ALIYEZAA NA ASKOFU WA KKKT ATAKA D.N.A

MAPYA tena! Lile sakata la Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera kudaiwa kuzaa watoto wawili na muumini wake, Peace Sylvester limeendelea kuchukua sura mpya kufuatia mwanamke huyo kumtaka askofu wakapime D.N.A.
Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera.
Mbali na madai hayo, naye baba mzazi wa Peace, mzee Sylvester Katoto (72) ameibukia jijini hapa na kumtaka askofu huyo kujitokeza hadharani na kuikana damu yake hiyo mbele yake.Akizungumza hivi karibuni na gazeti hili jijini hapa, mzee Katoto alisema ameamua kufika Arusha akitokea Karagwe kumsaidia binti yake huyo na kuongeza kwamba amesikitishwa sana kwa taarifa kuwa Askofu Bagonza amewatelekeza watoto wake.
“Nimeamua kuyasema haya ili jamii ijue. Bagonza aliwahi kuja kwangu (Karagwe) baada ya Peace kujifungua mtoto wake wa kike na kunieleza kuwa, yeye ndiye mhusika  wa mtoto huyo na aliniomba nimtunzie siri kutokana na wadhifa alionao kikanisa.
“Ninachotaka Bagonza ajitokeze ana kwa ana na ayakane hayo maneno aliyoniambia, pia nataka aikane damu ya hawa watoto hapa hadharani,’’ alisema.Mzee huyo aliongeza kusema kwamba, yeye na watoto wake watatu wa kiume waliamua kufunga safari mpaka Arusha kukanusha barua iliyoandikwa na mtoto wake (jina tunalo) ikisema kwamba, ukoo umemtenga Peace kufuatia sakata lake na askofu huyo kurindima kwenye vyombo vya habari.
Peace anayedaiwa kuzaa na askofu.
“Tutakwenda Ustawi wa Jamii kupeleka malalamiko yetu ili waone uwezekano wa kumwita askofu. Nimejaribu kumpigia simu na kumtumia ujumbe wa maneno (SMS) lakini hajanijibu hadi sasa.“Lengo letu ni kuhakikisha Peace anapata haki yake na si vinginevyo, pia namtaka askofu kuacha kuwatumia watu wengine katika suala hili ila ajitokeze ili azungumze na mimi,’’ alisema mzee Katoto.
Katika hatua nyingine, Peace ambaye ndiye mlalamikaji alimtaka mtu aliyenukuliwa na gazeti moja la kila wiki (si la Global Publishers ambayo ni makini) akidai watoto hao ni wake, ajitokeze hadharani na awe tayari kwenda kupima kipimo cha vinasaba (D.N.A) ili kubaini ukweli.
“Pia namtaka Askofu Bagonza twende wote tukapime kipimo hicho kitakachothibitisha kuwa watoto hawa baba yao ni yupi na nasisitiza askofu ajitokeze hadharani aikane damu yake kama anaweza,” alisema Peace.Peace alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, wiki iliyopita askofu mmoja wa kanisa hilo mkoani Kagera (jina tunalo) alimfuata Arusha  kwa ajili ya kushughulikia suala hilo.
Alisema askofu huyo alimwambia asiendelee tena kulitangaza jambo hilo kwani linashughulikiwa hatua ambayo Peace alisema hadi sasa hajapata mwafaka badala yake ameona kwenye gazeti moja la wiki kuwa aliyezaa na Peace ni mwanaume mwingine ambaye alidai hamfahamu na kudai kwamba amepandikizwa ili kuiaminisha jamii.
Baba wa Peace.
Peace kwa sasa  anajipanga kulifikisha suala hilo Ustawi wa Jamii na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa ajili ya msaada zaidi na ameiomba jamii na taasisi zinazotetea haki ya mwanamke zijitokeze kumsaidia ili haki ipatikane.
Alimlaumu kaka yake mmoja kwa kitendo chake cha kumvamia na kumpiga baba yake na ndugu zake hapo nyumbani kwake baada ya kukataa ushawishi wake kuhusu kuegemea upande wa askofu.
Gazeti hili lilimtafuta Askofu Bagonza kwa njia ya simu ambapo alipokea na baada ya mwandishi kijitambulisha alikata simu na alipopigiwa tena alipokea mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake ambaye alisema askofu alikuwa bize.
Katika Gazeti la Ijumaa Wikienda (ndugu na hili), toleo la 407, Aprili 20-26, 2015, ukurasa wake wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; AIBU…ASKOFU KKKT APIGA MIMBA MBILI NJE YA NDOA.
Katika habari hiyo, Peace alimlalamikia askofu huyo kwa kumzalisha watoto wawili, Piana (6) na Bariki (3) lakini amewatelekeza.Alisema kufuatia hali hiyo, alimfungulia askofu mashitaka katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha na kunukuliwa katika jalada lenye kumbukumbu Na.  AR/RB/5290/2015 KUTELEKEZA FAMILIA.

No comments:

Post a Comment