WIZI WA WATOTO WADOGO WATIKISA MOROGORO




WIZI wa watoto unazidi kutikisa mkoani hapa ambapo baada ya mwanamke Martha Masawe kuibiwa mwanaye mchanga katika Kliniki ya Nunge Ijumaa iliyopita, Wema Joseph (pichani), mkazi wa Manzese naye ameangua kilio hadharani baada ya kuibiwa mwanaye wa kike aitwaye Elizabeth mwenye umri wa miaka miwili.
Mtot Elizabeth aliyedaiwa kuibiwa.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea kwenye saluni ya kike ambayo ipo jirani na nyumba ya Wema wakati mtoto huyo alipokuwa akicheza ndani ya saluni hiyo.Kwa mujibu wa Wema, wakati tukio linatokea yeye alikuwa anapika ndani huku mwanaye akiwa anacheza nje na alipotoka hakumkuta ndipo alipokwenda kumuuliza dada anayefanya kazi katika saluni hiyo ambaye alimueleza kuwa aliondoka na mteja ambaye hakumfahamu.
Wema Joseph mama wa Elizabeth.
“Mimi nilikuwa napika, mwanangu alikuwa anacheza nje, chakula kilipoiva nilitoka nje kwa lengo la kumchukua ili akale lakini sikumuona.
“Nilipomuuliza mfanyakazi wa saluni akasema kuna mwanamke mmoja alifika hapo kusuka na kabla ya kusuka alikodi bodaboda na kumwambia anakwenda kuchukua pesa ya rasta kwa bwana’ke maeneo ya Masika, hivyo aliomba kwenda na mwanangu na huyo mfanyakazi wa saluni bila kunishirikisha alimkubalia, akaondoka jumla na mwanangu,” alisema Wema huku akiangua kilio.
Martha (aliyekuwa kulia) aliyeibiwa mtoto kliniki .
Baadaye Wema na ndugu zake walifika Kituo Kikuu cha Polisi cha Morogoro na kuripoti tukio hilo ambapo jeshi la polisi lilimshikilia mfanyakazi wa saluni kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.Baadhi ya mashuhuda wa tukio tukio hilo walidai matukio ya kuiba watoto yameshamiri mjini hapa kutokana na ongezeko la wanawake ambao hawajabahatika kupata watoto.

No comments:

Post a Comment