofika tulimkuta anagaragara chini huku akitokwa na damu nyingi mwilini na akilia kwa uchungu.“Tulipomuuliza kulikoni alisema  amecharangwa mapanga na hawara yake wa zamani  baada ya kumwona akiondoka na mwanaume mwingine, hivyo tukampa msaada wa kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Butiama ambako amelazwa,” aliongeza shuhuda huyo.
Afisa mmoja wa polisi mjini Butiama ambaye ameomba jina lake lisitajwe kwa kuwa siyo msemaji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, mtuhumiwa huyo anasakwa baada ya kutokomea kusikojulikana.

VIFO VYA WATOTO WENGINE WAWILI VYATIKISA DAR BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI

NImajonzi tena! Simanzi kubwa ilitawala kwa wakazi wa Jiji la Dar hususan Ukonga Mazizini kufuatia familia ya Emanuel Chadaha kufiwa na watoto wao wawili, Boniface  (6) na Kelvin (4) katika tukio moja la kuzama kisimani.

Majeneza yaliyobeba miili ya watoto hao yakiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
Vifo hivyo ambavyo vimeacha historia ya kusikitisha, vilitokea Mei 23, mwaka huu tena kwa  mateso makubwa kwa vile wakati wanazama mmoja mmoja ndani ya kisima hicho hawakupata msaada wowote.Kwa mujibu wa waombolezaji kwenye msiba huo, watoto hao ambao walikuwa wakipendana sana, siku ya tukio walikuwa wakicheza nje ya nyumba yao huku baba yao mzazi, Emanuel akiwa ndani akizungumza na mgeni.
“Baba yao kwa vile aliona hali ya hewa nje si nzuri, mvuamvua ilikuwa ikinyesha, aliwaonya watoto wake wasichezee nje.
“Baba yao aliwazuia mara tatu lakini si unajua watoto tena, waliendelea kucheza nje.
“Nyumba wanayoishi, kwa pembeni kuna kisima ambacho hakijafunikwa juu na mbaya zaidi kilijaa maji, sasa kwa uelewa wa watoto hao waliamini  kisima hicho hakijajaa,” alisema mwombolezaji mmoja.Simulizi hii ya watoto, iliendelea kusema kuwa, baba wa watoto haoa alianza kuhisi utulivu uliopo nje si wa kawaida hivyo kudhani kwamba watoto wake walikwenda kucheza mbali.

Waombolezaji wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuaga miili ya watoto hao.
Alitoka nje kuwaangalia hakuwaona, akaenda kwa majirani ambako pia hawakuwepo. Alipokuwa akipita usawa wa kisima, alishtuka kuona kandambili moja ya Kelvin ikielea.“Kama mzazi mwenye uchungu tayari alishahisi mauti imemfika mtoto wake, akachukua uamuzi ya kuingia ndani ya kisima ambapo aliwakutana watoto wake wote wameishakunywa maji, alipoibuka akapiga kelele.
“Majirani tulijitokeza baada ya kuomba msaada, tukawatoa na kuwakimbiza Hospitali ya FFU Ukonga (Dar) lakini madaktari walisema walishafariki dunia hivyo miili ikapelekwa Hospitali ya Amana kwa ajili ya kuhifadhiwa.
“Inavyoonekana, aliyeanza kuzama ni mkubwa, mdogo wake alipoona kaka yake amezama na yeye akajitosa ili kumwokoa, kumbe naye anaitwa na mauti,” alisema jirani mmoja.

Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, watoto hao walikuwa wawili waliozaliwa tumbo moja, hivyo wazazi hao wamebaki watupu. Inauma sana!Mama mzazi wa watoto hao, Vailet Muhaha aliposikia  watoto wake wamefariki dunia alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitali kiasi cha kumfanya ashindwe kuaga miili ya watoto hao.
Watoto hao waliagwa Mei 27, mwaka  huu  katika Kanisa  la Angalikana, Ukonga  na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi yaliyofanyika siku iliyofuata.
Mungu azilaze pema peponi, roho za watoto hao. Amina.

