Awali, mwandishi wetu alimshuhudia Manecky ukumbini humo akiwa mpole kwa mapozi ya ‘kusikiliza misa’ kabla ya jicho la ‘kiranja’ wetu halijamuona Rose Ndauka.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye, Rose alitinga na kinguo cha kutafunia bata huku akionekana amechangamka kwa ‘ulabu’ (pombe), sanjari na rafiki zake.Kama kawaida yake, akiwa na akili za usiku, Rose alianza kupita sehemu tofauti ukumbini humo huku akionekana kumchangamkia kila aliyekuwa mbele yake.
Kama haitoshi, muda mwingi alikuwa akiutumia kucheza kila muziki uliopigwa huku mauno yake yakionekana kuwaumiza wanaume wakware.Baadaye, Rose alimfuata Manecky aliyekuwa amekaa kwa kujiegemeza ukutani kwenye moja ya kona iliyojificha huku akipata ‘mbili tatu za baridi’.
Ule utulivu wa awali aliokuwa nao Manecky kabla ya Rose, ulianza kuwa msamiati mgumu kwani walichangamkiana huku wakioneshana mapozi ya kiuchokozi ikiwemo kushikana bila kuwa na nidhamu ya mikono.Akiwa anajua anachokifanya ukumbini kwa usiku huo mnene, haraka mwandishi wetu aliseti kamera yake na kuanza kuwanyemelea lakini kabla hajafanya chochote, Rose alikurupuka huku akimuita mwandishi wetu na kumsihi asipige picha.
“Usijaribu kupiga picha kabisa, tutakosana na kuharibiana sasa hivi,” alisikika Rose kwa sauti iliyojaa hasira lakini haikumzuia mwandishi wetu kutekeleza majukumu yake.
Staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
Baada ya kupiga picha kwa shida, mwandishi wetu aliwafuata na
kuwauliza kama wameamua kuanzisha ‘edeni’ yao ambapo Rose alionekana
kuwa msemaji mkubwa kwa kumfokea mwandishi wetu na kukwepa swali la
msingi huku Manecky akiwa kimya.Hata hivyo, wawili hao waliachana kwa
kila mmoja kushika njia yake huku Rose akiambatana na rafiki zake na
Manecky kuendelea na ‘hamsini’ zake.
No comments:
Post a Comment