Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo, kigogo huyo ni mtu mwenye fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia ambazo gazeti hili linazishikilia zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Mastaa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper sambamba na Jimmy Mgaya.
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, gazeti
hili lilimtwangia simu Wolper na kumsomea mashitaka yake juu ya mwanaume
huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”
Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika ndiye huyo Jimmy.
No comments:
Post a Comment