NI matumaini yangu wapenzi wasomaji wa safu hii mko poa. Leo tunamalizia vipengele vilivyosalia wiki iliyopita, ungana nami.
6.Karaha
Hili pia ni tatizo la wanawake ambalo hawapendi kulikubali. Karaha
nyumbani dhidi ya mwanaume huweza kumfanya ajisikie kuhitaji faraja nje
ya nyumba. Na wanawake wengi wakimuona mwanaume yupo peke yake baa,
hujua kuwa atakuwa amekimbia maudhi ya mkewe na anahitaji faraja.
7.Huruma ya wanawake
Hili nalo ni tatizo
linalotumiwa vibaya na wanaume. Wanawake wengi wana huruma na ni wepesi
wa kusamehe makosa ya wenza wao. Hii hutokana ama na woga wa maisha peke
yao, au kutotaka mambo yao kutoka nje, hivyo huwasamehe haraka wanaume
wao hata kwenye makosa ya wazi. Hili huwafanya wanaume kutojali na
kurudia tena makosa yao.
8.Kazi na maumbile
Maumbile ya wanaume yako
katika namna ambayo ni vigumu sana kwao kuvumilia kwa muda mrefu bila
kuhitaji wanawake, hivyo kama wakiwa mbali na nyumbani, hujikuta
wakitamani tendo la ndoa.
9.Uhuru uliopitiliza
Kutokana na kazi, wanaume wengi huwa huru kwenye familia zao, kwa
kuondoka asubuhi na kurudi usiku mwingi. Hii huwafanya kuweza kufanya
lolote wakati wowote bila kuwa na hofu. Ni rahisi kwao kujenga uhusiano
na wanawake wa barabarani au hata kazini kwake.
10. Ushawishi wa wanawake
Ingawa kiasili wanaume
ni watu wa kutongoza, lakini wapo wanawake ambao huifanya kazi hiyo kwa
ajili ya kutaka fedha au kuvuruga uhusiano kwa makusudi. Hutumia mbinu
mbalimbali na wanaume hujikuta wameingia mtegoni bila kujua.
No comments:
Post a Comment