Kuolewa ni tendo jema. Ni jambo Jema, na kila apataye mke amepata kitu chema.
Kwa maana hiyo kwa haraka sana ninaweza kukuambia maana ya kuolewa ni kwamba wewe msichana umekuwa kitu chema.
Kabla hujaolewa huitwi mke, ni msichana ama mwanamke,, lakini unapoolewa tu unabadilika na kuwa na cheo cha mke.
Na MKE NI KITU CHEMA.
Mahali pengine anasema, .. mali na mashamba mtu hurithishwa na babaye,, lakini mke mwema anatoka kwa Mungu.
Hii inanikumbusha jambo katka uumbaji wa Mungu, Mungu alipoumba
Ulimwengu alikusa akisema iwe inakuwa, lakini alipofikia kwa mwanadamu
AKAUMBA, haikuwa tena iwe,, ila aliumba. Lakini nazidi kufurahi kwa
sababu naona thamani ya mke hapa. Najiuliza kwa nini Adamu hakuumbiwa
mama na baba?? uliwahi kujiuliza swali hili wewe mwanamke?
Maana yake ni kwamba, Mungu alipomuumba mwanamke alimuumba katika
ukamilifu wa hali ya juu kuwa mke. Na ndio maana akasema MKE NI KITU
CHEMA.. kisha MKE MTU HUPEWA NA MUNGU… hii ni kwa sababu Mungu
alimuumba Eva/ Hawa peke yake kwa viwango vya kuwa mke… kukamilika
katika UMKE.
Hivyo ni lazima wewe msichana kabla hujaingia kwenye ndoa ujihakikishie kwamba NI MKE KITU CHEMA NA UMETOKA KWA MUNGU.
Tunaposema mke kitu chema nini maana yake?
Maana yake ni kwamba, KITU KIZURI, KISICHO NAMAWAA, KILICHO NA ADABU,
HESHIMA,UTII,, THAMANI, MVUTO, NA KILA SIFA NZURI… Hii ndiyo maana ya
KITU CHEMA.
Kama utakubaliana na mimi kwamba Mke ni kitu Chema,, basi
utanihakikishia kabisa wewe mwenyewe kwamba nichaguo sahihi la mumeo.
Lakini pia lazima ukubali kwamba,, katika wengi aliowaona wewe ndiye
uliyekuwa MWEMA AMA CHEMA KULIKO WOTE, Na ndio maana
” chema huvikwa pete”
Ingia kwa miguu yote ndani ya ndoa yako ukiamini hivyo,, yes, na ndivyo ilivyo na ndivyo ulivyo.
Wengi wakishaingia kwenye ndoa hujikuta wanabadilika na kuwa tofauti na
maana halisi ya Chema/ Wema. Unajikuta unaanza kupata Ugojwa wa kichaa
cha ndoa… rejea somo la tarehe 7March 2015…
Hapa hapa kwa blog hii ya bembelezahappy women.
Kichaa cha ugonjwa wa Ndoa kinamuanza mtu pale ambapo anashindwa
kujiamini na kujikubali yeye ni kitu chema, ama yeye ni chaguo la
mumewe… ukishakosea ama ukishapoteza kujiamini hapa ndipo sasa matatizo
ya ndoa yanaanza.
Wengi ambao wako kwenye ndoa zao na wamedumu na kuwa na furaha kwenye
ndoa,,, JAMBO AMBALO LIMEWASAIDIA SANA NI KUJIKUBALI WAO NI KITU CHEMA
NA KUMANTAIN HALI YA WEMA KATIKA NDOA ZAO.
Mithali 31:11-12
Mke kitu chema anachofanya hapa ni kuhakikisha mume wake anamuamini.. na
mume atakuamini tu pale endapo utamtendea mema wala si mabaya… na
akishakuamini …WEWE NI JEMBE AMA KOMANDO WA NDOA… Hutakuwa na kitu cha
kukushinda kwenye ndoa,, kwa vile sasa wewe na mumeo ni mwili mmoja..
Mnaambatana… Mtakuwa mwili mmoja….
Hatua ya kwanza ni kumuacha baba na mama…..
Hatua ya pili ni Kuambatana… ….
Hatua ya tatu… ni kuwa mwili mmoja……..
Huwezi kuambatana na mumeo kama hujaamua kuacha mengine…
Hivyo INGIA KWENYE NDOA YAKO UKIWA UMEMAANISHA KUAMBATANA NA MUMEO.. KUIAMBATA NDOA YAKO…
Ukifanikiwa katika hili eneo basi wewe utaweza kuiendesha ndoa yako… kwa
sababu ya urahisi upatikanao kwenye … kuambatana na kuwa mwili mmoja…
lakini je unamaanisha kuolewa kweli? Unamaanisha kuwa mke wa mumeo
kweli? Unamaanisha kuambatana naye na kuacha kila kitu kweli?
Unamaanisha kuwa mwili mmoja naye?
NINI KINAMVUTIA MUME? Ni kuona..
Umeacha yote nayeye sasa amekuwa sehemu ya maisha yako.
Kuona unaambatana naye..
Kuona mmekuwa mwili mmoja…
MOYO WA MUMEO UKISHAKUAMINI BASI… hutakaa useme..
1. Ndoa ndoano.
2. Wanaume wote ni mbwa.
KOMAA ,,,, Sasa sio msichana tena,, ni mke wa
Fulani, mama…. Ni lazima ujue na uwe na uwezo wa kujiendesha mwenyewe na
kuiendesha ndoa yako ama nyumba yako… Kila kinachofanyika kwako wewe
ndiye mhusika wa kwanza kuhakikisha mambo yanakuwa shwari,,, Hemaya yako
inakutegemea sana wewe katika kuijenga utakavyo…
Unaolewa na mtu ambaye ana mawazo yake, taratibu zake, tabia zake.. sasa
ni lazima uhakikishe unakuwa kitu chema ili sasa mfaidiane,,,
mfurahiane,,, majukumu yako ni mengi sasa..
Kwanza kuweza kumsoma mumeo na kujua hapendi nini na anapenda nini.
Kurekebisha tabia usizozipenda zitoke ili zibaki unazozipenda.
Kuchochea nguvu kwenye tabia uzipendezao ili zizidi kukupendeza zisiishe… HIZI NDIZO KAZI ZAKO SASA.
Na unapokuwa mvivu ama mzembe Ndoa itakushinda haraka sana na kuanza
kuwa wale waimbaji wa ule wimbo wa Wanaume wote ni Mmbwa… lakini sio
kweli… “ men are not dogs”
kwa nini wanaume wote sio mmbwa? hao hao ambao wanaachika kwenye ndoa
zao hujikuta wakiwa na mahusiano na wanaume tena,, je hao wanaume
wanaokuwa nao tena ni mmbwa?
KOMAA … WEWE NI KITU CHEMA….
Ili uwe na ndoa yenye furaha na amani, ni lazima ujikite kwenye kujua
wajibu wako na kuufanya. Ni lazima ndoa yako uijenge kwenye misingi
imara ama nguzo imara zifuatazo:
KUUJUA WAJIBU A.
KUUJUA WAJIBU B.
KUUJUA WAJIBU C.
Wajibu hizo ziko katika group la Nakufunda Tayari kwa Ndoa. katika
face book. Huko tumeziongelea wazi wazi na kwa uelewa zaidi na
kujimwaga zaidi.
No comments:
Post a Comment