WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAJIUZA SH.2000

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Farao! Kumekuwa na madai ya baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi mjini hapa kujiuza kwa waendesha bodaboda kwa gharama ya shilingi elfu mbili tu.
Mwanafunzi anayedaiwa kujiuza kwa waendesha Bodaboda.
Kufuatia madai hayo, mwandishi wa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ mjini hapa alifanyia kazi madai hayo na kufanikiwa kumnasa Ally Shabani (34) ambaye ni dereva wa bodaboda akiwa na mwanafunzi wa darasa la nne, Shule ya Msingi ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa (jina tunalo).Tukio hilo la kushangaza na kusikitisha pia, lilijiri Jumamosi iliyopita saa 7 mchana katikati ya mashamba ya mkonge yaliyopo Kihonda Kwachambo ambayo yanamilikiwa na Jeshi la Magereza jirani kabisa la Gereza la Kihonda.
MAMA MZAZI AISAKA OFM
Awali, mama mzazi wa denti huyo, Mariam Jongo alimtafuta Kamanda wa OFM Mkoa wa Morogoro na kumweleza kuhusu tabia ya bodaboda huyo na mwanaye, alisema:
”Naomba msaada wako baba, kuna dereva wa bodaboda nimempa tenda ya kumpeleka mwanangu shule.
“Lakini cha ajabu nasikia anamshawishi mwanangu mwenye umri wa miaka 9 ambaye hata maziwa hayajaanza kutoka kifuani ili afanye naye mapenzi akitumia chambo cha shilingi elfu mbili, hivyo naomba msaada wako kama kamanda wa kufichua maovu.”
Waliponaswa kichakani.
OFM YATOA MBINU
Kamanda wa OFM alimpa maelekezo mama huyo ya kutafuta vijana wa polisi jamii wa kata ambapo baada ya kupatikana mwandishi wetu alimpa maelekezo denti huyo na baadaye kwa kushirikiana na polisi jamii na OFM walitega mtego.
DENTI AMPIGIA BODABODA
OFM alimuita denti huyo na kumpa simu ili ampigie bodaboda huyo ambapo alimtaka aende kijiweni kwake Kihonda kwa Chombo, Mwisho wa Hiace. Denti alilazimishwa na mama yake afike kwenye kijiwe hicho akiwa anafuatwa kwa karibu na OFM na polisi jamii.
BODABODA AMPANDISHA DENTI KWENYE BODABODA
Bila kujua kuwa yupo kwenye mtego, bodaboda huyo alimpakia denti ambaye alionywa kutosema kuhusu mtego na kuondoka naye huku akiendelea kufuatiliwa kwa nyuma na kikosi kazi hicho.
Alipofika jirani na Barabara ya Mazimbo, alisimama, akataka kuingia  naye gesti lakini akajishtukia kwa vile ilikuwa mchana na jua kali.

Dereva bodaboda Ally Shabani aliyedaiwa kukutwa na mwanafunzi akiwa mikononi mwa wananchi.
AAMUA KWENDA MKONGENI
Bodaboda huyo alipoona ilikuwa vigumu ‘kujitoma’ gesti na mtoto wa watu, alielekea kwenye shamba la mkonge lililoko kando ya Barabara ya Dodoma na kuzama ndani.
Njemba huyo alijiongeza kwa kusimamisha bodaboda katikati ya shamba na kukaa chini na mtoto huyo ambapo walianza ‘love story’ kwanza.

OFM HIYO!
Ndani ya  dakika 10 tu, OFM na kundi lake waliwavamia kwa nyuma na kumkamata bodaboda huyo na kumuuliza kisa cha kuangukia kwa mtoto kama huyo ambaye ni sawa na mwanaye wa kumzaa akiwa ameshamkatia shilingi elfu mbili.

...Akivuja damu baada ya kuminyiwa kichapo.
UTETEZI WAKE
Katika utetezi wake, bodaboda huyo huku akiangua kilio alimtupia lawama shetani na kuomba msamaha akisema yeye ni mume wa mtu na mkewe analea!
”Shetani kanipitia jamani, mke wangu analea mtoto wetu wa mwisho ana mwaka mmoja kasoro, naombeni msamaha yaishe hapahapa, mnifichie aibu hii,” alisema bodaboda huyo.

WATU KIBAO
Baada ya muda habari za bodaboda huyo kufumwa zilisambaa kwa kasi ya upepo na watu kibao walifurika kwenye shamba hilo huku baadhi ya bodaboda wenzake kwa hasira walimshushia kichapo mwenzao huku baadhi wakitaka kumuua.


Binti huyo akiwasili kijiweni.
POLISI WAITWA
Baada ya kuona jamaa anaweza kuuawa, OFM waliita polisi wa pikipiki ambapo kwa mshangao, mmoja wa polisi hao alisema:
”Sisi tuna bifu na bodaboda baada ya mwenzetu kupigwa kule Mindu. Kama unaweza mpakie kwenye pikipiki yako mlete kituoni.”
Ilibidi OFM iite askari magereza ambao walimchukua bodaboda, denti  na mzazi wake na kwenda ofisi zao zilipo jirani na shamba hilo.
Baadhi ya watu, hasa wanawake waliokuwepo eneo hilo walisikika wakisema huenda bodaboda huyo alikuwa na lengo la kishirikina.
”Hii siyo bure hiki kitoto kinajua nini katika mapenzi. Huyu huenda ametumwa na mganga wa kienyeji. Sisi wamama tuko hatuna waume ameshindwa nini kuja... kwetu?” alihoji mwanamke mmoja.


...Wakiondoka.
MADAI YA KUJIUZA
Kwa mjini Morogoro, baadhi ya bodaboda wanadaiwa kutumia nafasi ya kuwa na chombo hicho cha usafiri kuwalaghai wanafunzi wa shule za msingi kwamba, wakilala nao watakuwa wanawapakiza kwenda shule na pia kutumia shiling elfu mbili kama chambo kikubwa.
“Kwa sasa mjini Morogoro madenti wa shule za msingi kujiuza ndiyo fasheni, wanarubuniwa na shiling elfu mbili na lifti. Jamani, watoto wetu watasoma kweli?” alihoji mwanamke mwingine.

STEVE NYERERE ANADAIWA KULAMBA FEDHA ZA KABURI!

Mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akiwa kwenye kaburi la marehemu Kuambiana.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, kaburi la nguli huyo wa sinema lilipokuwa linatimiza mwaka mmoja, ilidaiwa lilitoka fungu la shilingi milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ili zijengee kaburi hilo lakini zikazuiwa kwanza kwenye mifuko ya mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Wiki moja kabla ya shughuli ya misa ya kutimiza mwaka mmoja kifo cha marehemu, Nyerere (Steve) alipewa alipewa shilingi milioni moja, akakaa kimya hadi kaburi likajengwa na mke wa marehemu Julieth Lite (Diwani wa Kunduchi) kwa kutumia fedha zake,” kilisema chanzo hicho.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
UBUYU WAZIDI KUMWAGWA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, siku moja kabla kumbukumbu iliyofanyika Jumapili iliyopita (Jumamosi), mjane wa marehemu alipokea shilingi laki saba kutoka kwa mtu aliyejisajili kwa jina la Albert Msando akimwambia ni mchango wa Makonda wa kujengea Kaburi.Baadaye iliingia shilingi laki tatu kwenye namba nyingine ya simu ambayo ilielezwa kuwa ni mchango wa kujenga kaburi uliotoka kwa mwigizaji Jacob Steven ‘JB’.
STEVE NYERERE AJINADI
Wakati maandalizi ya misa yakiendelea, Jumamosi jioni, Steve Nyerere na baadhi ya wasanii walitupia picha kwenye mtandao wa kijamii huku wakisindikiza na ujumbe uliojinasibu kuwa wanamshukuru Mungu kuashiria wamefanikisha kujengea kaburi hilo kitu ambacho kilikanushwa baadaye na mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude.’
“Jamani hakuna msanii aliyehusika kujengea kaburi zaidi ya mke wa marehemu, Julieth Lite,” aliandika mitandaoni Dude ambaye ni mdogo wa Julieth.
Mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude.’
MJANE AFUNGUKA
Amani lilimvutia waya mjane wa marehemu Kuambiana, Julieth ambaye naye alisisitiza kuwa kaburi hilo alilijenga kwa fedha zake mwenyewe.“Nilijenga mwenyewe lakini wakati tunakaribia kufanya misa (Jumamosi) nakumbuka ilikuwa kama saa tano na nusu usiku,  ghafla nilipokea shilingi laki saba kutoka kwa Msando nikaambiwa ni za Makonda na baadaye nikapokea laki tatu nikiaambiwa ni za JB,” alisema Julieth.
NYERERE ANASEMAJE?
Amani lilipomtafuta Steve Nyerere na kuulizwa kama ni kweli alipewa shilingi milioni moja na Makonda kisha akakaa kimya na kama zile laki saba zilizokabidhiwa na Msando zinahusiana na zile alizopewa na Makonda, alijibu:
“Ninavyojua mimi hizo fedha hajatoa Makonda, tumetoa sisi wasanii kama huamini ongea na JB huyu hapa (akampa simu).
“Tulitoa sisi wasanii, kama ulikuwepo siku ile pale makaburini ungeona alichoongea mke wa Kuambiana. Ni sisi kaka ndiyo tumetoa. Wewe mpigie mke wa marehemu halafu muulize alichosema siku ile makaburini halafu nipigie tena,” alimalizia JB na kukata simu.
Alipopigiwa Makonda ili aweze kudadavua kiundani juu ya fedha alizotoa na nani aliyempa alijibu:
“Nipo katika kikao unaweza kunitumia meseji?”
Licha ya kutumiwa meseji, hadi tunakwenda mitamboni, hakuwa ametoa jibu lolote.