MPENZI WA FACEBOOK ANAYEDAIWA KUMNYONGA MKE WA MTU GESTI DAR NI HUYU HAPA MWANGALIE

Charles Raphael anayedaiwa kumnyonga mke wa mtu gesti.
MTUHUMIWA WA MAUAJI
Taarifa kutoka chanzo makini zimeeleza kuwa, mwanaume huyo mpaka anafikwa na tukio hilo la kudaiwa kumuua mwanamke huyo kwa kumnyonga alikuwa akijihusisha na kazi ya ubaharia  kwa safari za ndani na nje ya nchi hasa Yemen ambapo alikuja nchini kuchukua vyeti vyake ili akaajiriwe rasmi nchini huko.
VYANZO VYA POLISI
Kwa mujibu wa vyanzo vya polisi katika maelezo ya mtuhumiwa huyo, inadaiwa siku ya tukio, wawili hao walikubaliana wakutane kwenye gesti hiyo na kufanya mapenzi.
“Walifanya mapenzi kweli tena bila kinga. Walipomaliza, mwanaume alipekua mkoba wa mwanamke, akakuta vidonge ambavyo yeye alivitafsiri kwamba ni vya kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi (ARV).
MZOZO WAIBUKA
“Mzozo ulianza kuibuka. Mwanaume alimjia juu mwanamke kwamba huenda amemwambukiza virusi vya Ukimwi ingawa mwanamke alijitetea kuwa vidonge vile siyo ARV. “Kwa hasira mwanaume akamshika shingoni na kumkaba, kisha akamwachia na yeye akaondoka,” kilisema chanzo.
Kikaongeza: “Wakati mwanaume anaondoka kwa hasira, mwanamke alikuwa ameanguka chini lakini alikuwa hajafariki dunia. “Ndipo nyuma, wahudumu wa gesti walibaini kuwa, ndani ya chumba hicho kuna mwili wa mwanamke ukiwa chini na kutoa taarifa polisi.”
MTUHUMIWA ALIKAMATWAJE?
Habari zaidi zinadai kuwa, baadhi ya wafanyakazi wenzake marehemu walijua wawili hao walikuwa pamoja kwa hiyo kifo cha mwenzao walikihusisha na mwanaume huyo.
“Ili kumpata mtuhumiwa, polisi walimtumia mfanyakazi mmoja wa marehemu ambaye aliwahi kutongozwa na mwanaume huyo siku za nyuma. Yeye alimpigia simu mwanaume na kumwambia yuko tayari kwa sasa kumpa penzi. Jamaa akafurahi, wakapanga kukutana maeneo ya Jeti, Dar ambapo mtuhumiwa huyo alipofika, polisi walimkamata.
Habari zinasema kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa huku akiwa hajui chochote, akiwa ndani ya gari la kukodi aina ya Toyota Carina (namba zinahifadhiwa) na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar (anakoshikiliwa hadi sasa).

NDANI YA KITUO CHA POLISI
“Alipofikishwa kituoni aliambiwa kuwa ameua mwanamke kwa kumnyonga, akashtuka sana. Akasimuliwa mkasa wote na yeye akajieleza,” kiliongeza chanzo.
POLISI WAVIFANYIA KAZI VIDONGE
Habari zaidi zinawekwa wazi kwamba, polisi walivichukua vidonge hivyo na kuvipeleka kwa wafamasia kwa ukaguzi kama kweli ni ARV lakini vikabainika ni vya minyoo.
MUME WA MAREHEMU
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, siku ya tukio mume wa marehemu, Suleiman Othman alimpigia mkewe simu ili kujua alipo akamwambia anatoka kazini lakini kutokana na foleni za barabarani atachelewa kufika nyumbani.
Taarifa zaidi zinadai kwamba mume alipoona usiku unazidi kuingia, mkewe hajarudi alimpigia simu  ambapo iliita bila kupokelewa baadaye ikawa haipatikani hewani.
TAHADHARI KWA WATUMIA FACEBOOK
Polisi mmoja aliyezungumza na Uwazi kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa vile siyo msemaji, alisema kumekuwa na kesi nyingi kwenye vituo vya polisi ambapo chanzo chake ni Facebook.“Mimi nawaambia watumiaji wa Facebook kujihadhari na mawasiliano na watu wasiowafahamu, hasa kwenye suala la uhusiano wa mapenzi,” alisema afande huyo.

