MADAI, DENTI MIAKA 12 AWEKWA KINYUMBA NA NA MWALIMU WAKE WA KIKE

MWANAFUNZI mmoja wa darasa la sita katika shule moja ya msingi iliyopo Ubungo jijini Dar, aliyefahamika kwa jina la Magida mwenye umri wa miaka 12, mkazi wa Kipawa jijini Dar, anadaiwa kuwekwa kinyumba na mwalimu wake aliyetajwa kwa jina moja la Kimweri katika tukio lililofanyika kwenye nyumba mbalimbali za kulala wageni na kumfanya kushindwa kuhudhuria masomo.
Magida anayedaiwa kuwekwa kinyumba na ticha.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Mary Joseph akizungumza na paparazi wetu alisema, akiamini mwanaye ana umri mdogo na anahudhuria masomo kama kawaida, alishangazwa Machi mwaka huu mtoto wake alipokwenda shule na kutorejea nyumbani hadi siku iliyofuata.
Aliporudi, alidai alisumbuliwa na tumbo na kwamba alipata hifadhi kwa mtu aliyekataa kumtaja.
“Siku iliyofuata usiku saa saba akaniomba funguo aende kujisaidia, alipotoka alikaa muda mrefu bila kurudi, nikamfuata na kumtafuta sikumuona.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Mary Joseph.
Kesho yake nikatoa taarifa polisi kwa kuwa moyo wangu ulijawa hofu nikihisi katekwa usiku ule, siku mbili baadaye limuona kituo cha mabasi Ubungo lakini alinikimbia,”alisema mama huyo na kuongeza:
“Siku iliyofuata nilienda na kuomba msaada wa watu wakamkamata, baada ya kumpeleka Polisi Mawasiliano, akiwa analia alidai kwa kipindi cha mwaka mmoja alikuwa kwenye uhusiano na mwalimu huyo ambaye alimwambia afanye siri na alimkataza kwenda shule, akawa anamsubiri chini ya mti mmoja ambapo alimpitia kila alipotoka kufundisha na kumpeleka gesti tofautitofauti na wakiwa huko, humpatia maswali kisha kumsahihishia, kitu kilichokuwa kigumu mimi kugundua kama alikuwa haendi shule,” alisema mama huyo.
Kamanda Camillius Wambura.
Kaongeza kuwa, cha ajabu siku hiyo waliporudi nyumba alitoroka tena na mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni hakuwa akijulikana aliko.Jitihada za kumpata mwalimu Kimweri ziligonga mwamba kwa kuwa aliacha kufundisha tokea mwaka jana na kuhamia shule nyingine iliyopo Kisarawe ambako pia hakupatikana kwa maelezo kuwa hajaonekana kwa muda mrefu. Jalada la kesi yake limeandikwa SGR/RB/1216/2015 KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.

No comments:

Post a Comment