EFM KUPAMBA MIAKA 16 YA JUMA NATURE KWENYE MUZIKI

IKIWA ni siku chache tangu kituo cha Redio Efm cha jijini Dar kitimize mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake, kwa kutambua mchango wa msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Juma Kassim ‘Juma Nature’, uongozi wa redio hiyo umeandaa sherehe ya pamoja ya wao kutimiza mwaka na miaka 16 tangu staa huyo aanze kuimba muziki huo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Efm, Mikocheni jijini Dar, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Redio Efm, Dennid Sebbo, alisema wameamua kuunganisha sherehe zao pamoja na ya msanii mwishoni mwa mwezi huu kwa kuwa wanatambua umuhimu wake katika burudani.
“Sisi kama Efm ni wadau wakubwa wa muziki pamoja na wasanii, hivyo basi tumeona ni vema kufanya sherehe hizi kwa Tamasha la ‘Komaa Concert’ kwa sababu kwetu muziki ni nyenzo kubwa ya burudani na Juma Nature ni mmoja wa waasisi wakubwa wa muziki,” alisema Sebbo.
(Habari/Picha: Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata/ Gpl)

No comments:

Post a Comment