TUJIKUMBUSHE
Katika gazeti hili toleo lililopita, tuliandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; MPENZI WA FACEBOOK AMNNYONGA MKE WA MTU GESTI!
Tukio hilo lilijiri Mei 19, mwaka huu kwenye nyumba ya kulala wageni (guest house) iliyopo maeneo ya Afrikasana, Dar pembezoni mwa barabara ya kwenda Kijitonyama kupitia Polisi Mabatini.
Katika habari hiyo, mume wa marehemu alisema haamini kama mkewe alishawishika kukutana na mwanaume huyo kwa ajili ya kufanya mapenzi tu bali alikuwa na nia ya kumwibia pesa za mauzo ya siku hiyo.Alisema mkewe alikuwa akifanya kazi ya kuuza mafriji kwenye duka moja lililopo maeneo ya Afrikasana, Dar.

THEA ABARIKI MUMEWE KUOA TENA BAADA YA KUACHANA NAYE

Msanii mkongwe wa filamu, Salome Urassa ‘Thea’.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Thea alisema katika akili yake hana kumbukumbu kama aliwahi kuolewa na mwanaume huyo (ukweli walifunga ndoa 2010) na hataki kumzungumzia ila kama anataka kuoa aoe kwani hana shida naye na hana malalamiko yoyote.
Baada ya kumsikiliza mwanamama huyo, paparazi wetu alimtafuta Mike ambaye alisema; “Kutokana na Thea kuongea maneno ya kashfa na kudai kwamba hanijui, niko kwenye mazungumzo na familia na mke wangu wa kwanza, Ummy Mohamed ambaye tuna mtoto mmoja hivyo kama mambo yakienda vizuri  nitamrudia kwani namuona ni bora zaidi.”

MUME AFUKUZWA UKWENI KWA KUSHINDWA KUTOA MATUMIZI KWA WAKWE

Katika sakata hilo, baba Juma inasemekana amekuwa akiishi ukweni hapo ambapo masuala ya msosi wanachangia kwa zamu na familia nzima kila mmoja na siku yake.Kwa mujibu wa chanzo chetu, zamu ya wanafamilia wengine ikifika hununua chakula chenye mvuto kinywani, kama samaki wa Mwanza (sangara, sato) na mapochopocho mengine lakini zamu ya Mwanahamisi, mumewe hutoa pesa ya matembele jambo linalodaiwa lilikuwa likiwakera wanafamilia hao.
Kufuatia kero hiyo, kwa mujibu wa chanzo, wanafamilia hao inadaiwa waliamua kumvalia njuga baba Juma na kumtimua yeye na mkewe na mtoto wao Juma mwenye miaka miwili.
Ni wakati mtafaruku huo wa ‘aondoke huyo’ ukiwa umepamba moto, chanzo chetu hicho kilipiga simu Ofisi za Global Publishers, Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kupasha mchezo kamili na   akusema kuwa timbwili hilo lilikuwa likiendelea ‘laivu’....Bila kuchelewa, mmoja wa makachero wa OFM kwa kutumia pikipiki iendayo kasi, ndani ya dakika chache alifika eneo la tukio na kukuta baadhi ya wanafamilia hao wakiendelea kuwafanyia timbwili Mwanahamisi na mumewe ikiwemo kuwapa vichapo huku wasamaria wema wachache wakijaribu kutuliza.
Bila kuchelewa, paparazi wetu alianza kuwafotoa picha wanafamilia hao huku Mwanahamisi akijaribu kuokoa maisha yake kwa kukimbia huku amembeba mwanaye.Mwanahamisi alisikika akisema hawezi kuhama nyumbani hapo kwa vile nyumba hiyo ni ya baba yake mzazi hivyo ni bora wamtenge kwenye misosi lakini si kumfukuza kabisa.
Utetezi wake ulipingwa vikali na wanafamilia hao hasa mama yao mdogo aliyefahamika kwa jina la mama Hashimu.
Baada ya varangati kuzidi, Mwanahamisi aliona ni heri ambebe mwanaye na kukimbia naye huku mumewe akimfuata kwa nyuma na kwenda kusikojulikana.
Mke wa baba Juma nae akitimuliwa pamoja na mwanaye.
Katika hali ya kushangaza, wanafamilia hao walimgeukia paparazi wetu na kutaka kumfanyia vurugu ikiwemo kujaribu kuvunja kamera yake lakini wakagonga mwamba.Katika sakata hilo, mwanadada mmoja aliyekuwa amesahau kuchana nywele, akiwa amejifunga kanga moja kifuani, nyingine kiunoni huku hana viatu, alimporomoshea matusi paparazi wetu ambayo aliyarekodi.
Kwa vile kisa kilisikika wakati wa mzozo, gazeti hili lilifanya jitihada za kuzungumza na wanafamilia hao ili kusikia kutoka kwao lakini ilishindikana baada ya kukosa ushirikiano kutokana na hasira za kupigwa picha.