KUMBE JOHARI ALIKUWA MAMA NTILIE!!!! SOMA HAPA

KABLA hajaanza ‘kuuza sura’ kwenye runinga, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’ alikuwa akijihusisha na kazi ya upishi na uuzaji wa chakula biashara ambayo aliifanya jijini Dar kabla hajajiunga na Kundi la Sanaa la Kaole baada ya kuhitimu mafunzo ya Hotel Management.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’.
Johari alianza kupika na kuuza chakula kwenye catering ya shangazi yake huku akihangaika kutafuta njia ya kutimiza ndoto yake ya uigizaji aliyokuwa nayo tangu akiwa kijijini kwao Bugoyi mkoani Shinyanga.Johari anasema aliamua kusomea masomo ya upishi kwa kushinikizwa na ndugu zake walioamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kupika chakula kizuri na kitamu japo moyoni mwake hakuwa na ‘hobi’ hiyo.
“Kabla ya kutimiza ndoto yangu hii ya uigizaji, nilikuwa napika na kuuza chakula, si unajua katika maisha kabla hujatimiza ndoto na malengo yako ni lazima uhangaike kwa kupitia vikwazo na vizingiti vingi?
“Hivyo mimi nilijikuta nikiangukia kwenye u-hotelia japo sikuwa interested kabisa, lakini kwa sasa namshukuru Mungu kwa kuwa nimetimiza ndoto yangu,” alisema Johari katika mahojiano maalum na mwandishi wetu hivi karibuni.

MOSE IYOBO ASEMA HALI YA BEBI ( AUNT) IMENIFANYA NISIENDE LONDON

MPENZI wa staa maarufu wa filamu Bongo Aunt Ezekiel, Moses Iyobo ambaye pia ni dansa mahiri wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa hakwenda kwenye shoo iliyokuwa ikifanyika katika Jiji la London kutokana na hali ya mpenzi wake.

Staa maarufu wa filamu Bongo Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moses Iyobo.
Akichezesha taya na Centre Spread, Mose alisema kuwa  alishindwa kujumuika na wenzake akihofia hali ya mpenzi wake hivyo alipenda kuwa naye karibu hadi kwenye hitimisho lake la kumpata mtoto wao.
“Unajua nashindwa kwenda mbali sana kutokana na hali ya mpenzi wangu kwa kuwa nakuwa na wasiwasi sana hivyo hata London nimeshindwa kwenda kwani natamani kuona hatua kwa hatua ya bebi wangu hadi kumpata mtoto wetu,” alisema Mose.

MZEE WA UPAKO ASEMA ALISHIRIKIANA NA WACHAWI KUTAPELI MAMILIONI YA PESA

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi GRC, Lusekelo Antony ‘Mzee wa Upako’ amekiri kushirikiana na waganga wa kienyeji kujipatia pesa kwa njia ya utapeli wakati akifanya biashara ya madini ya rubi.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi GRC, Lusekelo Antony ‘Mzee wa Upako’.
Akizungumza katika ibada maalum hivi karibuni kanisani kwake Ubungo Kibangu jijini Dar, Lusekelo alisema utapeli huo aliufanya sehemu mbalimbali ikiwemo mkoani Dodoma kwa kuhusisha sangoma hao ambapo walikuwa wakimtaka mteja kuwapatia pesa huku wakimuelekeza mahali madini hayo yanapopatikana.
Alisema baada ya zoezi la kumuelekeza mteja, wao (Lusekelo na wenzake) walitengeneza kitu kinachofanana na madini hayo ambapo mteja hutoa pesa nyingi akiamini kuwa ni madini halisi.Kuhusu waganga hao, alisema walikuwa wakiwaandaa feki ambapo walimchukua mteja aliyehitaji madini hayo na kumtoza pesa nyingi ili mganga awaelekeze mahali yalipo na baada ya hapo huchukua yale madini feki kwa wingi na kwenda kuyaficha mahali ambapo mganga alimuelekeza mteja.
Alisema utapeli wa biashara ya madini ulimfikisha nchi mbalimbali duniani lakini Neno la Mungu lilipomfuata aliungama na kuanza kumtumikia yeye (Mungu).“Ulikuwa ni utapeli wa kiwango cha juu sana, kabla ya kufikia mafanikio maishani, watu hujikuta tukipitia njia zisizo halali. Msidanganywe na mtu yeyote, mafanikio ya kweli yanakuja kwa njia halali hadi sasa kila nikikumbuka huwa nasema Mungu anisaidie sana,” alisema Lusekelo.
Baada ya ibada hiyo, baadhi ya waumini walisikika wakiguna huku wakishangaa kusikia simulizi ya utapeli ya mchungaji wao.“Mmh, kumbe mtumishi amekutana na mapito mengi sana, hadi utapeli?” walisikika baadhi ya waumini wakati wakitoka kanisani hapo.  

Miriam Jolwa ‘Jini Kabula Arekodiwa Kwenye Mkanda wa Ngono

SHABAAASH! Staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, anadaiwa kurekodiwa mkanda wa ngono na kusambazwa katika mitandao ya kijamii, Amani linakupa stori kamili.

Staa aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Chanzo cha habari hii kimeeleza kwamba, tukio hilo lilitokea hivi karibuni baada ya mtu anayedaiwa kuwa ni mchumba wa staa huyo kumrekodi video hiyo na baadaye walipopishana kauli, akaamua kuisambaza kwa njia ya CD.
“Jana bwana niliona video ya utupu ya Jini Kabula ikiuzwa kitaani kwetu katika CD jambo ambalo ni aibu sana,” alisema mtoa ubuyu wetu, mkazi wa Manzese, jijini Dar.
Amani lilishuhudia baadhi ya picha zinazodaiwa kuwa zilikatwa kutoka katika video hiyo ndipo mwanahabari wetu alipomvutia waya Jini Kabula ili kujua nini kilimsibu hadi akarekodiwa video hiyo.Alisema kwa mazingira ya tukio hilo, anashindwa hata ajibu nini maana haelewi kilichotokea hadi mkanda huo ukasambaa kiasi hicho na kumsababishia matatizo kwa ndugu zake.
“Kiukweli nashindwa hata nikujibu nini maana kama aibu tayari imeshanikuta, hivyo sioni kama naweza kuongea kitu chochote kwa sasa kikanisafisha, kikubwa namwachia Mungu maana sina tena pa kuuficha uso wangu kwa hiki kilichotokea, yaani yamenikuta,” alisema Jini Kabula ambapo alipobanwa zaidi kuhusu aliyemrekodi, alijibu kuwa ni mchezaji wa timu ya Yanga pasipo kumtaja jina.
“Bwana ni mchezaji wa Yanga, alikuwa mtu wangu.”

