DUDE ASEMA KUZAAZAA NIMERITHI KWA BABA ANA WATOTO 7 SASA TOKA KWA WANAWAKE 4 TOFAUTI

STAA wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa tabia ya kuzaa watoto wengi na kwa wanawake tofauti amerithi kwa baba yake kwani alikuwa na watoto kumi na tatu.

Staa wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akipiga stori na gazeti hili, Dude alisema kwa sasa ana watoto saba kwa wanawake wanne tofauti na bado ataendelea kuongeza watoto wengine kwani haoni shida kwa sababu hata baba yake alikuwa ‘harembi’.
“Nina watoto saba kwa wanawake wanne tofauti, ikitokea nimempenda mwanamke nitamuoa, Eva atakuwa mkubwa,” alisema Dude.

No comments:

Post a Comment