WEMA AONESHA MAHABA NIUE LIVE NA MPENZI WAKE MPYA BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND

LIVE! The Big Boss wa Kampuni ya Endless Fame Productions, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amejikuta akionesha mahaba niue kwa ‘kujibebisha’ kwa Mshiriki wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Manana huku akimmwagia sifa nyingi na kudai ndiye laazizi wa moyo wake kwa sasa baada ya kuachana na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’.
The Big Boss wa Kampuni ya Endless Fame Productions, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa na Mshiriki wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Manana.
TUJIUNGE VIWANJA VYA POSTA
Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri ndani ya Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita kwenye Shoo ya Instagram Party ambapo Wema alikuwa mmoja wa washiriki wa tamasha hilo lililohudhuriwa na mamia ya mashabiki hivyo walipata mshtuko waliposikia habari hizo njema kutoka kwa Madam.
AMMWAGIA SIFA KEDEKEDE
Akiwa kwenye pati hiyo, Wema alipanda stejini kwa ajili ya kuongea na mashabiki wake na baadaye alipanda Luis ndipo Madam akaanza kummwagia sifa kedekede na kabla ya kumtambulisha rasmi kuwa ndiye ubavu wake.
Kwa kinywa chake bila kumung’unya maneno, Wema alidai kwamba Luis ndiye mwanaume ampendaye kwa sasa hasa akivua shati lake kwani ana vitu adimu ambavyo vinamfanya asimruhusu kuwa mbali naye.
LUIS NAYE
Baada ya sifa hizo, Luis naye alisema kuwa alipanda ndege kutoka Namibia hadi Dar kwa ajili ya kuja kujumuika na mwanamke ampendaye ambaye ni Wema.
Wema na Luis Manana wakifuatilia jambo.
TEAM WEMA FULL SHANGWE
Utambulisho huo ulizua shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki hasa Team Wema ambao kwa pamoja walionesha kusapoti uhusiano huo na hata baada ya kushuka walionekana kuwazonga huku wakipigana vikumbo kwa ajili ya kutaka kila mmoja kupiga nao picha. “Sisi Team Wema tumepitisha ile Team Haters (timu ya wenye chuki) wakale malimao kama alivyosema Gwajima (Askofu Josephat) kwamba kama kuna watu hawampendi Lowassa (Edward) basi wakale malimao,” alisikika mmoja wa Team Wema.
NI KWA MARA YA KWANZA BAADA YA DIAMOND
Usiku huo ulikuwa wa kwanza kwa mwaka huu kumuona Wema akimtambulisha mwanaume kwa mara ya kwanza kwenye tamasha kubwa kama hilo tangu alipoachana na Diamond ambaye kwa sasa anajivinjari na mwanamama Zarinah Hassani ‘Zari The Boss Lady’.Kuna madai kwamba baada ya wawili hao kuwa beneti tangu waliposhuka jukwaani walikwenda kulala hoteli moja kwa mujibu wa wafuatiliaji.
WALILALA WOTE HOTELINI
Chanzo chetu cha habari kilichokuwa ndani ya hoteli hiyo (jina linahifadhiwa) kilidai kwamba siku hiyo Wema na Luis waliingia hotelini hapo na kulala hadi kesho yake, jambo ambalo lilikuwa siyo kificho tena hasa kwa wahudumu na watu wote walioongozana na msafara wa wawili hao. “Kweli kabisa Luis anatoka kimapenzi na dada yetu Wema maana nimeshuhudia tangu jana, Wema alikuja hotelini na baadaye wakaondoka wote.
...Wakikumbatiana kimahaba.
“Hata usiku wakati wanatoka Viwanja vya Posta pale Kitonyama walirudi na kulala pamoja, achilia mbali hiyo, Wema na Luis ni watu ambao wanaonekana kuwa katika mapenzi kwa muda sema tu Luis alikuwa hajapata nafasi ya kuja Dar,” kilisema chanzo hicho.
KUMBE LUIS ANAJUA KISWAHILI!
Baada ya kujiridhisha na uwepo wa uhusiano wa wawili hao, mwanahabari wetu alifuatilia kwa makini baadhi ya akaunti zinazotumiwa na Luis kwenye mitandao ya kijamii ambapo aligundua kuwa jamaa huyo amekuwa akimuweka Wema kwenye peji zake huku akimmwagia sifa na maneno ya kimahaba tena kwa Lugha ya Kiswahili.

