NISHA AFANYIWA KITU MBAYA NA VIBAKA ABAKI ANALIA TU

MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na vibaka ambao walivunja  gari lake na kuchukua vifaa mbalimbali na fedha dola elfu moja za Marekani sawa na shilingi 1,900,000 za Kitanzania.
Mwanadada anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Akielezea tukio hilo, Nisha alisema lilitokea usiku wa saa tisa Jumapili iliyopita ambapo  watu wapatao watano waliruka ukuta na kuingia ndani na kuvunja gari lake aina ya Toyota Harrier na kuchukua vifaa kibao zikiwemo taa na side mirror.
Mbali na kuchukua vifaa hivyo, pia wahalifu hao walichukua dola elfu moja alizokuwa amezisahau kwenye gari kabla ya majambazi hao kukimbia baada ya Nisha na mfanyakazi wake kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani zao.
“Dada ndiye alinishtua, aliniambia kuna watu wanavunja gari, nilipochungulia dirishani nikawaona kama watano hivi, tukaanza kupiga kelele za kuomba msaada, tukawaona wanakimbia na kupakia kwenye gari lililokuwa nje wakatokomea,” alisema Nisha.
“Kweli nimeumia sana, inaonesha watu hawa walikuwa wananifuatilia maana nilichelewa kurudi nyumbani na muda mfupi tu baada ya kurudi ndiyo na wao waliingia, inauma sana,” alisema kwa majonzi msanii huyo.

No comments:

Post a Comment