UNA UHAKIKA GANI KAMA MPENZI WAKO HAWEZI KUNASWA NA WAJANJA, KWA KIPI?

NIkweli mapenzi ni imani, yaani kuamini kwamba uliyenaye anakupenda hata kama ukweli unaweza usiwe hivyo. Wengi walio na wapenzi wanajiaminisha kwamba wanavyowapenda wenza wao ndivyo wananvyopendwa.

Pia wapo ambao wanaamini kwamba eti kwa namna wanavyoonesha mapenzi yao, hata kwa dawa hawawezi kusalitiwa. Utamsikia mwanamke akisema; “bwana wangu mimi kwangu hapindui, ananipenda sana na hawezi kunisaliti’.
Mtu anayesema maneno hayo anajipa imani na ukifuatilia unaweza kukuta huyo anayesema hivyo, mpenzi wake ni kiwembe ile mbaya.
Ni wanaume wangapi ambao wewe unawajua wake zao wanawaamini sana lakini kumbe wanasalitiwa sana kwa siri? Ni wanaume wangapi, tena wengine wakiwa marafiki zako ambao wake/wapenzi wao wanawaamini sana lakini wanasifika kwa kupenda totozi?
Watu hao wako huko mtaani, tena wengi tu na yawezekana hata mpenzi wako unayemuamini sana si muaminifu, anajifanya ni mtu mpole, anayejiheshimu, asiye na mawazo ya kukusaliti lakini kumbe akiwa mbali na wewe, ni hatari.
Lakini sasa, kama ukweli uko hivyo, tuna sababu ya kuishi kwa hofu tukihisi kwamba wapenzi wetu si waaminifu? Hapana! Kuishi kwa wasiwasi ni kujipa presha za bure na za kujitakia.
Ni kweli kwa ulimwengu wa sasa hakuna mtu anayeweza kumuamini mpenzi wake kwa asilimia zote lakini kisaikolojia unatakiwa kumuamini kwa asilimia zote huyo uliyenaye.Hata kama yapo anayofanya akiwa mbali na upeo wa macho yako, iwe ni yeye na Mungu wake lakini kwa kuwa hujawahi kumfumania wala kuona ishara zozote za kwamba anakusaliti, jenga imani naye.
Imani unayojipa ni kwa lengo la kujipa amani ya moyo, uishi kwa furaha na kujiweka mbali na presha zisizokuwa na msingi.Ila sasa, nawashangaa sana wale ambao wanajiaminisha kwamba wapenzi wao hawawezi kuwasaliti kwa namna yoyote. Unajua kwa nini nawashangaa?
Ni kwa sababu huko mtaani kuna vishawishi vingi, wapo wasichana wazuri sana ambao wao hawajali kwamba huyu ni mume wa mtu, watamtega kwa kila namna ili wamnase.Wapo ma-handsome na mapedeshee ambao wakimtaka mwanamke yeyote watafanya kila njia wampate. Sasa wewe ambaye uko kwenye uhusiano unafanya yapi ya kumfanya mwenza wako ayashinde majaribu?
Maana usikae na kusema mpenzi wako hakusaliti, lazima uwe na sababu za kusema na kujiaminisha hivyo. Je, umejenga mazingira ya mpenzi wako kukuona wewe ndiyo wewe wengine takataka? Kama hujafanya hivyo usijidanganye, kaa ukijua wajanja wanakumegea penzi lako.
Ninachotaka ukijue leo kupitia makala haya ni kwamba, huko mtaani kuna mitego mingi kwa wapenzi kiasi kwamba ni wachache sana wanaoweza kuikwepa. Mfanye mpenzi wako awe kati ya wale ambao hawanasi kirahisi.
Mpende, mjali, mthamini, mpe penzi linalostahili lakini pia zungumza naye kila mara kwamba, hao wazuri huko nje wanaomtaka, hawana mapenzi ya kweli. Ni walaghai tu wanaomtamani ila mwenye mapenzi ya kweli kwake ni wewe.
Pia zungumza naye kuhusu magonjwa, mueleze kabisa kwamba, hata kama kwa tamaa zake atakusaliti huko gizani, magonjwa yatakuja kumuumbua.
Naamini ukifanya hivyo, hata kama hutawaambia watu kwamba mpenzi wako hawezi kukusaliti, wewe mwenyewe utakuwa na imani kubwa kwa kuwa umemuandaa kukwepa vishawishi. Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.

Haya Ndio Mabilioni Ya Watanzania Yanayoliwa na Watu Wachache Kijanja

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa ripoti ya ukaguzi mjini Dodoma jana,Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad alisema ukaguzi huo umefanywa katika taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109.