Baadhi ya maneno aliyokuwa ameandika Luis katika peji yake ya Instagram akiambatanisha na picha zao yalisomeka: “Najaribu kumtuliza... Mtoto mzuri.“Huyu msichana anaweka tabasamu usoni mwangu.”

HII SASA NI MWISHO WA DUNIA WANAFUNZI DAR WAFANYA MAPENZI NA MBWA

NI kweli kabisa dunia imekwisha! Kanisa la Maombezi la Ebenezer Deliverance la Mbezi ya Salasala jijini Dar lililo chini ya Mchungaji Benson Shirima limegeuzwa danguro la kufanyia ‘usodoma’ kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Benaco waliotoroka majumbani mwao na kukacha masomo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Benaco waliotoroka majumbani mwao na kukacha masomo wakiwa ndani ya Kanisa la Maombezi la Ebenezer Deliverance la Mbezi ya Salasala jijini Dar.
WAZAZI, WASAMARIA WEMA
Kufuatia kushamiri kwa vitendo hivyo kwenye kanisa hilo, wazazi wa wanafunzi hao na wasamaria wema walikwenda kutoa taarifa kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa Kilimahewa, Kata ya Wazo, Mbezi Salasala na kuweka bayana kila kitu.
Wanafunzi hao wakiwa katika katika pozi baada ya kunaswa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.
KISA CHA KUTOA TAARIFA
Awali ilidaiwa kuwa, baadhi ya wanafunzi kwenye eneo hilo walikuwa wakisakwa na wazazi wao kwani waliondoka majumbani wiki kadhaa kwenda shuleni lakini hawakurudi na shuleni hawakuwepo.
“Hata walimu walisema wanafunzi hao hawafiki shuleni na majumbani hawapo. Ndiyo tuliposikia kuna kanisa limefanywa geto tukaamua kwenda serikalini kutoa taarifa ili uongozi wa serikali ujipange tukavamie,” alisema mtu mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Godoro ambalo watoto hao walikua wakilitumia.
UAMUZI WA SERIKALI YA MTAA
Maelezo ni kwamba, baada ya taarifa hiyo kufikishwa ofisini hapo, wajumbe wa ofisi hiyo na vijana wa ulinzi shirikishi wakiongozwa na mwenyekiti wa ofisi hiyo, Kulthum Juma walikwenda kulivamia geto hilo kwa lengo la kulisambaratisha.
Wanafunzi wakiwa na mbwa hao.
OFM WAPASHWA
Wakati safari hiyo ikiandaliwa, mmoja wa wanyetishaji wetu alipiga simu kwenye Ofisi za Global Publishers,  kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, Bamaga- Mwenge, Dar na kuweka bayana kila kitu ambapo bila kuchelewa mmoja wa makachero wa OFM alitumia usafiri wa pikipiki iendayo kasi na baada ya dakika chache alikuwa ameshafika Salasala.
Wazazi na ulinzi shirikishi wakiwa katika geto baada ya kuwanasa wanafunzi wanaodaiwa kufanya ngono na mbwa.
Wasamaria wema wakikagua eneo hilo ambalo watoto hao walilkuwa wanalitumia kwa ajili yavitendo viovu.
KILICHOKUTWA GETO
