DIAMOND ASAKWA MAZISHI YA BABA WA BABU TALE BILA MAFANIKIOA

BABA mzazi wa Meneja wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amezikwa juzi Jumanne kijijini kwao Mkuyuni, mjini Morogoro lakini miongoni mwa mambo ya kushangaza ni kitendo cha baadhi ya waombolezaji kumsaka mwanamuziki Nasibu bila mafanikio.
Staa wa Bongo fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Hilo lilijitokeza baada ya msafara uliotokea Dar kufika eneo hilo ambapo vijana walilizingira gari lililokuwa na mastaa na kuanza kuuliza juu ya uwepo wa Diamond.Vijana hao waliotarajia kumuona msanii huyo msibani hapo, hata waliposikia tetesi kuwa hakuwepo, waliendelea kumsaka kila gari huku wakimuuliza kila waliyemuona lakini jibu lilikuwa lilelile, hakufika.
Majibu hayo yalionekana kuwanyong’onyesha vijana hao ambapo baadhi waliamua kuondoka kuonesha dhahiri kuwa kilichowapeleka pale ni kumuona Diamond na si kuzika.Hata hivyo, vijana wengine waliamua kujipoza kwa kupiga picha na Madee kisha kushiriki mazishi hayo mwanzo mwisho.

No comments:

Post a Comment