MASTAA WA KIUME WALIOBAKIZA MAJINA MJINI

WAPO mastaa ambao huko nyuma walikuwa maarufu sana kutokana na kazi zao. Walianza kuvuma tangu enzi zile za Kaole Sanaa Group, Splendid, Nyota Ensemble na Kidedea wakatesa kwenye maigizo yaliyorushwa kwenye TV kisha wakahamia kwenye filamu lakini cha ajabu sasa hivi hawasikiki kivile, wamebaki majina tu.
Wasanii hao wako wengi lakini katika makala haya utapata kuwajua baadhi yao ambao hata wewe msomaji utakubaliana nami kwamba, hawavumi kama zamani.
Mahsein Awadh Dr.Cheni.
Dr.Cheni
Anaitwa Mahsein Awadh, ni msanii mkongwe ambaye kwa sasa anajishughulisha sana na biashara na ushereheshaji (MC) kwenye harusi mbalimbali.Jina lake linambeba hapa mjini, si kwamba ameacha uigizaji bali kwenye fani hiyo amebakiza jina tu kwani hana kiki za filamu kama ilivyokuwa zamani.
Mike Sangu
Aliibukia kwenye Kundi la Maigizo la Nyota Esemble, aliwahi kuwa mume wa Ummy Mpallu ila sasa ni mume wa Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’. Hapo nyuma alitikisa sana alipokuwa katika kundi hilo na wenzake kama JB, Monalisa, Natasha, Mashaka na wengineo.Kwa sasa haonekani sana kwenye fani yake ya uigizaji, naye ni msanii mkongwe aliyebakiza jina tu.
Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’.
Chekbudi
Anaitwa Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’, alitokea kwenye kundi la filamu la Splendid pamoja na wenzake kama vile Dude na
Cloud.
Walitikisa sana enzi zile, yeye akiwa anaongoza na alikuwa hakauki magazetini kutokana na skendo za kugombewa na wanawake hasa kwa kuoa na kuacha.
Bishanga Bashaija
Ni msanii mkongwe wa siku nyingi ambaye aliuteka ulimwengu wa sanaa lakini sasa amebakiza jina tu, ukilitaja jina lake hakuna asiyemjua.Alikuwa akiigiza kwenye Kundi la Maigizo la Mambo Hayo ambapo aliigiza na wasanii kama vile Waridi na Aisha.
Jengua
Jina lake halisi ni Mohammed Fungafunga, aliwahi kuwashika mashabiki wa maigizo enzi zile lakini hata alipohamia kwenye filamu za Kibongo, alikuwa moto wa kuotea mbali.Kuna wakati alipotea kabisa lakini hivi karibuni amerejea kwenye filamu ila hawiki kama zamani, naye limebaki jina tu.
Mhogo Mchungu
Utakumbuka alivyokuwa moto wa kuotea mbali enzi zile za Kaole na hata alipohamia kwenye filamu alionekana kutaka kurudi kwenye ‘pick’ lakini ameshindwa.
Kwa sasa anaonekana kwenye tamthiliya zinazorushwa kwenye Televisheni za TV One na TBC1 pamoja na kwenye filamu chache.
Tito
Huyu naye ni msanii aliyewahi kuwashika mashabiki lakini ustaa wake umepotea kwa sasa na kubakiza jina tu. Bado anajaribujaribu kwenye filamu lakini hazimfanyi awe juu kama zamani alipokuwa Kaole.
Mastaa wengine ambao nyota zao zinaanza kufifia ni pamoja na Dino, Tino, Mlela na wengineo ambao huenda kuna kazi nyingine wanafanya zinazowafanya wawe bize.Hata hivyo, wasanii hawa na wengine ambao hawawiki kama zamani kama wataamua kurudisha umaarufu wao nafasi wanayo kwani mwisho wa sanaa ni pale msanii husika anapofariki.

No comments:

Post a Comment