Kama wewe ni mzazi lazima ushtuke! OFM, wazazi na ulinzi shirikishi walilivamia geto na kuwanasa wanafunzi wakifanya ngono na mbwa lakini baadhi yao walifanikiwa kuchoropoka kupitia juu ya paa huku wengine watano walikamatwa.
WALIOKAMATWA!
Miongoni mwa wanafunzi waliokamatwa ni; (kwa jina moja kwa sababu maalum,) David, Goodluck, Joseph, Mrisho na aliyetajwa kuwa kiongozi wao, Juma aliyefaulu darasa la saba na kuteuliwa kwenda katika Shule ya Sekondari ya Twiga, Dar lakini akakataa kuendelea na masomo! Inauma sana!
MAAJABU YA MBWA
Katika hali isiyotarajiwa katika akili za kibinadamu, wakiwemo wazazi wa watoto hao, mbwa waliokutwa kwenye danguro hilo, kwa kuzoea kuingiliwa na binadamu, hata msafara huo ulipovamia wao (mbwa) waliendelea kuwasogelea kimahaba wanafunzi hao.
Mbwa hao walionesha hisia zao hadharani jambo lililomfanya, Edresi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi David kuangua kilio kama mzazi mwenye uchungu.
WAELEZA WALIVYOKUWA WAKIISHI
Baada ya kibano kizito, wanafunzi hao walianza kueleza jinsi walivyokuwa wakiwaingilia kimaumbile mbwa hao na jinsi walivyokuwa wakipata chakula kwa kuiba kuku, mahindi, pesa na vitu vingine mitaani.
WAMTAJA  DADA ANAYEWAPIKIA
Wanafunzi hao, walimtaja msichana mmoja aliyefahamika kwa jina la Salome ambaye ndiye mpishi wao kwenye danguro hilo.
MSAFARA KWA MPISHI
Baada ya kumtaja msichana huyo, msafara huo ulitia timu nyumbani kwa Salome ambaye baada ya kubanwa alisema alishawahi kuwapikia mara moja.
MCHUNGAJI WA KANISA HILO ANENA
Kwa kutumia namba za simu zilizokutwa kwenye vipeperushi vya matangazo ya mikutano ya hadhara ya Neno la Mungu ya kansia hilo na kwenye bango la utambulisho wa jina la kanisa, kando ya barabara, paparazi wetu alifanikiwa kuzungumza na Mchungaji Benson ambaye alikiri kulimiliki kanisa hilo.
“Ndugu mwandishi ni kweli mimi ndiye mchungaji wa kanisa hilo lakini kwa sasa niko mbali na huko lakini nimeshapigiwa simu hivyo nitakuja kuweka mambo sawa.
“Kama hao wanafunzi wanaishi humo watakuwa wamevunja na kuingia wenyewe. Vipi, kitanda na vile vyuma vya jukwaa na vitu vingine umevikuta?” mchungaji alimuuliza paparazi wetu.
“Vipo baba mchungaji, nimeviona,” alijibu paparazi wa OFM.
 MWENYEKITI WA MTAA
Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa mtaa huo aliyeongoza msafara huo aliwaomba wazazi wenye watoto hao kupima afya zao kwani ilidaiwa kuwa walikuwa wakiingiliana hata wenyewe kwa wenyewe na kuna uwezekano mkubwa wa kupata maradhi ya ngono ambayo hupatikana zaidi kwa mbwa na binadamu. 

HUYU NDIO MPENZI MPYA WA DIAMOND! VIPI ZARI? ATACHWA?

