MUME AFUKUZWA UKWENI KWA KUSHINDWA KUTOA MATUMIZI KWA WAKWE

Katika sakata hilo, baba Juma inasemekana amekuwa akiishi ukweni hapo ambapo masuala ya msosi wanachangia kwa zamu na familia nzima kila mmoja na siku yake.Kwa mujibu wa chanzo chetu, zamu ya wanafamilia wengine ikifika hununua chakula chenye mvuto kinywani, kama samaki wa Mwanza (sangara, sato) na mapochopocho mengine lakini zamu ya Mwanahamisi, mumewe hutoa pesa ya matembele jambo linalodaiwa lilikuwa likiwakera wanafamilia hao.
Kufuatia kero hiyo, kwa mujibu wa chanzo, wanafamilia hao inadaiwa waliamua kumvalia njuga baba Juma na kumtimua yeye na mkewe na mtoto wao Juma mwenye miaka miwili.
Ni wakati mtafaruku huo wa ‘aondoke huyo’ ukiwa umepamba moto, chanzo chetu hicho kilipiga simu Ofisi za Global Publishers, Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kupasha mchezo kamili na   akusema kuwa timbwili hilo lilikuwa likiendelea ‘laivu’....Bila kuchelewa, mmoja wa makachero wa OFM kwa kutumia pikipiki iendayo kasi, ndani ya dakika chache alifika eneo la tukio na kukuta baadhi ya wanafamilia hao wakiendelea kuwafanyia timbwili Mwanahamisi na mumewe ikiwemo kuwapa vichapo huku wasamaria wema wachache wakijaribu kutuliza.
Bila kuchelewa, paparazi wetu alianza kuwafotoa picha wanafamilia hao huku Mwanahamisi akijaribu kuokoa maisha yake kwa kukimbia huku amembeba mwanaye.Mwanahamisi alisikika akisema hawezi kuhama nyumbani hapo kwa vile nyumba hiyo ni ya baba yake mzazi hivyo ni bora wamtenge kwenye misosi lakini si kumfukuza kabisa.
Utetezi wake ulipingwa vikali na wanafamilia hao hasa mama yao mdogo aliyefahamika kwa jina la mama Hashimu.
Baada ya varangati kuzidi, Mwanahamisi aliona ni heri ambebe mwanaye na kukimbia naye huku mumewe akimfuata kwa nyuma na kwenda kusikojulikana.
Mke wa baba Juma nae akitimuliwa pamoja na mwanaye.
Katika hali ya kushangaza, wanafamilia hao walimgeukia paparazi wetu na kutaka kumfanyia vurugu ikiwemo kujaribu kuvunja kamera yake lakini wakagonga mwamba.Katika sakata hilo, mwanadada mmoja aliyekuwa amesahau kuchana nywele, akiwa amejifunga kanga moja kifuani, nyingine kiunoni huku hana viatu, alimporomoshea matusi paparazi wetu ambayo aliyarekodi.
Kwa vile kisa kilisikika wakati wa mzozo, gazeti hili lilifanya jitihada za kuzungumza na wanafamilia hao ili kusikia kutoka kwao lakini ilishindikana baada ya kukosa ushirikiano kutokana na hasira za kupigwa picha.

No comments:

Post a Comment