ODAMA ATAKA WENZAKE WAJITUME WAACHE MASHINDANO

STAA ambaye ni mtafutaji anayemiliki Kampuni ya J-Son Film, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amewataka mastaa wenzake wa kike kujituma kufanya kazi, kwani ndiyo siri pekee ya kuwaepuka wanaume wakware wanaotumia fedha kuwarubuni kirahisi.
Staa ambaye ni mtafutaji anayemiliki Kampuni ya J-Son Film, Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Akipiga stori na gazeti hili, Odama alisema wanaume wakware wakiona staa wa kike anapiga mzigo, wanaogopa hata kumsogelea wakijua wazi watashindwa kwani mara nyingi hutumia fedha kuwarubuni, hivyo wakiona mtu anatafuta pesa kwa jasho lake wanakaa naye mbali.
“Mastaa wa kike wanaojituma wanaogopwa na wakware na nimejifunza kwamba mtu ukijituma heshima huwa kubwa, hata wanaume wanaodhani ukiwa na pesa unamnasa staa yeyote unayemtaka kirahisi, wananywea, wanashindwa kueleza utumbo wao, kwa hiyo nawasihi mastaa wenzangu waamke ili wanaume wasitufanye daraja lao,” alisema Odama.

No comments:

Post a Comment