TAUSI AMPAGAWISHA MWARABU

MSANII wa filamu za vichekesho, Tausi Mdegela amempagawisha kwa mauno mwanaume mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, mwenye asili ya Kiarabu na kuzua mishangao na miguno kutoka kwa wadau na mashabiki wa burudani.
Mwarabu akimkumbatia msanii wa filamu za vichekesho, Tausi Mdegela.
Kioja hicho kilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha Club, Oysterbay jijini Dar kulikokuwa na shoo ya Mrs. Mabeste Charity iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa filamu na muziki.
Katika hali ya kushangaza zaidi, Mwarabu huyo alipanda jukwaani hapo na kumtuza kabla ya kumkumbatia na kumganda kwa muda mrefu kama ruba huku akionekana kumnong’oneza hali iliyozua miguno na maswali mengi.

No comments:

Post a Comment