RAY, DAVINA HAPATOSHI NUSURA WACHAPANE HADHARANI

HAPATOSHI! Mkongwe wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na mwigizaji mwenzake, Halima Yahaya ‘Davina’ nusura wazichape kavukavu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar baada ya Ray kudaiwa kumshika mwenzake huyo sehemu nyeti, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
 
Staa wa Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray alipofika na kuharibu shughuli.
“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Halima Yahaya ‘Davina.
“Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.
Baada  ya kupata habari hiyo, gazeti hili liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Davina.
“Jamani mi nafikiri nisizungumzie hilo tukio maana naona ni la aibu, si kitendo kizuri na kinaniumiza mno kwa maana ni udhalilishaji mno na kwa nini mtu akufanyie hivyo?,” alisema Davina. Simu ya Ray iliita bila kupokelewa

No comments:

Post a Comment