ANG’OLEWA JICHO, AKUTA MAFURIKO YAMEIKUMBA NYUMBA

Mohamed Omary akiwa na bandeji jichoni.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Omari alisema kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na tatizo la jicho na amejaribu kupata matibabu katika hospitali kadhaa mkoani Lindi bila mafanikio, kabla ya ndugu na jamaa zake kumshauri kwenda Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
“Baada ya kufika Muhimbili walinifanyia uchunguzi na wakagundua kuwa ana tatizo la kansa ambalo liliwafanya wanihamishie Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambako nilipofika na kufanyiwa vipimo, nikafanyiwa upasuaji wa kulitoa kabisa,” alisema.
Alisema baada ya kufika nyumbani hapo akiwa na maumivu ya upasuaji na kukuta mafuriko, jicho lake liliuma mara mbili kwani alikosa sehemu ya kupumzika kama alivyoshauriwa na madaktari.
“Hali yangu kimaishi ni mbaya, sina pesa ya kunisaidia kujikimu kwani nipo tu kwa ndugu yangu hapa Magomeni, sina namna ya kujisaidia hata katika kupata tiba ya kidonda cha jicho langu, ninaomba mwenye uwezo anisaidie,” alisema mwananchi huyo.Kwa yeyote aliyeguswa na matatizo ya Omary anaweza kumpata kupitia namba 0784619470 ambayo ni ya nduguye alikofikia.

No comments:

Post a Comment