MAJAMBAZI WAKAMATWA WAKITAKA KUIBA KATIKA BENKI YA NMB TAWI LA SINZA-MORI, DAR



Majambazi hao wakiwa wametiwa pingu baada ya kukamatwa na jeshi la Polisi jijini Dar.
...wakiwa chini ya ulinzi.
Wananchi wakiwa eneo la Benki ya NMB Sinza-Mori, Dar wakifuatilia tukio hilo.
Gari walimowekwa majambazi hao wakati wakipelekwa kituo cha Polisi Mabatini, Kijitonyama.
Wakiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar.
Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo.
Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar.

No comments:

Post a Comment