Alisema usimamizi wa bajeti kwa mamlaka ya Serikali za Mitaa ulibaini kuwapo upungufu wa fedha za maendeleo Sh bilioni 312. 04, Serikali kuu Sh bilioni 1.8, fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo hazikutumika lakini hazikutolewa ni Sh bilioni 417.
Fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo hazikutumika ni Sh 203.13, alisema.
Alisema ripoti hiyo imebaini ukiukwaji wa matumizi ya utoaji wa misamaha ya kodi, kuendelea kwa mishahara hewa, usimamizi mbovu wa mipango miji,madeni ya Serikali katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Kuhusu misamaha ya kodi, Profesa Assad alisema iliyotolewa kwa mafuta yanayotumika migodini imefikia Sh bilioni 22.33 kati ya yale yaliyotakiwa kutumiwa na makampuni ya Geita Gold Mine na Resolute Tanzania Ltd na yalipelekamafuta hayo kwa wakandarasi wasiostahili msamaha wa kodi.
“Matumizi ya misamaha ya kodi kwa malengo tofauti na yasiyokusudiwa na kusababisha upotevu wa Sh milioni 392.7, iliyosababishwa na Kampuni ya Kiliwarrior Expenditions Ltd. ya Arusha iliyokuwa imesamehewa kodi ya Sh milioni 465.2 kuingiza magari 28 ambako kati ya Sh milioni 465.23, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeambulia kukusanya Sh milioni 72.5.
“Misamaha ya kodi ya Sh milioni 53.4 ilitolewa kwa Kampuni ya Kilemakyao Mountain Lodge Limited kwa ajili ya mradi wa ujenzi na upanuzi wa hoteli katika Kijiji cha Changarawe wilayani Meatu. Kampuni hii iliagiza magari matatu kwa kutumia msamaha wa kodi wa gari moja ya Hyundai Santa.Magari mengine ni BMW X5 na Toyota Land Cruiser Prado hayakufahamika yalipo,” alisema.
Alisema amebaini kudorora kwa uwekezaji wa Serikali kwenye makampuni mbalimbali ambako Serikali ina hisa kutokana na kuchelewa kuongeza mtaji, wakati inapohitajika kufanya hivyo kama ambavyo inataka kutokea katika benki ya NBC Ltd.
Mashirika ambayo yamegubikwa na kusuasua kwa usimamizi wa uwekezaji wa Serikali ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania (ATC),Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Shirika la Reli Tanzania (TRL) ambayo yote yanahitaji ruzuku kutoka serikalini.
Mashine za EFD’s
Katika ukaguzi wa malipo, CAG amebaini kampuni binafsi hazitumii mashine za elektroniki za kutolea stakabadhi na hivyo kusababisha Sh bilioni 4.4 kutokuwa na stakabadhi hizo wakati taasisi za Serikali zimefanya malipo yenye thamani ya Sh bilioni 4.6 bila kutumia mashine hizo, mbali na halmashauri 22.
“Katika suala hili, TRA ilitoza faini ya Sh milioni 440.8 kwa wafanyabiashara walioshindwa kutumia EFD’s ambako milioni Sh 72 zililipwa na hivyo kufanya bakaa ya Sh milioni 369 ambayo haikulipwa,” alisema Profesa Assad.
Mapato ya ndani
Ukaguzi wa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2014, ulibaini taasisi zilizo katika mpango wa kubakiza maduhuli na hazikurejeshwa zilikuwa Sh bilioni 32.74, hivyo kuathiri utekelezaji wa kazi zilizokuwa zimepangwa na taasisi husika.
Mishahara hewa
Ukaguzi wa CAG umebaini wafanyakazi walioacha kazi na kustaafu wameendelea kulipwa mishahara kupitia akaunti zao, licha ya Serikali kuwekeza katika mfumo wa Lawson kama njia ya kudhibiti hali hiyo.
Pia fedha za makato ya mishahara yao zimeendelea kupelekwa kwenye taasisi kama vile Bima ya Afya, TRA na mifuko ya hifadhi ya jamii.
Kutokana na hali hiyo mpaka sasa fedha zilizolipwa ni Sh milioni 141.4.
Alisema katika halmashauri 36, Sh bilioni 1.01 zililipwa kwa watumishi waliotoroka kazini.
Wizara ya ujenzi
Ripoti hiyo imeitaja Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Waziri Dk.John Magufuli kuwa inaongoza kwa kudaiwa na wakandarasi.
Alisema mpaka anatoa ripoti hiyo wizara hiyo inadaiwa Sh bilioni 800.
Lakini jambo la kushangaza wizara hiyo pia imetumia Sh bilioni 250 nje ya bajeti husika.
UKAGUZI WA MIRADI
Alisema ukaguzi wa miradi ya maendeleo mwaka 2013/14 ulihusu miradi mikubwa mitano.
Miradi hiyo ni Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), Mfuko wa Afya (HBF), Mfuko wa Barabara (RF), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) na miradi mingine ambayo inatekelezwa wizara, idara na mashirika ya umma.
“Katika ukaguzi wa hesabu za halmashauri 162, tulibaini Sh 52.7 zilizoidhinishwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo hakikutolewa hivyo kuathiri utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa.
“Hii imechangia malipo yaliyocheleweshwa kulipwa mwaka wa fedha 2013/14,” alisema.
Alisema ukaguzi ulibainia fedha zilizotolewa na kutotumika ndani ya mwaka wa fedha 2013/14, ni Sh bilioni 495.9 ikiwa ni asilimia 25.45 ya fedha zote za miradi.
“Sababu kubwa ya bakaa hii ni pamoja na ucheleweshaji wa kutoa fedha kwa wadau wa maendeleo na mchango wa Serikali, mchakato mrefu wa taratibu za ununuzi, uwezo mdogo wa halmashauri wa kutumia fedha za miradi na wafanyakazi wachache wenye utaalamu katika kusimamia fedha za miradi.
Ocean Road
Alisema Taasisi ya Ocean Road inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya uchunguzi na matibabu kwa wagonjwa wa kansa.
“Mahitaji halisi ni mashine 36, wakati zilizopo ni mashine 11 tu ambazo kati ya hizo, mashine tatu zimeshapitwa na wakati zinangoja kuondolewa na mashine nne zinahitaji kufanyiwa ukarabati.
“Hali hiyo inasababisha ucheleweshaji wa matibabu hususan mionzi kwa wagonjwa ambako humchukua mgonjwa zaidi ya miezi mitatu kutibiwa wakati viwango vinavyokubalika kimatibabu ni chini ya wiki mbili,” alisema.
Aliishauri Serikali kuchukua hatua za haraka kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la vifaa katika taasisi hiyo.
Mipango Miji
Alisema ripoti yake imethibitisha halmashauri 148 ambazo ni asilimia 80 zinaendelezwa bila kuwa na mipango kabambe inayoweza kutoa miongozo wa shughuli zote za uendelezaji wa miji nchini.
“Halmashauri 96 au asilimia 65 kati ya halmashauri 148, hazijawahi kuandaa mipango kabambe tangu zianzishwe,” alisema.
Alisema maeneo mengi yanaendelezwa bila kufuata mipango kabambe iliyopo.
Usambazaji dawa
Alisema kwa mujibu wa ukaguzi, imebainika tathmini ya makadirio ya uhitaji wa dawa na vifaa tiba muhimu katika vituo vya afya haufanyiki kwa uhakika.
Alisema hali hiyo inatokana na asilimia 50 ya ripoti zinazohitajika za makisio ya dawa za vifaa tiba muhimu kutoka halmashauri za wilaya kutowasilishwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kama inavyotakiwa.
“Imebainika asilimia 54 ya oda zinazopokelewa na MSD kutoka bohari za kanda ni kuanzia muda wa siku 14 kulingana na muongozo wa MSD.
“Hii imesababisha kutetereka kwa mtaji kushuka kwa zaidi ya asilimia 69 kutoka Sh bilioni 81 mwaka 2008 hadi Sh bilioni 25 mwaka 2013.
“Hii imechangiwa na ongezeko la deni la Serikali ambalo limeongezeka zaidi ya mara nne kutoka Sh bilioni 14 mwaka 2008 hadi Sh bilioni 69 mwaka 2014,” alisema CAG.
Kutokana na hali hiyo, CAG alipendekeza uboreshaji wa upatikanaji wa dawa na vifaa muhimu katika vituo vya huduma ya afya.
“Ninapendekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na MSD kutathimini hali ya mtaji wa uendeshaji wa mfumo mzima wa makisio na usambazaji wa dawa na vifaa tiba muhimu kwa lengo la kutatua tatizo la uhaba wa dawa,” alisema.
Wastaafu,watumishi
Kuhusu wastaafu, ripoti yake imegundua Sh milioni 5.43 zimelipwa kama posho na pango kwa watumishi walioko ubalozini nje ya nchi.
“Hii ni kinyume na kanuni za kudumu za utumishi, fedha hizo zinazoendelea kulipwa kwa wastaafu hao ambao hawafanyi kazi si zingeweza kulipwa kwa wafanyakazi?” alihoji Profesa Assad.
Majengo ya Serikali
Alisema ukaguzi huo umebaini majengo mengi yanayomilikiwa na Wakala wa Majengo yalijengwa kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita, hali inayosababisha majengo hayo kuwa katika hali isiyoridhisha.
“Ilibainika hakuna utaratibu madhubuti wa usimamizi wa ukarabati wa majengo ya Serikali, hii ni kwa kuwa mikoa mingi haifuati taratibu zilizopo za ukarabati wa majengo ya Serikali.
“Kati ya mikoa sita iliyotembelewa hakukuwa na mkoa hata mmoja ulioweza kufanya marekebisho ya viwango vilivyowekwa vya ukarabati wa majengo ya Serikali.
“Pia hakukuwa na nyaraka kama vile vitabu vya rejista vya kuweka kumbukumbu ya hali ya ukarabati wa majengo katika ofisi zao na pale ukarabati unapotekelezwa, hutekelezwa bila kuwa na mpango kazi uliowekwa,” alisema.
CAG alipendekeza Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Majengo kuweka sera ya ukarabati wa majengo yanayomilikiwa na Serikali na kufuatilia utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi ya majengo hyo.
Mifumo ya uhifadhi
Alisema katika ukaguzi uliofanyika ilibainika mipango ya usimamizi wa mazingira iliyoandaliwa na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), haitilii mkazo suala la viashiria hatarishi.
“Ilibainika NEMC halikutoa adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 kwa makampuni mbalimbali ya migodi inapokiuka sheria hiyo.
“Na hata pale adhabu zinapotolewa hakukuwa na ufuatiliaji mzuri kuweza kubaini kama adhabu husika imetekelezwa ipasavyo,” alisema.
Alisema pia halmashauri hazifanyi ufuatiliaji wa shughuli katika migodi hali inayosababisha NEMC kushindwa kuwa na picha halisi juu ya utunzaji mazingira katika migodi nchini.
“Vilevile imebainika kuwa hakuna utaratibu wa shughuli za usimamizi wa mazingira migodini, NEMC ilishindwa kuratibu kwa ufanisi ushirikiano wa wadau mbalimbali katika usimamizi wa mazingira migodini,” alisema.
CAG amependekeza NEMC kutathmini utekelezaji wa mfumo ulipo pamoja na kuanzisha uandaaji wa taarifa itakayoonyesha hali ya mazingira katika sekta madini na kutoa adhabu stahiki kuzuia uvunjaji wa sheria kutojirudia.
Huduma za ugani
Alisema katika uchunguzi huo, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika hawajasambaza kwa ukamilifu miongozo inayohusiana na utoaji wa huduma za ugani kwa maofisa ugani.
“Pia hakuna vitabu vya rejista na ratiba zinazoonyesha utendaji kazi wa maofisa ugani hali inayosababisha utekelezaji usioridhisha wa mipango na miradi ya mendeleo ya kilimo,” alisema.
Alisema ripoti hiyo pia ilibaini kuwapo teknolojia duni za shughuli za ilimo, ucheleweshaji wa fedha na kusababisha huduma duni za ugani na ufuatiliaji na tathimini za utoaji wa huduma za ugani kutofanyika ipasavyo.
“Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika zifanye tathmini ya huduma ya ugani na kuangalia na jinsi gani hizo zinaweza kuboreshwa katika maeneo ya uandaaji wa mipango, uratibu, uwezeshaji, ufuatiliaji na utoaji wa mrejesho ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo,” alisema.
Kauli ya PAC
Akizungumzia ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau alisema inaonyesha mapato ya serikali bado yanapotea na kulitaka Bunge lijalo lipambane na hali hiyo.
“Kwa ujumla hali ni mbaya, kwa mfano Wizara ya Ujenzi ililidanganya Bunge lililopita, angalia Tanroads (Wakala wa Barabara Tanzania), wanaongoza kwa madeni. Lakini pia Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kimetumia fedha vibaya na hili lazima tulishughulikie haraka” alisema Mwidau.
(CHANZO: MTANZANIA)

