SHOGA USIMWAMBIE MUMEO UMECHOKA, UTAACHWA!

Mada yangu ni mahususi kwa wenzetu ambao huwanyima waume zao ‘chakula cha usiku’ kwa madai kwamba wamechoka hivyo hawahitaji kusumbuliwa.Kauli hizo zinazotolewa na baadhi ya wenzetu kwa waume zao ndizo zimenifanya nizungumze nanyi kwa sababu zina athari kubwa katika ndoa zetu.
Ngoja niwaulize, hivi unapomwambia mumeo kwamba umechoka na huwezi kumpa chakula cha usiku unafikiri nani atakayempa chakula hicho?Shoga, nafikiri unajua mtu anapokuwa na njaa anahitaji nini ili hali yake iwe sawa, ni wazi kwamba anahitaji chakula, akila utamuona anavyochangamka kwa furaha.
Hiyo ni njaa ya kawaida, sasa inakuwaje kwa mkuu wa kaya ambaye anakuwa amemmisi sana mkewe na kuhitaji kupata naye chakula cha usiku halafu mkewe amwambie amechoka na hajisikii.Bila shaka, atanyong’onyea na ni rahisi kuamua kuitafuta shibe hiyo kwa wanawake wa nje wanaoweza kuwapa chakula hicho bila masharti tena kikienda sambamba na mapochopocho kibao.
Ni kweli unaweza kuwa umechoshwa na majukumu ya nyumbani au ofisini, lakini ni vyema kutumia lugha ya kujiongeza kumuelewesha mumeo ili akuelewe kuliko kumwambia; “Na wewe baba Moza umezidi, kila siku unataka, nimekwambia nimechoka, sitaki sasa!”
Wapo ambao hudiriki kuwaambia kwamba kama wamebanwa sana na njaa wakatafute wanawake wa nje wanaoweza kuwapa chakula cha usiku kila siku.Shoga yangu, kauli za namna hiyo zinaweza kuisambaratisha ndoa yako na mumeo kuamua kutafuta mtu mwingine mwenye kauli nzuri za kujitetea inapotokea amechoka na mumewe kuhitaji chakula cha usiku. Kwaheri!

No comments:

Post a Comment