Pole! Msanii wa
sinema za Kibongo, Ummy Mohammed amenusa kifo baada ya kunusurika kwenye
ajali ya Basi la Al-Saeed alilopanda akitokea mkoani Morogoro kwenda
Dar ambapo ameumia mkono wa kushoto.
Akilisimulia Ijumaa Wikienda mkasa mzima, Ummy ambaye ni mwigizaji mkongwe aliyeibuka staa kwenye Sinema ya Mke Mchafu, alisema kuwa basi hilo liligongana na lori maeneo ya Mikese Morogoro na kupondeka.
“Kwa jinsi ile ajali ilivyokuwa sikutegemea kabisa kama ningenusurika kifo, nilikuwa nasali sala ya mwisho, namshukuru Mungu nimeambulia jeraha la mkono japokuwa ninapata maumivu makali ya mwili,” alisema Ummy.
No comments:
Post a Comment