HUU NDIO WASIWASI WA MASTAA KUHUSU SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliipitisha sheria ya makosa ya mitandao kwa kutia saini.Ni sheria ambayo wengi hawajajua namna itakavyofanya kazi na huenda wengi wakaingia kwenye mtego.

Jaqueline Wolper.
Miongoni mwa watu watakaojikuta kwenye wakati mgumu kupitia sheria hii ni mastaa, tena hasa wa kike. Je, wao wanaizungumziaje sheria hiyo? Hebu wasikie hawa baadhi ya wasanii wa kike…

Jaqueline Wolper
Hii sheria sijaielewa, ila kwa kusikiasikia tu naiona kuwa ni nzuri, itatusaidia sisi wasanii na kutokomeza hayo ‘matimu’ maana tumechoka kutukanwa.
Maimartha Jesse
Nimeipenda, nimeielewa ndiyo vizuri tunakuwa na haki zetu kwani tumechoka hasa sisi wanawake. Mtu anakupiga picha mkiwa faragha kisha anazitupia mtandaoni, busara iko wapi? Ila kile kipengele cha kutumiwa picha naiomba serikali ikiangalie upya, mkosaji abaki kuwa mkosaji tu.
Aunt Lulu.
‘Aunt Lulu’
Sijui chochote, natukana tu na hakuna atakayenifanya lolote. Watu unakuta wanakuchokoza hata hujafanya lolote baya, siwezi kukaa kimya kwa kweli.
Wastara Juma
Dah! Mimi naona imekuja kutubana sisi wasanii, naiomba serikali iwafuatilie na wale wasiokuwa na majina ambao wanapenda kutukana watu wasiokuwa na hatia.
Miriam Jolwa ‘Kabula’
Nimeifurahia sana kwani kuna watu wananyanyaswa sana huko mitandaoni. Mimi naona kwa sheria hiyo itaongeza adabu mtandaoni kwani kila mtu ana haki ya kutumia mtandao na akawa happy bila matusi.
Rose Ndauka.
Rose Ndauka  
Kwa kweli sijaijua kiundani ila nina imani itasaidia kuwabana wale ambao wanatumia mitandao ndivyo sivyo.

No comments:

Post a Comment