AUNT NA WEMA WAPATANISHWA UPYA VILIO TUPU VYATAWALA!

Aunt Ezekiel akimbembeleza Wema baada ya kupatanishwa.
Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.
Habari zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.
Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.
Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
“Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.
Wakiwa na rafiki yao Daudi Mambya anayedaiwa kuwapatanishwa.
Ilielezwa kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco Beach akimuambia kuwa anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo akimwambia Aunt naye wakutane ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na Wema, huku akifanya mawasiliano na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili huku kila mmoja akibaki katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa uso.
Sosi huyo alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya lakini Daudi aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila mmoja.Mambo yakipokaa vizuri, wawili hao walishuhudiwa wakiwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio kilichochukua takribani nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.
“Yaani mpaka Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza kulia.
“Yaani ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda huyo.Akizungumza na gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua kuwapatanisha wawili hao kwa kuwa alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na kwamba wote ni rafiki zake.
Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”
Wema alisema: “Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

'AMAZING' SHOO YA DIAMOND ALIYOFANYA LONDON YAACHA GUMZO

AMAZING! Hiyo ndiyo kauli pekee unayoweza kuitamka kuakisi shoo baab’kubwa aliyoifanya mkali wa wimbo wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’, London, Uingereza, Risasi Mchanganyiko linakujuza zaidi.
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipagawisha wakazi wa jiji la London.
Shoo hiyo iliyoacha gumzo la aina yake nchini humo kutokana na kupata idadi kubwa ya mashabiki, ilifanyika Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa Royal Regency, maeneo ya Manor Park.
Chanzo chetu kilichoambatana na msafara wa Diamond kwenye shoo hiyo ijulikanayo kama Diamond are Forever, kiliweka bayana kuwa shoo hiyo ilikuwa ya kustaajabisha (amazing) kwani ilikadiriwa kuwa na watu zaidi ya 1500 ambao ni Wabongo waishio nchini humo waliochanganyika na wazungu.
Akitambulishwa mbele ya mashabiki.
“Jamaa kapiga shoo ya nguvu, watu walijaa kweli, si Wabongo pekee bali Wazungu nao walikuwepo. Si zile shoo za kupiga sebuleni ambazo wasanii wengi wa Kibongo huwa wanafanya. Yani hadi leo (Jumatatu) kila mtu anaizungumzia. Imeacha gumzo la aina yake.
“Ilikuwa yenye hadhi maana kiingilio kilikuwa ni shilingi laki moja na ishirini kwa V.I.P na elfu tisini viti vya kawaida, Wazungu walichanganyikiwa hadi ikabidi waulize Who is Diamond? (Diamond ni nani?) wakaambiwa na meneja wa msanii huyo, Babu Tale kuwa ni msanii anayeiwakilisha Tanzania akitokea Tandale, Dar es Salaam,” kilimwaga data chanzo hicho.

Mbali na umati huo ‘kuinjoi’ nyimbo za Diamond kama Kamwambie, Mbagala, Kesho na Nasema Nao na nyingine kibao, shoo hiyo iliongeza msisimko kufuatia uwepo wa balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Peter Kalaghe ambaye alipewa nafasi ya kuzungumza machache jukwaani, burudani ikaendelea.

Sababu za Wanaume Kuchepuka

NI matumaini yangu wapenzi wasomaji wa safu hii mko poa. Leo tunamalizia vipengele vilivyosalia wiki iliyopita, ungana nami.
6.Karaha
Hili pia ni tatizo la wanawake ambalo hawapendi kulikubali. Karaha nyumbani dhidi ya mwanaume huweza kumfanya ajisikie kuhitaji faraja nje ya nyumba. Na wanawake wengi wakimuona mwanaume yupo peke yake baa, hujua kuwa atakuwa amekimbia maudhi ya mkewe na anahitaji faraja.
7.Huruma ya wanawake
Hili nalo ni tatizo linalotumiwa vibaya na wanaume. Wanawake wengi wana huruma na ni wepesi wa kusamehe makosa ya wenza wao. Hii hutokana ama na woga wa maisha peke yao, au kutotaka mambo yao kutoka nje, hivyo huwasamehe haraka wanaume wao hata kwenye makosa ya wazi. Hili huwafanya wanaume kutojali na kurudia tena makosa yao.
8.Kazi na maumbile
Maumbile ya wanaume yako katika namna ambayo ni vigumu sana kwao kuvumilia kwa muda mrefu bila kuhitaji  wanawake, hivyo kama wakiwa mbali na nyumbani, hujikuta wakitamani tendo la ndoa.
9.Uhuru uliopitiliza
Kutokana na kazi, wanaume wengi huwa huru kwenye familia zao, kwa kuondoka asubuhi na kurudi usiku mwingi. Hii huwafanya kuweza kufanya lolote wakati wowote bila kuwa na hofu. Ni rahisi kwao kujenga uhusiano na wanawake wa barabarani au hata kazini kwake.

10. Ushawishi wa wanawake
Ingawa kiasili wanaume ni watu wa kutongoza, lakini wapo wanawake ambao huifanya kazi hiyo kwa ajili ya kutaka fedha au kuvuruga uhusiano kwa makusudi. Hutumia mbinu mbalimbali na wanaume hujikuta wameingia mtegoni bila kujua.

WAPENZI JAMANI, MNAKULA GIZANI MNAMFICHA NANI?

