VUNJA
ukimya! Baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu na fununu za kutembea na
wanaume kadhaa tangu kufariki kwa aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko
‘Sajuki’, msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma hatimaye amefunguka na
kujiapiza kwa kulamba kidole, kuchovya mchanga na kukipitisha shingoni
akidai tangu kuondoka kwa Sajuki hajawahi ‘kuchangia shuka’ na mwanaume
yeyote na kama yupo, ajitokeze hadharani!
‘Akibadilishana sentensi’ na ‘kiruka’ njia wetu kwa njia ya simu hivi
karibuni, Wastara ambaye bado anafanya vyema kwenye sanaa, alishutumu
na kuonekana kuchukizwa vikali na tetesi juu yake akihusishwa na wanaume
kadhaa akiwemo msanii mwenzake, Bond Bin Suleiman.
“Nashangazwa sana na wanaoeneza uvumi wa mimi kutembea na wanaume
wengi baada ya kifo cha mume wangu, kwani mimi sina haki kama mwanamke
jamani? Kama kuna mwanaume mwenye uthibitisho wa kutembea na mimi si
ajitokeze!” alisema Wastara huku akiashiria jazba.
No comments:
Post a Comment