Madai mazito! Mshiriki wa Kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2011/12 ambaye alianza harakati za kunyakua taji hilo akitokea Mkoa wa Shinyanga na baadaye kutwaa Taji la Miss Kanda ya Ziwa, Glory Samwel anadaiwa kumchokonoa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile kinachodaiwa kuwa ana ukaribu wa ‘kimalovee’ na mpenzi wa Zari, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa katika pozi na miss huyo.
Chanzo cha ‘unyunyuzi’ huo kilitonya kwamba, mlimbwende huyo amekuwa akionekana mara kwa mara akijivinjari na Diamond jambo ambalo wadau wamelishtukia na kubaini kuwa ana mpango wa kuingilia penzi la Zari na kusambaratishia uchumba wa wawili hao.
Ijumaa Wikienda lilinyetishiwa habari hizo hivi karibuni na kuamua kuzifanyia kazi hatua kwa hatua, ambapo liliweza kujiridhisha kwa baadhi ya matukio ya picha ambazo mrembo huyo amekuwa akipiga na Diamond.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Mbali na picha pia kuna matukio ya sherehe za ‘bethidei’ ambazo Diamond alionekana akiwa karibu na mrembo huyo.
Ukiachilia mbali uchunguzi huo, mwanahabari wetu alimtafuta mrembo huyo kwa lengo la kutaka kujiridhisha juu ya madai hayo ambapo alikiri kuwa na ukaribu na Diamond huku akifafanua kwamba uhusiano wake na jamaa huyo si wa kimapenzi kama wengi wanavyomchukulia.
“Hizo picha za karibu zaidi ni zile ambazo tulipiga kwenye bethidei ya meneja wa Diamond aitwaye Salaam, ambayo ilifanyika pale nyumbani kwake (Salaam) Kijitonyama (Dar) hivi karibuni.
“Ni kweli watu wengi wananituhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond lakini si kweli maana ninajuana naye kawaida tu,” alisema Glory.
Kwa upande wa Diamond aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa ni kweli anamfahamu Glory ila si mpenzi wake na anachokijua ni shabiki wake kama ilivyo kwa wengine.
Alisema hata picha alizopiga naye hakuna picha za hovyo maana zilipigwa hadharani.

“Glory ni shabiki wangu wa kawaida tu kama ilivyo kwa mashabiki wangu wengine, suala la kupiga naye picha halimaanishi ni demu wangu,” alisema Diamond.

KALIO LA MASOGANGE LALETA AJALI MBAYA SOMA HAPA UONE

Makubwa! Lile kalio la haja la muuza nyago maarufu kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange’ limesababisha ajali kati ya bodaboda na Bajaj maeneo ya Sinza-Mori baada ya mrembo huyo kushuka kwenye gari akielekea saluni.

Agness Gerald ‘Masogange’ akiwa katika pozi.
Shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa bodaboda ilikuwa ikitokea upande wa Baa ya Meeda na Bajaj ilikuwa ikitokea upande mwingine ambapo muendesha bodaboda alitumia muda mwingi akimtazama Masogange aliyekuwa akikatiza huku akilitingisha wowowo ndipo jamaa huyo akasababisha ajali.
Agness Gerald ‘Masogange’ akionyesha jinsi alivyoumbika.
“Yaani aliposhuka Masogange tu kwenye gari yule mwendesha bodaboda hakuwa anaangalia mbele kabisa wakati Bajaj ilikuwa ikija kwa kasi hivyo akashindwa kuikwepa akaivaa na kumrusha dereva wa bodaboda upande mwingine kwa kishindo,” alisema shuhuda.
Mpashaji wetu alizidi kuweka wazi kuwa baada ya ajali hiyo kutokea, watu walikusanyika kitendo ambacho hata Masogange kilimshtua na kumfanya asimame kuangali tukio hilo.
Hata hivyo, shuhuda huyo alisema madereva hao walielewana na kuyamaliza palepale.
Baada ya gazeti hili kupata ‘ubuyu’ huo, lilimtafuta Masogange ambapo alikiri kutokea kwa ajali hiyo lakini mwanzo hakujua kama yeye alikuwa chanzo cha ajali hiyo.
“Unajua mimi nilivyosikia kishindo na watu wakipiga makelele sikujua kama  nilikuwa chanzo hadi niliposikia watu wanaanza kunong’ona maana hata mimi nilikuwa nashangaa na kujikuta nikicheka tu kwani sikujua wowowo langu lilisababisha shida,” alisema.ge.