Natamani kucheka kwa jicho unalonikata na huku ukijisemea moyoni mwako kuwa siku ukinitia mikononi utanipasha nipashike, wapiiii, wan’kula huu na hasara juu. Hivi wee mung’unya jeuri ya kutaka kunipasha umeipata wapi? Kwa taarifa yako tu, hicho ni  kiburi cha nazi kutaka kushindana na jiwe.
Jamani leo nataka nizungumzie raha ya kusafiri, siku zote watu wengi, wanaume kwa wanawake wanapenda kusafiri usiku tena kukiwa na giza totoro, kweli si kweli?
Basi nawaambia raha ya safari ni mchana au hata kama ni usiku mwangaza uwepo babuuu…shurti mtu upate fursa ya kuona kule uendako.
Utaujua mji, utaona mandhari yake na kufaidi kuliko kusafiri usiku au kukiwa na giza.
Ndiyo, watu wanalipenda giza hawajui kuwa giza  ni la mwizi au wachawi… maana hata kama kuna taa wanazima na kuamua kusafiri gizani mpaka wanafika mwisho.
Jamani hakuna raha katika safari ya giza hata kidogo, kwani ukisafiri kweupe utaiona safari mwanzo hadi mwisho pia, mtu unapata fursa ya kuujua mji vizuri.Umenielewa au nimekuacha umelewa? Kama haitoshi nataka nikwambie kwamba utamu wa chakula ukione kwa macho yako kikiwa kwenye sahani safi.
Hapo hata kijiko cha kulia nacho ukikishika kinatulia mkononi. Utayaona maandalizi yaliyoandaliwa mezani na kukufanya uwe na hamu ya chakula ambacho machoni kitaonekana kuwa ni kitamu na kitakupa hamu ya kula, bado upo?
Hata ukila chakula huku unakiona ukisindikizwa na chombezo la maneno matamu hakika hutachoka kukitafuna kwa madaha huku utamu ukinoga na chenyewe kikikata kona katika mwili wako.
Eeeeheee! Acha niseme miye kwani  nisiposema leo nitasema  lini?  Unadhani nitasema nikiwa ndani ya kaburi?
 Kawaida ya wanawake huwa tuna milio yetu wakati wa safari, huwa tunahema kwa mihemo yenye kuongeza mahanjamu pale safari inapokolea.

Jamani kwa kuwa mada ni ndefu, tuonane wiki ijayo kwa mwendelezo wake.

SOMA SKENDO YA PADRI ALIYENASWA NA MREMBO, YATIKISA KANISA KATOLIKI

KISA cha Padri Anatoly Salawa (pichani) ambaye pia ana cheo cha Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, Tec), kunaswa hivi karibuni kichakani akiwa na mrembo, kimechukua sura mpya, Gazeti la Kufichua Maovu, Uwazi linakokotoa.
Padri Anatoly Salawa akitaharuki baada ya fumanizi hilo.
TUJIKUMBUSHE
Tukio hilo la kushangaza lilijiri hivi karibuni majira ya saa 8: 02 usiku ambapo padri huyo na mrembo walinaswa ndani ya gari aina ya Toyota RAV 4 lenye namba ya usajili T 674 ADA kwenye kichaka kilichopo maeneo ya viwanda na gereji za magari makubwa, Kurasini jijini Dar.
Gazeti ndugu na hili, Ijumaa la Mei 15, mwaka huu liliandika kwa kina habari hiyo ikiwa na kichwa kisemacho; PADRI WA KATOLIKI ANASWA KICHAKANI!
YALIYOJIRI SASA
Kabla ya tukio hilo halijapachikwa kwenye Gazeti la Ijumaa, Padri Salawa alipigiwa simu mara kadhaa ili kupewa nafasi ya kujitetea lakini hakupokea na hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa simu ya mkononi, hakujibu.
Gari aina ya Toyota RAV 4 lenye nambari ya usajili T 674 ADA alilonaswa nalo Kiongozi huyo wa dini.
GAZETI LATOKA, AWEKWA KITI MOTO
Kwa mujibu wa mtu wa karibu kutoka ofisi za Tec, Kurasini jijini Dar (jina tunalo) aliliambia gazeti hili juzi kuwa, baada ya Gazeti la Ijumaa kuingia mtaani, Ijumaa iliyopita, wakuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki walimuweka kikao padri huyo kwenye Ofisi za Tec na kumtaka aweke wazi kisa chote.
“Jamani mmeua bendi huku Tec. Mnajua kama Padri Salawa amewekwa kitimoto kikali sana? Yaani ni tatizo kubwa,” kilisema chanzo hicho.Kikaendelea: “Baada ya Gazeti la Ijumaa kutoka, maaskofu, mapadri nchini kote walishtuka! Kumbe magazeti yenu yanafika nchi nzima! Mimi nilikuwa sijui.
“Ilibidi awekwe kikao na kuulizwa nini kilitokea mpaka ametoka kwenye gazeti tena kichakani na mrembo halafu mbaya zaidi usiku mnene, ndipo akaanika kisa chote.”
Mrembo aliyenaswa kichakani na Kiongozi wa dini.
PADRI ASIMULIA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, padri huyo alisimulia kilichompata ambapo alisema kuwa usiku wa siku ya tukio, yeye alikuwa kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Kurasini ambapo huwa kunakuwa na muziki.“Alisema akiwa kwenye baa hiyo, alitokea msichana huyo na kumwomba ampeleke nyumbani kwake maeneo yaleyale kwa vile yeye ana gari na ni usiku.
“Akasema alimkubalia lakini alimwambia anamchukua mtu mwingine waongozane wote, yule msichana akakataa, akasema waende wawili tu.”
PADRI AINGIA LAINI, WAONDOKA
“Padri akazidi kusimulia kwamba, waliingia kwenye gari na msichana huyo, waliondoka kuelekea alikoomba kupelekwa ambako si mbali sana na baa hiyo.”
ENEO LA TUKIO
“Maaskofu waliendelea kumsikiliza. Huku akidondosha machozi, akasema kuwa walipofika eneo lililotokea tukio, alisimamisha gari kwa lengo la kumshusha msichana huyo, ndipo ghafla akavamiwa na watu na kuanza kupigwa picha, wengine kutaka kumshika.”
Mrembo huyo akifaa nguo baada ya kunaswa.
ALITUMIA KARETI KUJIOKOA!
“Padri alisema kabla ya kudhibitiwa alicheza kareti kwa vile anazijua ili awasambaratishe lakini kwa vile watu hao walikuwa zaidi ya wanne walimzidi nguvu.”
TURUDI KWA OFM
Uwazi liliwageukia wapiga picha wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers na kufanya nao mahojiano kwa kupitia utetezi wa padri huyo.OFM: “Siyo kweli, baada ya walinzi Wamasai kutupigia simu na sisi kwenda pale ulipita muda. Kwa hiyo kama ni msichana kushuka angeshashuka. Pia, wakati wanakurupushwa ndani ya gari, padri alitaka kujua sisi ni nani, tukatoa vitambulisho vya kazi kuonesha ni waandishi wa habari wa OFM.
Kumbe walinzi wale wa Kimasai, waliwapigia simu polisi ambao tulikutana eneo la tukio. Kingine ni kwamba, walinzi walisema gari hilo limekuwa likienda mahali pale mara kwa mara na walikuwa wakilitilia shaka kwamba huenda ni la wahalifu.“Baada ya kuwafumania kichakani na kuwapiga picha, polisi walichukua namba zetu na kutuambia kwamba watakapotuhitaji watatuita, hivyo padri na mrembo huyo tuliwaacha na polisi.”
Padri Anatoly akijistili baada ya tukio hilo.
MASWALI KWA PADRI
Utetezi wa Padri Salawa unapingana na akili za kawaida. Kwamba, aliombwa lifti na mrembo huyo na alikubali! Je, kama angekuwa adui angetambuaje hilo hususan kwa kitendo cha kumwambia aondoke na mtu mwingine wawe watatu lakini msichana akamkatalia!
Pili, kama kweli alivamiwa, kwa nini yeye alikutwa suruali iko nusu mwilini na msichana hana nguo kabisa? (picha zipo) na kwa nini walikutwa kichakani?Tatu, ni jambo la kawaida kwa mapadri kuwa baa, lakini je, ni sawa kila anayetokea na kuomba kupelekwa mahali inakuwa hivyo kweli?

