UBAYA KWA UBAYA NAY NAYE ASALITIWA NA SHAMSA FORD

Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford akipozi kimahaba na Rammy Galis.
Ishu hiyo ‘ilidakwa’ na ‘balozi’ wa gazeti hili  usiku wa Jumapili iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha, Masaki jijini Dar kulipokuwa na onesho la Mrs. Mabeste Charity hafla iliyokusanya mastaa kibao na watoto wengi wa mjini.
Katika pitapita zake huku akikodoa macho kila kona ndani ya ukumbi huo, mwandishi wetu alibahatika kuwaona wawili hao wakiwa wamegandana kwa staili ambayo si ya kujadili katiba mpya huku ukaribu na kutazamana kwao kukiwa na maswali mengi kuliko majibu.
...Wakisakata rumba.
Hata hivyo, umbali wa mkao wao ulianza kupungua kila dakika moja ilipopita wakawa wanabadili mapozi yakiwemo kutazamana kimahaba na kushikana kwa kujitawala.
Baada ya kuhakikisha kuwa amepata picha za ushahidi wa kutosha, mwandishi wetu aliwafuata wawili hao na kumuuliza Shamsa kama huyo ndiye mbadala wa Nay, akamwambia mwandishi kuwa haikuwa kazi yake kujua kwani pale walikuwa eneo la starehe hivyo hawakutaka bughudha na karaha yoyote.
Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
“Ebwana ee, mbona hivyo jamani? Siyo kazi yako kujua huyu ni nani kwangu, ni msanii mwenzangu na hapa tuko kwenye sherehe na hatuhitaji usumbufu wowote,” alisema kwa mkato Shamsa.
Kwa upande wake Galis, alisema hana cha kusema kwani hakuwa eneo la mahojiano.
“Kaka huyu ni msanii mwenzangu na hapa si sehemu ya mahojiano,” alijibu.
Nay alipopigiwa simu alisema: “Hawa wanawake wa Bongo Muvi utawaweza! Ila nitadili naye.”

No comments:

Post a Comment