WAUMINI WASEMA MAPADRI WARUHUSIWE KUOA

Mpasuko! Kufuatia kuibuka wimbi la kashfa za ngono zinazowagusa waseja wa daraja la upadri duniani, baadhi ya waumini wa madhehebu mbalimbali yakiwemo Katoliki na Anglikana, wameibuka na kudai kuwepo kwa marekebisho ya sheria ya makanisa hayo yanayoruhusu watumishi hao kuoa kwani kwa sasa wanayaaibisha, jambo ambalo linaharibu imani juu ya Ukristo.
Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
NINI KIMETOKEA?
Hayo yanakuja kufuatia tukio la hivi karibuni la kunaswa kwa Padri Anatoly Salawa ambaye ana cheo cha Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, Tec) aliyekutwa na mrembo vichakani.
Father Salawa alinaswa na mrembo huyo vichakani ndani ya gari maeneo ya Kurasini jijini Dar.
Mbali na tukio hilo, pia yapo matukio mengine ya mafumanizi likiwemo lile la Father Urbanus Ngowi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi aliyefumaniwa ‘laivu’ na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la mama P.
Katika tukio hilo la mwaka 2013 lililoripotiwa na gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda, Father Ngowi alikutwa na mwanamke huyo ambaye alikuwa muumini wake, chumbani kwake maeneo ya Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini.
Padri Anatoly Salawa aliyenaswa na binti kichakani.
WAUMINI WAFUNGUKA
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, mwanzoni mwa wiki hii, waumini hao walitolea mifano ya baadhi ya viongozi wa madhehebu hayo kunaswa katika skendo za uhusiano wa kimapenziu hivyo kuona ni bora wakaruhusiwa kuoa ili kuliondolea aibu kanisa.
“Ni bora kama ni sheria irekebishwe ili hawa mapadri waruhusiwe kuoa kwani sasa hii ni aibu kwa kanisa, kuliko kuendelea kuchafua taswira ya misingi ya dini ambayo imekuwepo tangu enzi na enzi.
“Mbona mapadri wengine wa Ulaya Mashariki wa madhehebu ya Katoliki (Ukranian Greek Catholic Church na Coptic Catholic Church) wanaoa? Kwa nini na wa kwetu wasioe?” alihoji mmoja wa waumini hao katika mahojiano na mwandishi wetu ndani ya ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
BARUA YA WAZI KWA PAPA
Mbali na waumini wa hapa nchini, mapema mwaka jana, wanawake wapatao 26 waishio nchini Italia, walimwandikia barua ya wazi Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis wakimueleza mateso wanayopata kwa kuwa na uhusiano wa siri wa kimapenzi na baadhi ya mapadri wa kanisa hilo.
Mkuu wa Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis.
PAPA ANENA
Akifafanua sakata hilo katika mahojiano maalum na Jarida la Republica la jijini Vatikani, Papa Francis alikiri kuwepo kwa taarifa za mapadri kuwa na uhusiano wa kimapenzi, kauli ambayo ilipingwa vikali na msemaji wa kanisa hilo, Federico Lombardi kwa madai kuwa mwandishi wa jarida hilo alimnukuu papa vibaya.
Mbali na hayo, padri mmoja aishiye Italia kutoka Kanisa la Kigiriki la Byzantine lililo chini ya Mamlaka ya Vatican, Jani Pecoraro alisema ifike wakati sasa nyakati zitambuliwe kwani kuoa kwa mapadri hakuondoi weledi wa huduma zao.
“Tunapaswa kusoma nyakati na hakuna shaka kwamba jamii ya sasa imekuwa ikiibua hoja kuwa mapadri waliooa wanaweza kuwa na kiwango sawa cha utumishi na wengine,” alikaririwa padri huyo.
PAPA AWA MAKINI
Hata hivyo, Papa Francis amekuwa makini na jambo hilo huku akieleza kuwa zuio la mapadri kuoa liliasisiwa karne 10, ikiwa ni karne tisa nyuma kabla ya kifo cha Yesu Kristo huku kukiibuka sintofahamu juu ya uamuzi wa papa juu ya mapadri wanaokiuka misingi hiyo.
PIGO KWA KANISA
Mbali na waamini wanaotaka mapadri kuruhusiwa kuoa, wapo wanaoliona jambo hilo kuwa ni pigo jipya kwa kanisa kwani wanatamani mapadri kuendelea kuwa waseja.
Father Urbanus Ngowi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi.
Kuhusiana na sakata hilo, gazeti hili lilikwenda Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kukutana na Katibu wa Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, Denis Aminias na kuzungumza naye ambapo alisema:
“Sisi kama kanisa tutaendelea kusimamia katika misingi ileile ya mapadri kutooa.”