MWANAUME AMNYONGA MKEWE, KISA WIVU WA MAPENZI

Magdalena Lucas enzi za uhai wake.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa majirani wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Benson Boaz alisema, imekuwa vigumu kwao kujua chanzo hasa cha kifo cha msichana huyo aliyekuwa mfanyabiashara ndogondogo, ingawa alikiri kuwa mara kwa mara wanandoa hao walikuwa wakizozana kutokana na wivu uliokithiri wa mwanaume.
MUME ALIKUWA NA WIVU
“Mwanaume ambaye alikuwa fundi ujenzi, alikuwa na wivu uliovuka kiwango kwa Magdalena, alikuwa akimuwekea mipaka kuzoeana hata na majirani, huyu kijana hakutaka na alipomuona mkewe anajichanganya na watu hakupendezwa kabisa,” alisema.
Jeneza lililobeba mwili wa Magdalena Lucas likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
Aliongeza kuwa mara ya mwisho walimuona marehemu Ijumaa ya Mei 8 mwaka huu akiwa na mumewe lakini hawakuwaona tena na hawakuwa na shaka kwa kuwa mlango wao ulikuwa umefungwa kwa nje.
CHUMBA KUTOA HARUFU
“Jumapili jioni tukasikia chumba chao kikitoa harufu kali, ndipo tukapata hofu na kutoa taarifa polisi, walipofika na kuuvunja mlango, wakamkuta dada huyo ameuawa, akionekana kupigwa na kitu kizito kichwani maeneo ya usoni kiasi cha jicho lake kunyofoka. Hatujui kilichotokea maana hatukusikia kelele huenda kwa vile mvua nyingi ilikuwa inanyesha na mwanaume hajaonekana hadi leo,” alisema jirani huyo.
DADA HAMJUI SHEMEJIYE
Dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Asteria alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwenye familia yao kwa kuwa tangu mdogo wake aanze kuishi na Stephano, hakuwahi kuwaonesha ndugu zake.
Mwili ukiagwa kwa ajili ya mazishi.
“Tangu mdogo wangu aanze kukaa na huyo shemeji,  sisi ndugu hatukuwahi kutuoneshwa tukamjua hata kwa sura, lakini majirani walijua kuwa ni mke wake, naumia sana, ni bora asingeamua kuishi naye kwani hakuwa na upendo wa kweli ndiyo maana kaweza kumfanyia ukatili wa aina hiyo,” alisema.
Marehemu ambaye hakubahatika kupata mtoto, alizikwa katika Makaburi ya Tandale kwa Ali Maua lakini ndugu na jamaa hawakupata nafasi ya kuuaga mwili wake kutokana na kuharibika.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura alisema habari hizo hazijamfikia lakini atafuatilia kwa kina tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake.

SHOGA USIMWAMBIE MUMEO UMECHOKA, UTAACHWA!

Mada yangu ni mahususi kwa wenzetu ambao huwanyima waume zao ‘chakula cha usiku’ kwa madai kwamba wamechoka hivyo hawahitaji kusumbuliwa.Kauli hizo zinazotolewa na baadhi ya wenzetu kwa waume zao ndizo zimenifanya nizungumze nanyi kwa sababu zina athari kubwa katika ndoa zetu.
Ngoja niwaulize, hivi unapomwambia mumeo kwamba umechoka na huwezi kumpa chakula cha usiku unafikiri nani atakayempa chakula hicho?Shoga, nafikiri unajua mtu anapokuwa na njaa anahitaji nini ili hali yake iwe sawa, ni wazi kwamba anahitaji chakula, akila utamuona anavyochangamka kwa furaha.
Hiyo ni njaa ya kawaida, sasa inakuwaje kwa mkuu wa kaya ambaye anakuwa amemmisi sana mkewe na kuhitaji kupata naye chakula cha usiku halafu mkewe amwambie amechoka na hajisikii.Bila shaka, atanyong’onyea na ni rahisi kuamua kuitafuta shibe hiyo kwa wanawake wa nje wanaoweza kuwapa chakula hicho bila masharti tena kikienda sambamba na mapochopocho kibao.
Ni kweli unaweza kuwa umechoshwa na majukumu ya nyumbani au ofisini, lakini ni vyema kutumia lugha ya kujiongeza kumuelewesha mumeo ili akuelewe kuliko kumwambia; “Na wewe baba Moza umezidi, kila siku unataka, nimekwambia nimechoka, sitaki sasa!”
Wapo ambao hudiriki kuwaambia kwamba kama wamebanwa sana na njaa wakatafute wanawake wa nje wanaoweza kuwapa chakula cha usiku kila siku.Shoga yangu, kauli za namna hiyo zinaweza kuisambaratisha ndoa yako na mumeo kuamua kutafuta mtu mwingine mwenye kauli nzuri za kujitetea inapotokea amechoka na mumewe kuhitaji chakula cha usiku. Kwaheri!

USIHUZUNIKE KWA KUACHWA, UTAMPATA AKUPENDAE

Huzuni hiyo husababisha wengine kupunguza ufanisi wao wa kazi, wakati mwingine humfanya mtu kuwa dhaifu katika maamuzi na fikra zake, huku wengine wakijiona kana kwamba hawana thamani kabisa katika huu ulimwengu.
Inafikia wakati, wengine huchukia watu wa jinsia ile iliyowatenda, wanaume huwachukia sana wanawake, huku wanawake huwachukia wanaume na kuwasemea maneno mabaya, kwa sababu tu msongo wa mawazo baada ya kuachwa na mwenza aliyempenda.
Kwa sababu ya maumivu ya kuachwa wanayoyapata, maumivu makali kuliko mtu aliyepigwa risasi au aliyejeruhiwa na kitu chenye ncha kali, hujikuta wakitamani kuishi bila kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda, kwa kuamini hata atakayempa nafasi kwa mara nyingine naye atamtenda kama alivyofanya wa mwanzo.
Kwa wakati huo, aliyetendwa huamini hivyo na hata akishauriwa na watu wake wa karibu kwamba mwenza aliyekuwa naye hakupangiwa na Mwenyezi Mungu huwa vigumu kuamini.Huna sababu ya kukata tamaa na kuhuzunika, jipe moyo, amini kuachwa kwako ni sehemu ya maisha ambayo ulipaswa upitie ili ujifunze maumivu hayo.
Ninachoweza kusema na kuamini ni kwamba kama ipo ipo tu, msemo huu una maana ila haiwezi kuwepo kama hutafuti kile unachotaka kuwa nacho.Kama Mungu amepanga wewe kuishi au kuolewa na huyo mtu basi ndivyo itakavyokuwa hata kama ni baada ya miaka 20 ijayo, cha kufanya mwambie Mungu hivi; “kama umepanga niolewe au nimuone mtu huyo na iwe hivyo,  kama hujapanga pia nashukuru.’’
Mtu mmoja aliwahi kunisimulia namna alivyoanza uhusiano na binti mmoja wakiwa na umri mdogo, walipendana sana hadi kufikia kuwekeana ahadi ya kuoana kama wafanyavyo wengine.
Muda ulisonga wakiwa wapenzi katikati ikatokea wakakorofishana na kuachana kabisa, kila mtu akashika hamsini zake, msichana akawa kama kaolewa na mtu mwingine. Siku moja mwenza wake wa zamani alipita jirani na anapoishi msichana yule na kumkuta akifua, alichomwambia ni kuwa ipo siku utakuwa wangu wa maisha.
Siku zikasonga wakiwa mbalimbali, ikaja kutokea siku moja wakakutana na kuanzisha uhusiano mpya kwa  mara nyingine tena.Lakini safari hii uhusiano wao ulikuwa wa nguvu na upendo mwingi, kila mtu akiwa na hamu ya kukutana na mwenziye faragha.
Ndugu, jamaa na marafiki zao waliokuwa wakifahamu walivyoanza kuwa na uhusiano na kufarakana kwao walishangazwa jinsi walivyoweza kurudiana na kupendana kwa dhati.Watu hawa hatimaye walifanikiwa kufunga ndoa na mpaka sasa wana watoto wawili na maisha yanaendelea kwa upendo na furaha tele.
Ninaachoweza kukushauri haijalishi changamoto na misukosuko unayokutana nayo katika uhusiano wako, kama mtu uliyenaye ndiyo chaguo lako kutoka kwa Mungu, ipo siku atarejea kundini hata kama atarukaruka vipi.
Maisha ya mwanadamu ni kama kitabu kilichoandikwa tayari, kinachofanyika kwa wanadamu ni kuperuzi kurasa ili kukamilisha kile kilichoandikwa.

ONA KAJALA ALIVYOJITOA UFAHAMU NA KUACHA WATU HOI

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja akikata mauno.
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni maeneo ya Twende Polepole, Mkoa wa Pwani kwenye sherehe ya kumkaribisha mtoto wa mwigizaji Aunt Ezekiel (Baby Shower) iliyohudhuriwa na watu wengi akiwemo Kajala.
Awali, mwanahabari wetu aliyekuwa akikusanya matukio eneo hilo alimshuhudia Kajala akipata ‘kilaji’ kisha akaitwa na mshereheshaji Maimartha Jesse na kupewa nafasi ya kucheza muziki ndipo alipoanza kuionesha tatuu yake iliyopo bajani kabla ya kuanza kukata mauno.
...akizidi kunengua.
Watu waliokuwepo ukumbini humo walipigwa na mshangao kwani hakuna aliyeamini staa kama huyo alikuwa mahiri wa kuzungusha nyonga.“Yaani ni balaa, sijui ni kuzidisha kilaji au ni vipi, mtoto wa kike kajitoa ufahamu kwelikweli, leo ndiyo amefunika watu wote hapa,” alisema mmoja wa waalikwa.
“Aunt Ezekiel kwa kushirikiana na marafiki zake, waliamua kufanya sherehe kwa lengo la kufurahi pamoja na kumpa mwigizaji huyo zawadi mbalimbali za mtoto wake mtarajiwa.
Mbali na Kajala, sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kadhaa akiwemo Husna Idd ‘Sajenti’ (mwigizaji), Nice Chande (muigizaji), Zamaradi Mketema (mtangazaji) na wengineo ambao nao walicheza muziki, kula na kunywa.

WOLPER ANASWA LIVE AKIINGIA JUMBA LA FREEMASON

Mshtuko! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameibua maswali kwa mashuhuda walimuona ‘live’ akiingia kwenye hekalu la watu wa Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemasons yenye nguvu duniani inayohusishwa na imani za kishetani.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe akiingia kwenye hekalu ilo.
TUJIUNGE MTAA WA SOKOINE
Tukio hilo lililoibua kizaazaa kwa mashuhuda waliomuona Wolper, lilijiri juzikati, mishale ya jioni kwenye hekalu hilo lililopo Mtaa wa Sokoine mkabala na Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar jirani na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
SIMU ZAMIMINIKA
Likiwa kwenye majukumu ya kusaka habari kama kawaida yake, gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa mashuhuda hao wakiwataka wanahabari wetu kuwahi eneo la tukio.
Kufuatia umbali waliokuwa mapaparazi wetu, ilibidi kuwaomba mashuhuda hao ‘kumfotoa’ picha ambapo mmoja wao alifanya hivyo na kuziwasilisha kwenye meza ya gazeti hili.
...akitoka.
ALINASWAJE?
Akidadavua mazingira aliyonaswa Wolper, shuhuda huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza mwanzoni hatukumjua kama ni Wolper lakini kuna dada ambaye anamjua vizuri na ni shabiki wake mkubwa ndiye aliyetuhakikishia kuwa ni Jacqueline (Wolper).
“Kuna waliomuona akiingia. Nilipofika mimi nilimkuta getini anatoka. Walisema hakukaa muda mrefu kwani alitumia dakika kadhaa kisha akatoka na kwenda kwenye gari lake aina ya Prado (Toyota) alilopaki mbali kidogo na lango hilo,” alisema shuhuda huyo kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza:
“Baada ya hapo alitoka nduki maana nzi (watu) walikuwa wameanza kumjalia na kulizingira gari lake.”
WOLPER AJITETEA
Baada ya kuzikagua picha za Wolper akiwa katika mazingira hayo na kujiridhisha kuwa ni yeye, gazeti hili lilimbana mwigizaji huyo ambapo alijitetea:
...akiwa getini.
“Jamani nilikuwa sina hili wala lile. Kuna jengo nilikuwa nalitafuta ndiyo nikajikuta nimetokea maeneo hayo.
“Mimi mwenyewe nilishtuka kuona watu wananiangalia sana kumbe ndiyo nikagundua nipo kwenye lango la Freemasons.”
Risasi Jumamosi: Mbona kuna mashuhuda walikuona wakati unaingia na wakati unatoka?
Wolper: Unajua mimi sikuona kibao chao lakini sikuingia kabisa hadi kule ndani.
Risasi Jumamosi: Lakini kuna madai kwamba wewe ni mwanachama. Unasemaje?
Wolper: Mimi siyo Freemasons, nakumbuka kuna siku watu walinifuata wakaniambia nijiunge Freemasons nitakuwa na mafanikio lakini sijakubaliana nao.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2012 wakati wa kifo cha aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ kuliibuka madai ya baadhi ya wasanii ambao ilisemekana ni ‘memba’ wa Freemasons.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
Mbali na Kanumba, wengine waliotajwa kwenye listi hiyo mwaka huo alikuwepo Wolper na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye madai hayo yamekuwa yakiendelea kumganda huku wengi wakiwa na imani potofu kuwa ukijiunga na jamii hiyo unapata utajiri wa ghafla.

WASANII WANASWA LIVE WAKIFANYA UPUUZI HADHARANI


SHABAASH! ‘Makinda’ wawili wanao penyapenya katika sanaa ya maigizo runingani wa Kundi la Sanaa la Jakaya Theatre Arts Group, Sefu Ngao ‘Stefano’ na Vanessa Msofe wamenaswa wakifanya uchafu kwa kuoneshana mahaba mazito huku wakiwa ‘bwii’, Ijumaa Wikienda linakupa ishu nzima.
Wasanii hao wakiwa katika mahaba mazito baada kulewa.
Tukio la uchafu huo unaotia kichefuchefu cha ‘mimba changa’, lilinaswa na ‘kiona mbali’ cha gazeti hili namba moja kwa skendo na ufuska wa wasanii, waigizaji na mastaa mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Sinza-Legho jijini Dar na kuzua mshangao mkubwa.
Wasanii hao wakiendelea na starehe zao....
Kitendo cha wasanii hao kufanya uchafu huo kisa ulevi, kilikatishwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo.
“Jamani nilipeni hela yangu na muondoke hapa,” alisikika mhudumu huyo aliyekerwa na vitendo vichafu vya wasanii hao.

MUME WA ZARI ANASA KWA SHOSTI WA ZARI PENZI MOTOMOTO

Aliyekuwa mume wa Zari akiwa na mpenzi wake mpya ambaye ni shosti wa kufa na kuzikana wa Zari.
Ubuyu kutoka jijini Kampala nchini humo ulidadavua kwamba, Ivan na Stella ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’, hivi karibuni wamekuwa wakijiachia kimalovee kwa raha zao.
Zari akiwa na shosti wake Stella Nankya ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’.
Tukio la juzikati lililoacha gumzo ni pale wawili hao waliponaswa wakiwa wamegandana kimahaba kwenye Ukumbi wa Ekitone uliopo Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo kulikuwa na tamasha la muziki.
Modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’ Stella Nankya akiwa katika pozi.
“Walikaa pamoja, walijiachia pamoja ziro ‘distansi’ kwani hakukuwa na kitu cha kuwatenganisha kati yao. Kwa kweli walionekana ‘kapo’ ya kupendeza mno,” alisema shuhuda wa tukio hilo na kukaririwa na gazeti moja la nchini Uganda.
Kufuatia urafiki wa Stella na Zari walivyokuwa wameshibana, mashabiki wao wamekuwa na maoni tofauti huku Stella akionekana msaliti kwa Zari.
Habari nyingine zilidai kwamba, Ivan ameamua kufanya hivyo ikiwa kama kisasi au kumrusha roho Zari aliyezaa naye watoto watatu ambapo anatarajia kumzalia Diamond siku chache zijazo.
Ilielezwa kuwa, Stella alipoulizwa kwa nini ameamua kumsaliti rafiki yake Zari kwa kutembea na Ivan alisema kwa kifupi:
“Sitaki kuwa karibu na mtu mkavu (Zari), na mimi nimeamua kuwa mkavu.”
Zari au mama kijacho na Stella walikuwa ni marafiki wakubwa ambapo kuna wakati Zari alimpa sapoti ya nguvu Stella alipokwenda kuiwakilisha Uganda kwenye mashindano ya urembo ya Miss Asia Pacific huko Seoul nchini Korea Kusini ambapo walisafiri wote.